Kwa mbali nimeanza kuuelewa ulinzi mkali wa Rais...

Kwa mbali nimeanza kuuelewa ulinzi mkali wa Rais...

Kumbuka kilichotokea kwa Kabila Njia sahihi na kutafuta maridhiano kimya kimya na wanaompinga ndani ya chama.. hili swala la kuvujisha clip za wanaompinga ni kuchochea mgogoro zaidi na kuzidi kukigawa chama...sizani kama wanaCCM wa kweli wanafurahishwa na anayofanya Musiba
 
Nadhani kuna mtangulizi ambaye anajutia kumpisha. Ila aongeze zaidi ulinzi. Hata ikiwezekana, awaondoe wapishi abaki mama tu. Mijitu inayo washwa washwa isije mdhuru. ee Mola mpe maisha marefu na ujasiri zaidi hadi awakomeshe wezi wa keki yetu. Asiyaruhusu majizi kuzikimbiza nje ya nchi. Taifisha akaunti zao zote, hela tujengee reli mpya.
 
Hakika tulimuhitaji Rais kama huyu wakuibadilisha Tanzania,pamoja na yote yanayoendelea Mimi nitampambani Rais wangu kwa njia yoyote hata kwa kuvuja damu
Vijana anaowategeneza ni wa Ovyo sana, Linatengenezwa Taifa la kusifia na kujipendekeza ili mtu apate Cheo/madaraka, Taifa lisilo taka mwenye Mamlaka kukosolewa..
 
Kweli ulinzi mkali kabisa unahitajika, aongeze zaidi ulinzi, kuanzia, hasa katika safari zake zote, hata ktk ndege zake aongeze ulinzi kote yaani, sbb kumbe maadui zake ni watu wakubwa wastaafu walioshika madaraka makubwa.. Kupambana na maadui kama hawa kweli unahitaji kutumia njia zote kushinda. Naunga mkono hoja aongeze ulinzi mkali kabisa
Mlinz wa kweli Ni Mungu na matendo yako tu.binadamu si mlinz wako wa kudumu muda wowote hubadilika na kuwa adui wako pia.Na mtu wa Kwanza kukuua Ni mlinz wako.
 
Kumbuka kilichotokea kwa Kabila Njia sahihi na kutafuta maridhiano kimya kimya na wanaompinga ndani ya chama.. hili swala la kuvujisha clip za wanaompinga ni kuchochea mgogoro zaidi na kuzidi kukigawa chama...sizani kama wanaCCM wa kweli wanafurahishwa na anayofanya Musiba
Tunafurahi sana..na washughulikiwe kabisa.
 
Kama Mambo ndani yako hivi Tena kwa watu wa karibu...kwa hawa tu tunaowajua..itakuwa vipi kwa Wale wengine tusiowajua?
Daa nilikuwa sijakuelewa nimefikiria sana.ndani kuko salama kabisa wao wanaangalia usalama wa nchi usiwe na shaka.
 
Hakuna lolote, yani kusiwe na ushindani wa kisiasa? Watu kutaka tu kugombea 2020 nayo inaonekana ni sababu ya mtu kujiongezea ulinzi? Watu wasikosoee?

Basi hakuna haja ya demokrasia. Hivi JK alivyokuwa anakosolewa na hata kutaka kupokonywa kiti ndani ya chama na Edo naye angesema aongezewe ulinzi.

Tusidanganyane, tusitafute kichaka cha kijifichia. Tumekwama kama Taifa, mtu kaharibu mambo wazalendo wanaona sasa inatosha hali hii haiwezi kwenda miaka 10. Kujenga ni kazi ngumu na ya muda mrefu kubomoa ni kazi kidogo sana.

Biashara vilio, kilimo huko ni vilio, uchumi hoi, watumishi hoi, mwaka wa tano huu tunazungumzia Stigler, SG. Nini cha kujivunia kama Taifa?
Kilimo hoi Rais amezuia mvua au amezuia zana za kilimo kuuzwa au ameziba njia za kwenda mashambani

You're hopeless
 
Kama Mambo ndani yako hivi Tena kwa watu wa karibu...kwa hawa tu tunaowajua..itakuwa vipi kwa Wale wengine tusiowajua?

JK alikaa muda mrefu wa kitisho cha Lowasa na hakuwa na ulinzi wa hivyo iweje hili la kina Makamba mtake kuhalilisha kuuza nguruwe msikitini? Bado mnaamini mnaweza kulazimisha matumizi mabovu kwa kisingizio cha maadui zake? Hiyo ni hali ya kawaida sana kwenye siasa, labda kama mlishiba hii propaganda mfu ya kimkakati kwamba anakubalika sana. Mzee acha kutaka kutakatisha Kaniki.
 
Babu unaona mbali sana.

This post is thinking outside the bottle.

Inaonyesha kumbe incumbet ameishi na hatari jirani mno, lakini sisi tukawa tunajihoji kuwa huo ulinzi wa nini? Mungu aweke ulinzi zaidi kwake na kwetu pia
Sasa nimeaza kumuelewa magufuli.watu hii inchi walifanya ya kwao sasa mkuu anataka kuondoa dhana hiyo
 
Nahisi Raisi alikuwa anatamani aongee mengi kutujulisha watanzania jinsi watu wanavyoitaka roho yake lakini alikuwa anashindwa.

Ndio ujue zile kelele za Mange na wenzie kuwa walinzi wanatoka nchi jirani zilikuwa zinatoka kwa watu wa karibu yake walioshindwa kumdhuru.

Ili ufanikiwe kumdhuru lazima uwe na mamluki ndani ya walinzi wake.
Mungu anampigania
 
Hata wapishi nina hakika wamebadilishwa
 
Back
Top Bottom