Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Kwa nini yeye asijue kusoma halafu wengine wajue wakati wapo kwenye mazingira sawa?
Tatizo lako hujui kufikiri kidhahania.

Mfano wangu una familia moja tu.

Baba kamuweka mtoto katika mazingira ambayo kushindwa kujua kusoma ni lazima. Hakuna shule.

Wakati aliweza kumuweka mtoto katika mazingira ambayo kuna shule.

Halafu mtoto akishindwa kusoma, utamlaumu mtoto kashindwa kusoma au utamlaumu baba kamuweka mtoto katika mazingira ya kutoweza kujua kusoma?

Kati ya aliyeumba uwezo wa ubaya kufanyika, na anayefanya ubaya tu kwa sababu kajikuta yupo katika ulimwengu ambao ubaya unaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa hapo?

Kati ya aliyeumba ulimwengu ambao mtu mmoja anaweza kumuua mwingine, ule uwezo wa mauaji kufanyika, na mtu anayefanya mauaji kwa sababu ulimwengu unaruhusu mauaji kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi hapo?
 
Halafu mtoto akishindwa kusoma, utamlaumu mtoto kashindwa kusoma au utamlaumu baba kamuweka mtoto katika mazingira ya kutoweza kujua kusoma?
Kwa nini wenzie wajue kusoma na yeye ashindwe wakati wapo mazingira sawa
Kati ya aliyeumba uwezo wa ubaya kufanyika, na anayefanya ubaya tu kwa sababu kajikuta yupo katika ulimwengu ambao ubaya unaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa hapo?
Kwa nini wenzie wasifanye huo ubaya na yeye aufanye
Kati ya aliyeumba ulimwengu ambao mtu mmoja anaweza kumuua mwingine, ule uwezo wa mauaji kufanyika, na mtu anayefanya mauaji kwa sababu ulimwengu unaruhusu mauaji kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi hapo?
Kwa nini wenzake wasiue halafu yeye aue na wakati wote wapo ulimwengu mmoja?
 
Kwa nini wenzie wajue kusoma na yeye ashindwe wakati wapo mazingira sawa

Kwa nini wenzie wasifanye huo ubaya na yeye aufanye

Kwa nini wenzake wasiue halafu yeye aue na wakati wote wapo ulimwengu mmoja?
Maswali yako ya "kwa nini wenzie" yanaonesha hujaelewa mfano, hujaelewa swali, hujaelewa chochote cha msingi.

Ungeelewa, ungejua kuwa swali la wenzie halitakiwi kuwepo.

Kwa sababu hakuna wenzetu walio katika ulimwengu usioruhusu mabaya.

Ni vigumu kujadiliana nawe na kuhojiana nawe kimantiki kwa sababu uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana.

At this point you just bore me.
 
Kwani Uislamu ni nini? na madhehebu yake ni yapi?

Ukiweza kujibu hilo, basi hapo tutajua kama Shia ni Islam au sio Islam.
Uislamu ni dini ya kumtii au kumnyenyekea Allah kwa kufuata maamrisho na makatazo yake

Madhehebu yake ni Hanaf,Malik,Shafi na Hanbal
 
Kwa sababu hakuna wenzetu walio katika ulimwengu usioruhusu mabaya.
Kwani katika ulimwengu huu ni wote wanafanya mabaya?

Mimi ninaposema "wenzake" namaanisha wale ambao hawatendi mabaya
Kwa hiyo huwezi kumtetea eti hana kosa kwa kuwa ameletwa kwenye ulimwengu wenye mabaya na wakati kuna wenzie hawatendi hayo mabaya katika ulimwengu huohuo.
 
Waislam katika nchi ya Iran ni kama asimilia 40%, Kumbuka hao sio Waarabu wana utanadunia wao wa kale na kale kama Persian culture. Hao unaowaona wanatawala kwa kivuli cha dini ni jamii tu kama BAKWATA kwa hapa bongo ipate madaraka. Kwa hiyo maelezo yako yote ni ya uongo na yamejaa ujinga na kukosa taarifa sahihi.
Duuh, kwamba Muslim Iran ni 40% tu 🤔

Sina hakika na hili, ila nadhani ni zaidi ya hapo.
Dini haifati rangi ya ngozi, kuwa Mwarabu haifanyi kwamba wewe ndo muislamu.
Islam ni dini, dini sio rangi ya ngozi, ni imani.

Unaweza kuwa rangi ya ngozi ni mzungu ila Kiimani ukawa Buddha au Hindu.

So, Iranians kuwa waarabu au kutokuwa waarabu (watu wenye vinasaba ya penisula ya Arabia) haihusiani na wao kuwa Islam au kutokuwa Islam. (I repeat, dini ni imani na haifati rangi ya ngozi, bali ni nini unaamini)

Wapo arabs pia wanaoamini katika imani ya kiyahudi (ndio ipo dini ya kiyahudi)
Pia wapo arabs ambao ni wakristo.
Na wapo Wazungu ambao ni Waislamu dini kali haswa kuliko hata muislamu aliyepo Mecca.

My point is, tusichanganye dini (imani) na rangi ya ngozi.

Ndo maana Pakistani kiasili kwa rangi ya ngozi (rangi) ni Wahindi, ila Kiimani wengi wao ni Islam.

Indonesia, kimuonekano ni mchanganyiko wa Indians na Chinese/Japanese, ila Kiimani wengi wao ni Islam.

With that being said so, Iranians, achana na rangi ya ngozi yao, ila Kiimani wao majority ni Muslim.
 
Mangi kimambi naye anasimama na watu wengine katika kuushutumu utawala wa Kiisilamu wa Irani kusema ni mgumu afadhali ule wa Saudia arabia na baadhi ya inchi zingine za Kiisilamu

Nimeona ngoja niwajibu watu wote waujue Uisilamu wa kweli,Ukisoma historia ya kweli kabisa ya Uisilamu alioishi nao Mtume Muhammad (S.A.W) ndiyo haya maisha halisi wanayoishi wairani,inamaana hakuna kitu kipya walichoingiza kila wanachokifanya ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume wake Muhammad(S.A.W)na wao wanayafwata na haya yanayotokea leo yalishatokea miaka 1400 huko kabla
Saudia Arabia

Kuna Waisilamu lakini kama inchi haina sifa ya kuitwa inchi ya Kiisilamu sababu tayali imeshajitoa katika misingi ya kiisilamu,wameungana na Waisrael pamoja na inchi za Magharibi wamejikuta wao wanafwata tamaduni zao wakati Mungu anatukataza Waisilamu kukaa mbali na watu kama hao

Mfano leo hizo inchi zinazojiita za kiisilamu zimewakalibisha wazungu zimejikuta zinauza pombe,kuna clabu za malaya nazani hata nyama za nguruwe zinauzwa watu wanatembea uchi kama Dubai na viongozi wao wanaishi maishi ya anasa,

Katika Uisilamu hivyo vitu vimepigwa marufuku sasa mnamshutumu Irani anayefwata sunna ya Mtume Muhammad(S.A.W) na maisha aliyoisha swahaba immamu Ali bin twalibu au manataka muendeleza wa maisha ya makafiri wa Makka kina Muwaiya kabla hawajakubali kusilimu kinguvu
Ni ujinga kuweka fikra za mtu mmoja kwenye maisha ya watu wengi.. ni mara mia bomu moja linalo vurumshwa na iran kwenda israel likosee njia likaangukie kule mnakoenda kumpiga shetani na kwenye nyumba ya milele ya huyo jamaa yenu ili akili ziwakae sawa
 
Kwani katika ulimwengu huu ni wote wanafanya mabaya?

Mimi ninaposema "wenzake" namaanisha wale ambao hawatendi mabaya
Kwa hiyo huwezi kumtetea eti hana kosa kwa kuwa ameletwa kwenye ulimwengu wenye mabaya na wakati kuna wenzie hawatendi hayo mabaya katika ulimwengu huohuo.
Mbona unabadilisha swali?

Mimi naweka hoja kwamba hakuna mtu aliye katika ulimwengu usioruhusu mabaya, unakubali hilo?

Na kwa nini unaishia kwenye mabaya ya kufanywa tu, kwani hakuna mabaya tofauti ya kutokea tu bila mtu kuyafanya?

Hivi unaeleea hata hoja yangu ni nini au unabisha kidini tu kumtetea Mungu wako?

Nimekuuliza maswali hapo juu hujayajibu.

Kati ya aliyeumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, na wanaofanya mabaya kwa sababu tu wapo katika ukimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi?

Hujajibu.

Kwa nini?

Hujajibu swali la nsingi.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?

Hujajibu swali hili. Umejaribu kusema anatujaribu, nikakuuuliza anatujaribu ili iweje wakati yeye anajua yote na ndiye anatupa uwezo wa kufanya mema na mabaya na mipaka ya uwezo huo?

Hujajibu maswali haya.
 
Serikali ya Iran ili ua waandamanaji zaidi ya 6000, Mange na watz wapenda Haki hatusapoti ukiua waandamanaji
Laana ya kua waandamanaji itaitafuna Iran na Tz Karma is real
 
Kati ya aliyeumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, na wanaofanya mabaya kwa sababu tu wapo katika ukimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi?
Kwa mfano hapa nakujibu mwenye kosa ni huyo anayefanya mabaya kwa sababu ameamua mwenyewe kuchagua mabaya wakati wenzie wakichagua mazuri
 
Uislamu ni dini ya kumtii au kumnyenyekea Allah kwa kufuata maamrisho na makatazo yake

Madhehebu yake ni Hanaf,Malik,Shafi na Hanbal
Uliyoyataja hapo ni vi-sub-part (shule za sheria) vya dhehebu la Sunni.

Endelea kuchimba zaidi ili ujue madhehebu makubwa ya Islam ni yapi.

Kisha uje utuambie kama Shia ni Islam au sio Islam.
 
Kwa mfano hapa nakujibu mwenye kosa ni huyo anayefanya mabaya kwa sababu ameamua mwenyewe kuchagua mabaya wakati wenzie wakichagua mazuri
Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayapo, hayajulikani, hayawezekani kufanyika, huyo aliyefanya mabaya angeweza kufanya mabaya?

Mfano, Mungu angeumba ulimwengu ambao mauaji hayawezi kufanyika, watu wangeweza kuua?
 
Sijajibu au hujafurahishwa na majibu yangu?
Majibu yako hayana mantiki.

Mungu mjuzi wa yote anatujaribu ili iweje wakati yeye anajua yote na ndiye anatupa uwezo wa kufanya mema na mabaya na mipaka yake?

Sasa anatujaribu ili iweje wakati anajua kila kitu na yeye ndiye anayetupa uwezo?
 
Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayapo, hayajulikani, hayawezekani kufanyika, huyo aliyefanya mabaya angeweza kufanya mabaya?

Mfano, Mungu angeumba ulimwengu ambao mauaji hayawezi kufanyika, watu wangeweza kuua?
We endelea kutetea tu uovu lakini hilo ni kosa la mtu binafsi kwa kuchagua uovu badala ya uzuri
 
Majibu yako hayana mantiki.

Mungu mjuzi wa yote anatujaribu ili iweje wakati yeye anajua yote na ndiye anatupa uwezo wa kufanya mema na mabaya na mipaka yake?

Sasa anatujaribu ili iweje wakati anajua kila kitu na yeye ndiye anayetupa uwezo?
Hata wewe maswali yako hayana mantiki

Nimekwambia amekuleta duniani ili hata akikuhukumu uwe na yakini kuwa kweli nastahili adhabu kwa niliyoyatenda

Kuhusu kuwepo kwa ulimwengu usio na maovu hajataka uwepo na ukimlazimisha kuwa angefanya hivyo huyo anakuwa sio Mungu tena ila ni babu yako
 
We endelea kutetea tu uovu lakini hilo ni kosa la mtu binafsi kwa kuchagua uovu badala ya uzuri
Kwanza kabisa, hili si suala la mimi kutetea uovu, ni suala la kuhoji logical consistency, but I suspect you do not understand that.

Mtu binafsi angeweza kuchagua uovu badala ya uzuri kama Mungu angeumba ulimwengu ambao uovu haupo?

Mbona hili swali hutaki kulijibu?
 
Uliyoyataja hapo ni vi-sub-part (shule za sheria) vya dhehebu la Sunni.

Endelea kuchimba zaidi ili ujue madhehebu makubwa ya Islam ni yapi.

Kisha uje utuambie kama Shia ni Islam au sio Islam.
Bila shaka unatumia Google au AI

Anyway hiyo Sunni na mengine unayodai ni madheheb sio madhehebu ila zinaitwa Firaq

Nenda kasearch tena
 
Hata wewe maswali yako hayana mantiki

Nimekwambia amekuleta duniani ili hata akikuhukumu uwe na yakini kuwa kweli nastahili adhabu kwa niliyoyatenda

Kuhusu kuwepo kwa ulimwengu usio na maovu hajataka uwepo na ukimlazimisha kuwa angefanya hivyo huyo anakuwa sio Mungu tena ila ni babu yako

Kwa nini hukumu iwepo?

Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwapo hukumu ingekuwapo?

Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwapo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.

Sifikiri hata kama unalielewa swali.

Kwa majibu unayotoa, hujalielewa swali bado.
 
Back
Top Bottom