Kwa mechi hizi zilizobaki unampa nani ubingwa wa Premier League?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Ligi Kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni, zikiwa zimebaki mechi kadhaa, Arsenal anaongoza ligi kwa alama 5 huku akiwa amecheza mechi moja zaidi ya Man City.

Man City yeye amebakiza mechi 10 wakati Arsenal amebakiza mechi 9.

Haya tuone kila timu imebakiza mechi zipi na baada ya hapo tabiri nani atakuwa bingwa wako.

Hizi ndizo mechi 9 alizobakiza Arsenal;


Na hapa chini ni mechi 10 alizobakiza Man City;


Ikumbukwe, Arsenal hana tena mechi za Europa League wala FA Cup wakati Man City atakuwa na mechi za Uefa na FA Cup.

Kwangu mimi licha ya ratiba ngumu ya Man City, nampa nafasi kubwa Man City kuibuka na Ubingwa EPL.

Kwani naona kabisa, Arsenal atapoteza dhidi ya Liverpool, Man City na kutoa droo na Newcastle.

Haya lete utabiri wako kutegemea na mechi zilizobaki za EPL...
 

Bas sawa…!!!
 
Katika hizo mechi za Arsenal zilizobaki ana kugingi cha kupata point kwa Brighton, Newcastlena Southampton hizi mechi anaweza poteza point asipokua makini hizo nyingine zilizobaki amapata point bila shida ma namuona kwenye nafasi ya kubeba ubingwa.

Same kwa Man City mechi yake na Brentford ndio inaweza kuwa ngumu kwake. Sion kipara akibeba msimu huu.
 
Sio alama 5 sema alama 8 halafu ndio useme ana mechi moja zaidi

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Arsenal ana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwakua ndio anaongoza ligi kwa points 8 vile vile ana mechi na City ambayo anaenda kuongeza tofauti kufikiab11 kabla mwezi huu kuisha ambapo Arsenal atakua kabakiza mechi 4 huku atakua akihitaji point 6 tuu kati ya points 12 kwamaana hiyo Arsenal anaenda kutwaa ubingwa na tiketi za mechi ya Mwisho dhidi ya Wolves zinauzwa kwa gharama kubwa ili watu washuhudie kombe linavyokabidhiwa

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Ko man city wenyewe watashinda mechi zote 10??
 

Kwenye hao uliowataja mmoja, kapigwa mmoja katoa sare mmoja alimfunga Arsenal kwa technic ndogo ila mkuu ukaona bora useme kwamba Arsenal anapoteza kwa hao wote [emoji23].
Mwaka huu haikwepeki Arteta anabeba EPL.
 
Anaongoza kwa point 8,punguza mihemko?????

Subiri city acheze kwanza ndio hii thread yako iwe active......
Manyumbu mtaita maji mma mwaka huu,naona mmejificha kwa city
 
Ngoja tutunze risiti mpaka mwisho wa msimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…