Mimi Ni mgumu Sana kupongeza.Lakini kwa Hili la Wamachinga, nampongeza Sana Rais wetu Mama SAMIA.Ubarikiwe Mama yetu Rais Samia.BAAADA YA HILI LA WAMACHINGA,Naomba ufanye marekebisho kwenye baadhi ya vipengele vya Katiba ya JMuungano,e.g. Tume huru ya uchaguzi,na baadhi ya vipengele vya Muungano wenyewe.Ruhusu pia Uhuru wa kisiasa.Usikubali uchaguzi wa kusimamiwa na Wakurugenzi wa Majiji na Manispaa.Police wasipendelee chama chochote wakati wa campaigns na wakati wa uchaguzi.Nakuhakikishia ukifanya Haya na Mengine ya nyongeza, kwa kadiri utakavyoona inafaa,Mungu atakubariki,Hiyo 2025,hata upambanishwe na YEYOTE Ndani ya chama chako CCM,Lazima utaibuka mshindi.Pia nje ya chama,Hata upambanishwe na Tindu Lisu,Lazima UTASHINDAA TU,Maana Mungu na Wa-Tanzania wanataka Rais(Kiongozi)Mtenda Haki.Ubarikiwe Rais wangu Mama Samia.
JF ni kama kokoro, wamejaa watu wa kila aina kuanzia walioishia darasa la pili B shule ya msingi mpaka wenye phd, welevu na wajinga, wavumilivu na wakurupukaji, wenye exposure na wasio na exposure, wenye milengo ya kisiasa na wasiokuwa na milengo ya kisiasa n,k n.k n.k n.k. Hivyo usiwe na pressure sana humu.
Kama wewe ni machinga ujue kuna ustaarabu wa jinsi ya kuishi mijini.
Si Tanzania tu, bali duniani pote.
Ukiwa na kiongozi mshamba ambaye hana hata kizazi kimoja kuishi mjini haya ndiyo matokeo yake.
Madhara atayaona mwishoni mwa kizazi chake, then its too late.
Swala la machinga nampongeza Rais kwa kutoa maamuzi magumu machinga walishakuwa kero pia vibanda na uchafu ilikuwa aibu kwa majiji makubwa ilifanya tuonekane nchi ka ya vichaa, pia nimpongeze Makele jiji limeanza kuwa safi kuanzia Mwenge, ustawi na kwingine aisee vile vibanda plus mbao ulikuwa uchafu uliokubuhu Hadi nawaza kwanini machinga hawana aibu na hawajali usafi?
Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!
Huna hoja wala mchango wa msingi kwenye hili, hujielewi, hulijui tatizo wala huwezi kuwa na suluhu unaongeaongea tuu sababu ya chuki zilizokujaa, choyo, roho mbaya na ubinafsi. Ukipunguza roho mbaya na kufurahia maumivu ya wengine utaweza kujenga hoja za msingi na zenye maendeleo kwako na...
www.jamiiforums.com
Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!
Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF
Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!
Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.
Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni
1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi
2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri
3. Ushamba na kukosa exposure
Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu
Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya
1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena
2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa
3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa
4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya
Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi
Ni kwel mkuu namponeza sana SSH but hofu yangu kunauwezekano mkubwa huko baadae hapa Dar kutatokea wimbi la Wizi kila siku watu wanaibiwa maana baadhi ya machinga wamepiteza mali zao/mitaj yao vibanda vimevunjwa wamepoteza Asset zao..
Ni sulla la muda tuh but naomba isitokee hivyo
Mimi au wewe na wenzako ndio washamba malimbukeni wa ulaya, eti exposure…Nyie ndio mnaompotosha Raisi mnaiga mambo ya ulaya kwenye third world countries sio kila kitu cha kuiga..hizo exposure zenu zitawacost..ni swala la muda tu..

Kwa iyo kwa akili yako anayefanya biashara masaki akipelekwa kariakoo au Ubungo anatakiwa akaibe? Nani kakufundisha Hilo jambo? Au umeshawai liona wapi?
Kwa akili yako unaaamini kufanya biashara kwa uchafu, bila kulipa kodi na kuharibu miundombinu ndo maana ya third world countries?

Huyo anayefanya masaki unadhani huko Ubungo hakukuona!? Kila mtu anafanya biashara kuendana na eneo alilopo. Si ajabu mamalishe mliowarundika pale kisutu wengi tayari mitaji imekata na wengine wamekimbia pale. Wapi uliwahi ona mamalishe wote wanakusanywa sehemu moja!? Ili wamuuzie nani!?
Hivyo vijishule vyenu vinawafanya mjione kuwa mnajua kila kitu. Upuuzi.
Ni kwel mkuu namponeza sana SSH but hofu yangu kunauwezekano mkubwa huko baadae hapa Dar kutatokea wimbi la Wizi kila siku watu wanaibiwa maana baadhi ya machinga wamepiteza mali zao/mitaj yao vibanda vimevunjwa wamepoteza Asset zao..
Ni sulla la muda tuh but naomba isitokee hivyo
Ukiniambia bodaboda na bajaji zimepigwa marufuku kufanya kazi nitakuelewa maana ni kundi kubwa mno ambalo likiachishwa hizo kazi bila alternative basi jamii lazima itikisike. Waliokuwa vibaka, wezi, wadokozi, na hata majambazi wengi wamemezwa na kazi ya bodaboda na bajaji. Hawa wafanyabiashara ndogo ndogo (mnawaita Machinga) hawajaambiwa wasifanye kazi bali wamehamishwa tu kupelekwa maeneo muafaka kwa kazi yao sasa sijui hofu yako ni nini hapo? Au ndio yale mambo ya Fear of the unknown? MAISHA YANAENDELEA KAMA KAWA PONGEZI KWA SERIKALI YA MAMA SAMIA KWA KUTUONDOLEA UCHAFU WA MABANDA NA MOSHI WA KUNI MJINI.
Huyo anayefanya masaki unadhani huko Ubungo hakukuona!? Kila mtu anafanya biashara kuendana na eneo alilopo. Si ajabu mamalishe mliowarundika pale kisutu wengi tayari mitaji imekata na wengine wamekimbia pale. Wapi uliwahi ona mamalishe wote wanakusanywa sehemu moja!? Ili wamuuzie nani!?
Hivyo vijishule vyenu vinawafanya mjione kuwa mnajua kila kitu. Upuuzi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.