Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Usikaze fuvu la kichwa kama hujui historia ya Uisilamu,unajua kama wewe ni mtu wa kuswali msikitini na kuondoka bila kujua historia ya dini yako
Kwa hiyo Uislam ulianzia Irani, Muhammad alikua mPersian? hahaha wewe utakua ulipata ufadhili wa masomo kutoka kwa Mashia ndio maana umekua kipofu, iko hivi WaIran ni Mashia na Mashia sio Waislam, imba hivyo kila baada ya dakika 2
 
Ukishaona mgawanyiko kwenye dini tu, ujue hapo hakuna Mungu hizo ni siasa za watu tu, ni kama CCM na CHADEMA wanashindana.

Dini ni siasa ya kale iliyovishwa joho la utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, wote tungemjua, tungemjua bila utata, na kusingekuwa na dini wala madhehebu tofauti.

Hizi habari za hawa Shia, hawa Sunni, hawa Katoliki, hawa Protestant, hawa Buddhist, hawa Hindu, zinaonesha hizi dini zote ni hadithi za kutungwa na watu tu, watu wanapambana na hali zao, wanataka kutawalana, na huyo Mungu hayupo.
 
Weka hoja za kimantiki zisizokanushika hapa tuzijadili.

Uthibitisho wa kujihadithia wewe mwenyewe utajuaje kama una ugonjwa wa akili tu?
Nimejithibitishia mwenyewe maana ndio unanisaidia au unataka nikuthibitishie na wewe?
 
Mangi kimambi naye anasimama na watu wengine katika kuushutumu utawala wa Kiisilamu wa Irani kusema ni mgumu afadhali ule wa Saudia arabia na baadhi ya inchi zingine za Kiisilamu

Nimeona ngoja niwajibu watu wote waujue Uisilamu wa kweli,Ukisoma historia ya kweli kabisa ya Uisilamu alioishi nao Mtume Muhammad (S.A.W) ndiyo haya maisha halisi wanayoishi wairani,inamaana hakuna kitu kipya walichoingiza kila wanachokifanya ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume wake Muhammad(S.A.W)na wao wanayafwata na haya yanayotokea leo yalishatokea miaka 1400 huko kabla
Saudia Arabia

Kuna Waisilamu lakini kama inchi haina sifa ya kuitwa inchi ya Kiisilamu sababu tayali imeshajitoa katika misingi ya kiisilamu,wameungana na Waisrael pamoja na inchi za Magharibi wamejikuta wao wanafwata tamaduni zao wakati Mungu anatukataza Waisilamu kukaa mbali na watu kama hao

Mfano leo hizo inchi zinazojiita za kiisilamu zimewakalibisha wazungu zimejikuta zinauza pombe,kuna clabu za malaya nazani hata nyama za nguruwe zinauzwa watu wanatembea uchi kama Dubai na viongozi wao wanaishi maishi ya anasa,

Katika Uisilamu hivyo vitu vimepigwa marufuku sasa mnamshutumu Irani anayefwata sunna ya Mtume Muhammad(S.A.W) na maisha aliyoisha swahaba immamu Ali bin twalibu au manataka muendeleza wa maisha ya makafiri wa Makka kina Muwaiya kabla hawajakubali kusilimu kinguvu
Ishu ya imani au kuamini Mungu haipaswi kuwa ishu ya kitaifa, kwamba kila mtu ktk nchi au taifa husika lazima afuate mrengo huu wa imani na sheria kutungwa...

Na kwa hili nakubaliana na Kiranga kuwa, huu ni ujinga uliovuka mipaka ya ujinga kulazimisha kila mtu kufuata uislamu...

Hii ni sawa na lililotokea Zanzibar jana au juzi kwa kuwakamata watu kosa la eti kuuza pombe, kunywa na kulewa kipindi cha mwezi wa Ramadhani. Huu ndio ujinga wenyewe sasa...

Mungu mwenyewe aliyetuumba hawalazimishi watu au binadamu kumwabudu kwa kuwafunga kamba isipokuwa ameweka options zake pale (UZIMA na MAUTI) na mwanadamu mwenyewe ndiye achague kwa wakati wake awe upande gani...

Na wanadamu walishafanya machaguo yao. Ndio maana wengine wanaabudu ng'ombe, miti, mbwa, milima, mito, bahari na Mungu kamwe hawasumbui wala kuwatumia pilisi na maisha yanaenda...

Ila ipo siku moja tu ya kila mtu kutoa hesabu ya maisha yake hapa duniani. Siku ya hukumu..n
 
Huyo Mungu mwenyewe hayupo mkuu, hizi zote ni habari zetu wenyewe tunapigana na hali zetu tu.
 
Nimejithibitishia mwenyewe maana ndio unanisaidia au unataka nikuthibitishie na wewe?
Uthibitisho wa kujithibitishia mwenyewe hauna uhakiki wa nje, nimekuuliza, utajuaje huo ni uthibitisho na si kwamba wewe una matatizo ya akili tu unafikiri ni uthibitisho?

Hujajibu.
 
Uthibitisho wa kujithibitishia mwenyewe hauna uhakiki wa nje, nimekuuliza, utajuaje huo ni uthibitisho na si kwamba wewe una matatizo ya akili tu unafikiri ni uthibitisho?

Hujajibu.
Tuanze na wewe umejuaje kama Mungu hayupo baada ya kuzaliwa na kukuta habari za Mungu si kwamba wewe una matatizo ya akili?
 
Tuanze na wewe umejuaje kama Mungu hayupo baada ya kuzaliwa na kukuta habari za Mungu si kwamba wewe una matatizo ya akili?
Tatizo huijui dunia.

Nimekuwekea hoja hapo juu hujaweza kuzijibu kwa sababu inao ekana zimewekwa Kiingereza ambacho hukijui.

Unajua Epicurean Paradox ni nini?
 
Me sijaona hoja yako

Ndio kitu gani hicho?
Hiyo ndiyo hoja yangu, huijui dunia. Hujui Epicurean Paradox ni nini. Hujui Kiingereza.

Mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote, mfano Allah, kuumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, haiyumkiniki.

Ni contradiction. Haiwezi kutokea.

Lakini najua huwezi kuelewa.

Kwa sababu huijui dunia.
 
Sasa hiyo si ndio maana ya ulimwengu
Ulimwengu lazima uwe na mabaya na mazuri sio mazuri peke yake
 
Yeyote anayelazinishwa kufanya chochote kwa msingi wa dini katika Uislamu ni contradiction.

Mfano, ukimlazimisha mtu asinywe pombe, kisheria, kwa sababu ya dini, ni ujinga.

Kwa sababu Quran inesema dini ni suala la hiyari, si la kukazinishwa.

Ukilazimisha benki zisitoze riba, kisheria, kwa sababu ya dini, ni ujinga.

Kaa sababu suala la dini ni suala la hiyari, si la kulazimishana.
Unajua watu wengi wanazani sheria ya Dini ya Kiisilamu zimetungwa na mwanadamu,siyo kweli hizo sheria kazitunga Mwenyezi Mungu,siyo tu sheria bali utaratibu mzima wa Dini ya Kiisilamu kuanzia Kuswali,kula,kunywa,vyakula,kuvaa,kutembea,kulala,kujamiana,ndoa,kifo,kuongea,elimu,mkiwa vitani,na vitu vingi tu,na kila kimoja kina ufafanuzi wake
 
Hakulazimika ila aliamua

Au wewe kuna ulimwengu mwingine unaufahamu hauna mabaya?
Sasa kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aliamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati angeweza kuumba ukimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Back
Top Bottom