- Thread starter
- #41
Ukifanikiwa ukapata maduka madogo 10-20 ya pembezoni ukawateka wote wakawa wananunua Mali kwako hapo utakuwa umewini.Hao tumia mbinu zote wasihame kwako,Mimi dukani Nina wateja wauhakika kama 20 nimewashikilia baadhi ya mbinu ninazotumia
1.nina toroli na pikipiki mteja hana haja ya kuja dukani kwangu anapiga simu tunaandika oda tunampelekea mzigo Kwa gharama ndogo,mfano kama Kwa bodaboda nauli ni 5000 kwangu analipia 4000
2.mteja wa jumla akipungukiwa Hela Nampa mzigo namwambia tu akusanye Hela baada ya siku kadhaa atailipa,mfano sisi hapa kwetu tunanunua Mali ya kuuza Kila jumatatu ya wiki,basi Huwa nakusanya madeni Kila jumapili,kwangu Mimi imenijengea ukaribu na wateja wangu.strong bond.
3.Nawapigia simu wateja mara Kwa mara kuuliza kama Kuna Mali wanahitaji,kuwataarifu kama Kuna Mali mpya imeingia sokoni,kuwaambia mabadiriko ya bei,mfano bei ya sukari imepanda sana nimewataarifu wapandishe bei maana wakija watakutana na bei kubwa zaidi,pia kama Kuna Mali imeshuka bei Huwa nawataarifu wauze haraka isije kuwakamata wakala loss.
4.Nikipata muda Huwa nawasha kapikipiki kangu nawatembelea kuwatia moyo kuwa Kuna siku watatoboa,pia kuwajulia Hali pamoja na kushirikiana nao kwenye social life(misiba,uzazi,sherehe n.k).
4.nimerahisisha namba ya kufanya malipo,kwangu ni till ya mpesa Huwa nawaambia waliko wanaweza kulipia kupia mpesa au benki pia.
5.mteja akihitaji Mali ambayo mm Sina Huwa namnunulia Kwa jirani,lengo langu mteja asikose bidhaa,
6.nashughulikia changamoto wanazopata dukani kwangu haraka sana na kuwapa mrejesho na kuwaomba msamaha pale tunapowakosea,mfano Kuna muda vijana wanasahau bidhaa ya mteja Huwa najitahidi sana kuzuia tatizo lisijirudie Tena.
Kwangu mm mbinu hizi zimenisaidia sana,Kwa wateja hao wa jumla naona ndio wanaoendesha biashara yangu,Kila siku napambana kuongeza idadi ya wateja,biashara ya duka msingi wake ni idadi ya wateja