Kwa Mara ya Kwanza nimeona Mafanikio ya Serikali kwenye suala la Machinga, Hongera Serikali ya Awamu ya Sita

Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
Miaka 60 ya uhuru tumefanikiwa tu kufukuza wamachinga Kariakoo. Mungu anajua ni lini watoto wetu wote watakalia madawati shuleni, achilia mbali kufikia uchumi wa viwanda.
 
Kulikuwa na tabia za ajabu sana ilitengenezwa kwa watanzania! Watu hawataki kufuata taratibu na ustaarabu wa binadamu eti kisa kujiita mnyonge!

Walijipa hatimiliki ya kuvunja sheria, kuharibu miji, kuvunja utaratibu wa barabara zetu eti kisa wao ni wanyonge!

Huu ulikuwa ushamba uliotukuka
Kujiita tu wanyonge Hilo lilikuwa tatizo number moja lililofanya watu wasitumie akili ipasavyo Ili kupata excuse ya kutofata taratibu za mipango miji, naomba serikali ikimaliza la machinga waje kwa hawa bodaboda maana ni group linalohitaji msaada wa haraka kunusuru vijana na ulemavu
 
Miaka 60 ya uhuru tumefanikiwa tu kufukuza wamachinga Kariakoo. Mungu anajua ni lini watoto wetu wote watakalia madawati shuleni, achilia mbali kufikia uchumi wa viwan
mkuu naona bado hujaliewa somo.Machinga wanapaswa kupiga kelele ili kila mtu akae eneo rasmi wateja wawakute hapo.
 
Machangudoa na wala shisha ni wahalifu kwa mujibu wa sheria gani
Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
 
mkuu naona bado hujaliewa somo.Machinga wanapaswa kupiga kelele ili kila mtu akae eneo rasmi wateja wawakute hapo.
si kwa nchi yetu hii,yaani mteja amfuate muuzaji,machinga ni muuzaji wa kitu ambacho mnunuaji analazimishwa kununua,mfano umeshuka zako kariakoo unaenda kwenye pilikapilika zako ukakuta sendo njiani unakuja kukumbuka sina sendo ndo unaponunua hapo
 
Kiongozi, unajua huko wanakopelekwa hakuna wateja, wavumilivu ni wachache, wengi watajaribu kurudi na wengine kuacha kabisa coz mauzo yatashuka sana. Mfano ni pale Mbezi mwisho, wakiondokewa kupelekwa nyuma ya stand ya magufuli unadhani nani ataenda kununua bidhaa kule? Shana ya machinga ni kufuata mteja alipo, sio mteja kumufuata na sisi watanzania hatupendi kufuata huduma, tunapenda huduma zitufate, ndio maana machinga hawawezi kuisha.
Umeongea point kabisa
 
tumefungua kiwanda kipya cha makahaba, wezi , matapeli na majambazi.
 
Swala la machinga nampongeza Rais kwa kutoa maamuzi magumu machinga walishakuwa kero pia vibanda na uchafu ilikuwa aibu kwa majiji makubwa ilifanya tuonekane nchi ka ya vichaa, pia nimpongeze Makele jiji limeanza kuwa safi kuanzia Mwenge, ustawi na kwingine aisee vile vibanda plus mbao ulikuwa uchafu uliokubuhu Hadi nawaza kwanini machinga hawana aibu na hawajali usafi?
Yani abiria hawana srhemu ya kusubiri bus
 
tumefungua kiwanda kipya cha makahaba, wezi , matapeli na majambazi.
Uwe mwizi tapeli na Jamba I kwa kwenda kupangwa sehemu Nzuri ili ufanye biashara kwenye mazingira safi , salama na ulipe kodi?

Utakuwa umerogwa wewe
 
Mkuu kuna watu humu JF wanaona aibu kukiri kuwa hata hilo la machinga ndiyo legacy ya mwendazake.
Hatutaona aibu kukiri kuwa JPM aliwatendea mema wamachinga, na wenyewe wataendelea kumshukuru na kumkumbuka daima!

Huo muonekano unaoufurahia hauwapi shibe watu maskini watanzania
 
Ilikuwa aibu! Tulikuwa tunaonekana wote ni nchi ya wajinga tusio wasafi na tusiofuata taratibu!

Kweli kwa hili naipongeza awamu ya sita! Wasirudi nyuma tu
Nchi ya kijamaa haipaswi kuweka mbele fahari za miji na kupuuza maisha ya watu

Huo ni ubepari
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
Kwenye suala la Machinga subiri kutoa pongezi baada ya miaka miwili au mitatu. Sasa hivi kwa mfano hapa Jijini Mwanza, RC, RAS, RPC, DC, DAS, DED, Mayor, OCD, Mbunge, Watendaji Kata wote na maafisa wao WOTE wako mabarabarani ETI wanawapanga Machinga. Hakuna ofisi inayofanya kazi. Swali la kujiuliza, hawa maafisa wakirudi ofisini kwao, Machinga watabaki "site"?
 
Back
Top Bottom