Ukishaona mgawanyiko kwenye dini tu, ujue hapo hakuna Mungu hizo ni siasa za watu tu, ni kama CCM na CHADEMA wanashindana.
Dini ni siasa ya kale iliyovishwa joho la utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, wote tungemjua, tungemjua bila utata, na kusingekuwa na dini wala madhehebu tofauti.
Hizi habari za hawa Shia, hawa Sunni, hawa Katoliki, hawa Protestant, hawa Buddhist, hawa Hindu, zinaonesha hizi dini zote ni hadithi za kutungwa na watu tu, watu wanapambana na hali zao, wanataka kutawalana, na huyo Mungu hayupo.