Kuna swali nimeulizwa umiliki wa kompyuta ya mezani au mpakato nikajibu sijawahi miliki kwa mda wanaotaka wao...swali lililofuata nimeulizwa je nimetumia hizo compyuta za mezani au mpakato kwa mda huo? Kujibu yes ikagoma ikabidi karani aanze mwanzo....Sasa Ina maana kitu Kama hukimiliki huwezi kutumia hata kwa mtu mwingine au maofisini? Mbona taarifa wanazozitaka zitakuwa za uongo Sana?Kwanza maswali ni mengi bila sababu ya msingi halafu mengi ni ya kijinga na kipuuzi. Ingewezekana kabisa kuwa na dodoso lenye maswali machache na ya msingi. Baadhi ya maswali wangeachiwa watendaji wa mitaa/vijiji wakisaidiwa na wenyeviti wao kwani ni ya kifamilia zaidi na yanahitaji utulivu.
Kwa ufupi hii itakuwa sensa ya hovyo kabisa kufanyika nchini na itachukuwa muda mrefu bila sababu yo yote. Wananchi wengi watayakwepa au kuyapuuza baadhi ya maswali kwa kusema uongo!
PIA, SOMA:
- Maswali 100 ya sensa ya watu na makazi ya mwaka