Kwa Marufuku hizi za Zanzibar ni wakati muafaka wa Mikoa ya Pwani kukamata fursa ya Utalii

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Utajiri wa uswizi leo hii umechangiwa sana na namna ambavyo walitumia mwanya wa kutengeneza Sheria nzuri zilizowafanya matajiri wengi wa ulaya kupeleka fedha zao Uswizi kwa kuwa nchi za ulaya zilitengeneza Sheria kali sana za kodi baada ya vita kuu ya pili ya Dunia.

Leo hii Zanzibar wametangaza Sheria kali ikiwemo kupiga marufuku upigwaji wa mziki maeneo ya fukwe.

Sote tunajua moja ya sababu iliyokuwa ikifanya Zanzibar kuwa sehemu ya kuvutia ni kutokana na bata zake zilizokuwa zikifanyika katika fukwe zake.

Kama Viongozi wa Mikoa ya Pwani hasa Tanga, Pwani na Dar, marufuku hizi za Zanzibar ni fursa kabambe kwenu kutengeneza mipango kabambe ya kuwafanya watalii waje kwenu na kuongeza mapato ya mikoa yenu.

Tumieni fursa maana wakati ni sasa.

Kwa marufuku nyingine zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika

 
Wazanzibari ukichunguza vzr uwezo wao wa Akili ni Mdogo sana.

Ndio maana muna baadhi ya maamuzi wanayafanya mpaka unajiuliza ni kundi la watu limekaa chini wakifikia huu muafaka?
Sawa lakini kiongozi wako mkuu ndo anatokea huko
 


Hakuna kitu. Kelele zisizo maana, mimi najua kampuni inapeleka box 300 kil week za pork product zanzibar, zinapita bandarini, wazi, kweupe, hii sheria ya pork Zanzibar yenyewe haitekelezeki, hizi nyingine ndo kabisa.
 
Kupata watalii sio lazima mziki hebu tuwe wabunifu
Mtalii anataka kujifunza culture za watu tofauti kama ni mziki wameuacha kwao pia
Unless mziki uliokuwa unapigwa ni wa nje pia, ila huwezi ku separate music na culture...
 
Bagamoyo kiutalii imesahaulika kabisa
 
Maza hawezi kukubali Zanzibar ipitwe na bara, lengo kuu kwa sasa ni kuifanya Zanzibar iwe kama Dubai na bara kuwa kama Wilaya ndani ya Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…