Kwa maslahi makubwa ya nchi mechi ya Simba na yanga ipelekwe mbele kupisha mashindano ya kimataifa

Kwa maslahi makubwa ya nchi mechi ya Simba na yanga ipelekwe mbele kupisha mashindano ya kimataifa

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Simba na Yanga zinacheza tarehe 16/04/2023. Mechi ya Simba na Yanga au Derby ya kariakoo ni mechi inayoitaji akili, nguvu na utimamu wa mwili kuikabili mechi hii kwa timu zote mbili.
Wapizani wa Simba na Yanga pia wapo kwenye tension kubwa namna gani kuzicheza mechi zao na hizi timu ambazo kila mwaka wanaimarika panapo mashindano ya Afrika. Hivyo watatumia derby hii kujijenga zaidi, na pia wachezaji muhimu wanaweza kuumia kwenye derby hii na hivyo kupunguza morali kwa wachezaji wengine.

Kushinda kwa Simba kimataifa ni kushinda kwa taifa zima, pia kushinda kwa Yanga kimataifa ni kushinda kwa Taifa zima hasa kwenye hatua hii ya robo fainali walioifikia.
 
Simba na Yanga zinacheza tarehe 16/04/2023. Mechi ya Simba na Yanga au Derby ya kariakoo ni mechi inayoitaji akili, nguvu na utimamu wa mwili kuikabili mechi hii kwa timu zote mbili.

Mechi hii inahitaji mganga mwenye nguvu tu...
 
Masimba yanaogopa kipigo Cha mbwa koko
Makolokolo hatuogopi maana tutaingia kinyume nyume uwanjani, manyaunyau meusi yatapita katikati ya uwanja kabla ya mechi kuanza au tukishindwa saana basi tutawasha moto uwanjani.

Sisi ndiyo;
• Makolokolo
• Mbumbumbu
• Manyaunyau
• Madunduka
• Mipang'ang'a
• Mikia
• Malalamiko
• Makelele
• Ngada
• Zuwena
• Kolowizards
• Kinyume nyume
• Mazumbukuku

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ulaya Madrid kacheza jana
Anacheza J5, anacheza Jmosi, anacheza J4 anacheza Jmosi.

Iweje sisi tuwe na likizo nyingi hivo?
Simba walishajiandaa kwa ratiba ngumu za kipindi hiki maana walijua zinakuja. Wakati wanachekwa kwa kwenda Dubai, mara wanacheza na Al Hilal, wengine walikuwa wanawacheka. Matokeo yake sasa hivi Simba wamoto, wengine pamoja na rotation zao wanacheza mpira haueleweki.
 
Masimba yanaogopa kipigo Cha mbwa koko
16/4/2023 afe kipa, afe beki madunduka FC mlete timu uwanjani. Msianze visingizio, iwe kuna za kimataifa au ndondo, mtacheza.

Tukutane 16/4/23
Ukiangalia kwa umakini, Yanga ndio wanatakiwa waombee hii mechi ipelekwe mbele. Hao ni Yanga makini lakini, sio kila mwana Yanga. Yanga wasio makini wanaifikiria mechi ya tarehe 16, wanajisahau kuwa baada ya hapo kuna safari ya kwenda Nigeria, tena kupitia Ethiopia au Dubai, wakati Simba watabaki Dar. Mimi kama mwana Simba naombea mechi ibaki pale pale 16 April
 
Sisi ndiyo;
• Makolokolo
• Mbumbumbu
• Manyaunyau
• Madunduka
• Mipang'ang'a
• Mikia
• Malalamiko
• Ngada
• Zuwena
• Kolowizards
• Kinyume nyume
• Mazumbukuku

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app

Hayo majina yooote iliyoyaita hapo ukijumlisha hayawezi kulishinda jina tukufu "UTOPOLO". What a name woooh
 
Ukiangalia kwa umakini, Yanga ndio wanatakiwa waombee hii mechi ipelekwe mbele. Hao ni Yanga makini lakini, sio kila mwana Yanga. Yanga wasio makini wanaifikiria mechi ya tarehe 16, wanajisahau kuwa baada ya hapo kuna safari ya kwenda Nigeria, tena kupitia Ethiopia au Dubai, wakati Simba watabaki Dar. Mimi kama mwana Simba naombea mechi ibaki pale pale 16 April
Yanga kubwa, tuna wachezaji wengi. Shida yako umejifungia ndani ya box. Toka humo kwenye box, angalia kwa upana. Kikosi kitakachoenda Nigeria si lazima kicheze mechi ya ligi kuu.
Narudia kila mchezaji Yanga, tunamuamini kutuletea matokeo mazuri.
Hii siyo shida yetu...
 
Wewe ni shabiki oya oya. Hakuna klabu isiyo na wachezaji muhimu.
 
Back
Top Bottom