Kwa mara ya kwanza niliijua maana halisi ya "Mtoto wa kishua" kupitia huyu dogo. Kuna watoto wamezikuta pesa aisee!

Kwa mara ya kwanza niliijua maana halisi ya "Mtoto wa kishua" kupitia huyu dogo. Kuna watoto wamezikuta pesa aisee!

Wakati niko mwanafunzi, kuna jamaa yangu alikuwa anafanya kazi tayari basi akanipeleka sehemu posta Dar tukala. Alilipa TZS50,000 ile bill yangu. Nilimlaani sana (kimoyomoyo). Mimi sina hela ya chakula chuoni halafu ananipeleka sehemu expensive, ananinunulia chakula cha 50,000/= na kuniacha hivyo hivyo!! Jioni chuoni mkate na chai!
Ndivyo ilivyo mkuu, ukiwa huna pesa utaona waliinazo kama wanazichezea..
 
Nilikuwa nimeripoti chuoni mwaka 2011 kwa mara ya kwanza nikiwa nimehitimu form 6,

hostel kulikuwa na vyumba ambavyo mnakaa watu wawili wawili, Nilimkuta dogo flani yeye kamaliza form 4, alikuwa ameshaanza form 5 lakini aliachana nayo ili asome chuo

kwa haraka haraka tu nilijua kwamba huyu dogo nimemzidi umri ila siwezi kumsogelea hata robo ya uchumi wake, simu aliyokuwa ya bei mbaya mno. black berry bold touch 9900, simu nyingine alikuwa haitumii sana ilikuwa i phone 4 nakumbuka nilikuwa naitumia mara kwa mara na hatimae kujimiliisha kimtindo, hii simu ilinipa sana title chuoni...yani dogo alikuwa ana badilisha simu karbu kila baada ya miezi miwili hadi sio poa.

Ukiwa huishi na huyu dogo ilikuwa ni ngumu sana maisha yake kiuchumi, alikuwa anavaa kawaida tu, hana fujo ya pesa, haringishii alivyonavyo, huji kumsikia akisema baba yake ana cheo flani, n.k ni mpaka uishi nae ndio utamjua, hivi hivi ni kazi sana.

Pocket money yake laki 6 hadi 8, hata uwe na boom husogelei kabisa, hapo kila chuo kikifungwa alikuwa anakatiwa tiket ya ndege, ile tiketi ya kurudi chuoni nilimwambia apande basi, atunze pesa kuna mradi nataka tuufanye, pesa yote iliishia kwenye nyama aisee, hadi leo tukikumbushana huwa tunacheka sana.

Alinitoa ushamba wa vitu vingi sana, nilizijua pizza kupitia yeye, nilizijua kumbi za sinema kupitia yeye, niliijua mitaa ya dar ambayo ipo kimya yenye nyumba kali kupitia yeye (sikumbuki jina la mtaa mimi sio mwenyeji dar) , n.k kiukweli vilikuwa vitu vingi sana.

huo mda wote kaja kusoma chuoni ili tu apoteze mda kidogo aende zake kusomea nje, ada aliiacha na mitihani ya kualizia muhula hakufanya, yani nilibaki nashangaa sana, nilimshauri apige pepa achukue hata cheti ila alikomaa na mpiango yake.

Dem wake alimgeuza kuwa atm, nilikuwa natamani kumnasa vibao huyu dogo

Kuna kipindi dogo nusu nimzabue vibao 😂 kapata gf ni mjanja sio poa yani, kampanga dogo kwamba ana maisha magumu, dogo akawa anampa elf 50 kila baada ya siku 3 ama 4, nilipogundua nilikuwa napatwa sana hasira, nilimshauri sana dogo awe mjanja linapokuja swala la wanawake ila dogo kichwa kizito, na kweli ile pisi ilikuwa kali sana si mchezo na ilijua kumzuzua dogo si kitoto, siku dogo kasafiri weekend karudi kwao sijui alipangwa vipi, kanitumia laki 2 na nusu eti nikampe dem wake iwe kama sapraiz, kiukweli uso ulijaa ndita za hasira, yani laki 2 na nusu kiboya boya tu hivi dogo anapunwa mchana kweupe!! dogo mda huu nilimkaripia na kumfokea sana kwa hasira astuke anachezewa lakini yeye alikuwa anacheka tu, angekuwa karibu ile siku nilikuwa nampiga vibao, niliona dem wake kamwambia aje aongee na mimi nimtumie hio, dakika 5 si nyingi kashatia maguu, nilijituliza chumbani kmyaaa!! aligonga hodi kama dakika 4 hivi siitiki simu nimeiweka silent, 😂 baadae sana nilimtumia huyo dem elf 80 tu, elf 20 niliikatia kwangu kupunguza hasira, hiyo nyingine nilimwambia dogo aje mwenyewe siku akirudi, siku anaenda kumpa nilimsihi sana lakini wapi aisee, nilipiga ngumi kwa nguvu sana ukutani, baada ya miezi miwili dogo ndio anakuja kustuka dem wake hajatulia ni mapepe mtoto wa mjini, dogo alikuwa hoibintaaban kitandani siku 2, dogo aliumia sana kuumizwa ila liikuwa ni fundisho muhimu sana kwake maana alikuwa anachezewa kama mtoto.

siku anaondoka nilimsindikiza hadi maeneo ya kusubiri gari ya airport, ile narudi kanitumia mesej "oya cheki chini ya blanket lako" nilidaka boda boda chap sana, kwenda kufunua yani machozi yalinilenga, dogo aliniachia sim moja mashine sana samsung galaxy s2, hapo kuna ile iphone 4 ambayo niliificha ili machawa zake wasiione nilikuwa naitumia kisiri siri ila yeye ni kama aliipotezea mazima hana habari nayo, vilikaa basi ??

Kiufupi hii nchi kuna watu watu wana pesa sana, usije kuthubutu kusema hatuna pesa. cha ajabu ni kwamba nae alikuwa anajiona wa kawaida sana hajafikia level za wakishua, hapa ndipo nilikuwa nachoka aisee!!!
Tatizo sio kuwa dogo alikuwa wa kishua sema wewe ndio ulikuwa choka mbaya
 
Ndo hivyo mkuu Kuna madogo ukimhadisia life la ulikotoka anakushangaa,shida anasikiaga tu!! mm Kuna dogo tulisoma nae ss Kuna sku dogo akaamua kuja na semi trailer mpya kabisaa,tunashangaa semi imeleta nn ,kumbe dogo kaja nayo,halafu akashuka akaenda mpaka nyuma ya trailer akapanda na kutoa begi ya madaftari [emoji23][emoji23].kumbe dogo alifanya makusudi kisa Kuna siku alinyimwa lift na tcha .
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaaah
 
Halafu eti mnasema maisha hayana shortcut?

Kuzaliwa familia yenye mpunga kama huyo dogo hiyo tayali ni shortcut.

Masikini tuache kujifariji.

Mjukuu wa Bakhresa tayali keshapita shortcut.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati niko mwanafunzi, kuna jamaa yangu alikuwa anafanya kazi tayari basi akanipeleka sehemu posta Dar tukala. Alilipa TZS50,000 ile bill yangu. Nilimlaani sana (kimoyomoyo). Mimi sina hela ya chakula chuoni halafu ananipeleka sehemu expensive, ananinunulia chakula cha 50,000/= na kuniacha hivyo hivyo!! Jioni chuoni mkate na chai!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom