kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,832
- 4,070
Sikuwahi kumkubali huyu mwamba kipindi chake chote Cha utawala mpaka anakufa.
Akili imenikaa sawa sawa, kama binadamu ni kweli alikuwa na mapungufu yake hakuna mkamilifu.
Nakubali huyu mwamba alikuwa na nia ya dhati ya kulipigania hili taifa. Nahisi labda njia tu ndo zilitukwaza baadhi yetu nimemsahe pale ambapo alinikwaza kama mwananchi wa kawaida.
Nampa udhuru pia kwasababu naamini ilitakiwa iwe vile, kwa namna ambavyo Watanzania tulivyo ilimlazimu awe vile. Kubembelezana na kulambanalambana kumetufanya tuchelewe Sana. Kama kiongozi alikuwa sahihi kuwa mkali hasa Kwa mafisadi, wahujumu uchumi, mabeberu na vibaraka wa mabeberu.
Kwa haya yanayoendelea nchini ni dhahiri tunarudishwa nyuma mnoooo haina ubishi. Kama mtanzania nimeona nisiwe mnafki, nasema kweli kutoka moyoni mwangu.
Alisema Magufuli "mutanikumbuka, tena sio Kwa ubaya mtanikumbuka Kwa mazuri" Nakiri kumkumbuka Magufuli Kwa mazuri yake.
Mnisamehe Watanzania wenzangu ambao niliwakwaza Kwa namna yoyote ile hasa wale ambao walibahatika kuwa na maono ya haraka juu ya uzuri wa Magufuli. Nakiri nilitenda kosa la kumzungumza vibaya mzee wetu.
Magufuli ametenda, kwa hali iliyopo Sasa hivi Kila mtu anashuhudia. Na huko tuendako tutaimba nyimbo moja.
Ahsanteni sana.