Kwa mazingira yetu ya Afrika biashara ya duka la mahitaji ya nyumbani inaweza kukutoa katika umaskini

Ukifanikiwa ukapata maduka madogo 10-20 ya pembezoni ukawateka wote wakawa wananunua Mali kwako hapo utakuwa umewini.Hao tumia mbinu zote wasihame kwako,Mimi dukani Nina wateja wauhakika kama 20 nimewashikilia baadhi ya mbinu ninazotumia
1.nina toroli na pikipiki mteja hana haja ya kuja dukani kwangu anapiga simu tunaandika oda tunampelekea mzigo Kwa gharama ndogo,mfano kama Kwa bodaboda nauli ni 5000 kwangu analipia 4000
2.mteja wa jumla akipungukiwa Hela Nampa mzigo namwambia tu akusanye Hela baada ya siku kadhaa atailipa,mfano sisi hapa kwetu tunanunua Mali ya kuuza Kila jumatatu ya wiki,basi Huwa nakusanya madeni Kila jumapili,kwangu Mimi imenijengea ukaribu na wateja wangu.strong bond.
3.Nawapigia simu wateja mara Kwa mara kuuliza kama Kuna Mali wanahitaji,kuwataarifu kama Kuna Mali mpya imeingia sokoni,kuwaambia mabadiriko ya bei,mfano bei ya sukari imepanda sana nimewataarifu wapandishe bei maana wakija watakutana na bei kubwa zaidi,pia kama Kuna Mali imeshuka bei Huwa nawataarifu wauze haraka isije kuwakamata wakala loss.
4.Nikipata muda Huwa nawasha kapikipiki kangu nawatembelea kuwatia moyo kuwa Kuna siku watatoboa,pia kuwajulia Hali pamoja na kushirikiana nao kwenye social life(misiba,uzazi,sherehe n.k).
4.nimerahisisha namba ya kufanya malipo,kwangu ni till ya mpesa Huwa nawaambia waliko wanaweza kulipia kupia mpesa au benki pia.
5.mteja akihitaji Mali ambayo mm Sina Huwa namnunulia Kwa jirani,lengo langu mteja asikose bidhaa,
6.nashughulikia changamoto wanazopata dukani kwangu haraka sana na kuwapa mrejesho na kuwaomba msamaha pale tunapowakosea,mfano Kuna muda vijana wanasahau bidhaa ya mteja Huwa najitahidi sana kuzuia tatizo lisijirudie Tena.
Kwangu mm mbinu hizi zimenisaidia sana,Kwa wateja hao wa jumla naona ndio wanaoendesha biashara yangu,Kila siku napambana kuongeza idadi ya wateja,biashara ya duka msingi wake ni idadi ya wateja
 
Upo sahih mkuu , nimepend idea yako.
Je biashr ya duka la jumla unawez pia kufungua mtaan au lazima sehem ya town ?, maan naonag watu weng wanaend kw wahind kupt vitu vya jumla.
 
Ungesoma na maelezo ungepata mwanga
 
Mi Niko field wewe haupo field unasikia maneno tu,haipo hivyo,mm Nina duka la jumla nawauzia wa mtaani mchana kweupe
Mkuu mtaji wa duka la jumla unaweza kuwa kama kiasi gani roughly...?
 
Hiyo 20 kubaki kwa duka na 10 inazunguka umemaanisha nini kiongozi...?
 
Mali ya chini unamaanisha nafaka au...?
 
Mkuu mtaji wa duka la jumla unaweza kuwa kama kiasi gani ro

Hiyo 20 kubaki kwa duka na 10 inazunguka umemaanisha nini kiongozi...?
Ina maana ukianza duka Leo Kwa 30 mil hautaweza kuuza Mali yote ndani ya wiki ukapata 30 mill Tena Bali utauza kiasi inaweza kuwa 10mill hiyo ndo utaenda kununua mzigo Tena kuongeza Kwa bidhaa zilizopo Kwa duka
 
Huelewi kitu kwenye hiyo biashara

Hiyo biashara unatakiwa duka moja lizalishe duka lingine mtaa mwingine unaenda chukua vijana kijijini wa kukukuzia yakifika maduka matano unafungua duka la jumla ambayo hayo maduka mengine matano yatakuwa yanachukua duka lako Hilo la jumla umefungua pia Hilo la jumla litakuwa la jumla Kwa maduka mengine ya watu wengine

Lakini pia waweza tajirika kama duka lako liko eneo lenye mama ntilie wengi na unauza vyakula Kwa bei rafiki kwao unatoka sokoni bei ya jumla unawauzia bei rafiki

Pia Yako maeneo yenye watu wengi ambao kiasili hawaendi biashara mbona watu wanatajirika sana kupitia hayo maduka Nenda mbeya wakinga wetarijikia hayo maduka
 
Mzee darasani ulikuwa unapata ngapi? Ni mgumu sana kuelewa hata concept rahisi hivi. Hajasema hiyo estimate ya kuanza ni ya jumla anazungumzia how unaweza kuanza kwa hiyo 500k just to take off.
 
Mzee darasani ulikuwa unapata ngapi? Ni mgumu sana kuelewa hata concept rahisi hivi. Hajasema hiyo estimate ya kuanza ni ya jumla anazungumzia how unaweza kuanza kwa hiyo 500k just to take off.
Ufaulu wangu darasani haukuwa na haujawahi kuwa mbaya ila ni mwanafunzi safi wa mfano. Mbili soma tena kwa jamaa na usome kwangu. Usikurupuke wakati wa kusoma.
 
Ufaulu wangu darasani haukuwa na haujawahi kuwa mbaya ila ni mwanafunzi safi wa mfano. Mbili soma tena kwa jamaa na usome kwangu. Usikurupuke wakati wa kusoma.
Sijaanza kusoma huu uzi leo, wewe ndo umemix madesa. Yaani kwa kifupi unapata ugumu kucatch concept kwa urahisi hivyo tu.Anyways tuendelee kufatilia uzi , sitaki sana kubishana nipo hapa kujifunza maana ndo nimeanza hizo mishe.
 
Sijaanza kusoma huu uzi leo, wewe ndo umemix madesa. Yaani kwa kifupi unapata ugumu kucatch concept kwa urahisi hivyo tu.Anyways tuendelee kufatilia uzi , sitaki sana kubishana nipo hapa kujifunza maana ndo nimeanza hizo mishe.
Kwangu hujajifunza, naona umekua conservative kuona nilichoongea.
 
Mzee darasani ulikuwa unapata ngapi? Ni mgumu sana kuelewa hata concept rahisi hivi. Hajasema hiyo estimate ya kuanza ni ya jumla anazungumzia how unaweza kuanza kwa hiyo 500k just to take off.
Asante Kwa kumuelimisha yy Yuko too general hasomi between the lines,mi nilisema laki na sabuni ilikuwa starting capital na si mtaji wa kuuza jumla,from nowhere huwezi kuanza kuuza jumla Kwa maskini lazima uanze chini kabisa
 
Ukweli mtupu ambao vijana hawaijui
Kuna jamaa naendaga kuchukua vitu kwake aise yeye ndani kwake kuachana na chumba cha duka yaani kajaza makororo yote unayoyajua wewe yaani mtaji wake ni zaidi ya mil50 aise hii biz ina hela acheni utani
 
Wewe ni kijana wa ovyo mwenye akili ndogo kabisa. Mfano gani huu wa kijinga unaleta hapa. Yaani hako kaduka ka-mangi kanauza milioni 20 kwa siku na faida milioni 1!!! Unaelewa unaandika nini kweli wewe. Unaijua milioni ishirini inapatikanaje kwa kuuza mchele nusu, sukari robo, sabuni nusu kipande...
Kwa ujinga tu unasema kwa siku unapata faida ya Milioni moja?
 
Mkuuu huu n uongoo bhanaa unasemaa,mbona Kila cku magari ya mo na azam wanashusha mizigo Kwenye maduka ya kina mangi na hata magari ya coca na Pepsi pia yanafanya hvyo hvyo Tena mchana kweupeee .
Nimefanya biashara ya mauzo DSM kwa zaidi ya miaka minne. Hakuna mfanyabiashara wa jumla mkubwa ambaye hanijui kwa rout ya kimara,ubungo, mbezi zote, kawe, tegeta, bunju na huo ukanda wote.

Nina uzoefu na maduka pengine zaidi ya hata wafanyabiashara wenyewe. Na nikuhakikishie tu, jamaa anachokiongea ni kweli.

Mfanyabiashara mkubwa, bidhaa anazoshusha mchana niza MO,AZAM, CIGARETTES na makampuni ya kiswahili yanayompa mzigo kwa Mali kauli. Hizo bidhaa faida yake unaweza kuta ni 500-1000 kwa bidhaa.

Mzigo unaowapa pesa niwa magendo, mfano, mafuta ya MIKO na HAYATI, haya yanaingua kupitia bandari bubu na hawapewi risiti. MO dumu akiuza let's say 74000 ye anauza 74,500-75000, Miko au hayati ananunua kwa 66,000 anauza kwa 72000. Faida 6,000 kwa faida. Akiuza dumu 100 kwa siku? Pado sukari za nje za magendo nk.

Pesa kwa Tz hii ipo kupitia njia za panya, kwenye biashara yeyote ile. Hata humu, jifunze kwanza njia ambazo wenzio wanatengenezea pesa kweli kabla hujaingia kichwakichwa. After all ata ukijifanya kunyooka wanasiasa wanazitafuna tu.
 
 
Bo
Brother naweza kupata mawasiliano yako, samahani lakini +255757001391.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…