Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Wakuu mganga hajigangi, mimi kama Bush Dokta sio dokta wa mauzauza bali ni dokta Herbalist yaani wa mitishamba.
Sasa nina mtoto amezaliwa miezi 12 iliyopita. Mimi ni mweusi Tii, Mama ni maji ya kunde ila mtoto amekuwa maji ya kunde zaidi ya Mama yake.
Hata kama mimi sio msomi wa sayansi kubwa lakini naamini mchanganyiko wa mbegu nyeusi na maji ya kunde lazima ije zao ya kati kati.
Sasa nikawa najipa muda labda atabadilika kadiri muda unavyosonga lakini wapi ndio kwanza anazidi kuwa white. Sasa kuna siku Mama kaja kutembea na kumuona mtoto akiwa na kama miezi miwili hivi.
Nikiwa nimelala ndani nikasikia Mama anahoji Mke wangu akimuuliza kama stori tu kuwa huyo mjukuu anafanana na nani mbona ana kiwaraza? Mimi sina na mama yake hana. Tena akahoji mbona mweupe sana?
Ni kama kulikuwa na mahojiano serious ikafika mahali akamuuliza leta picha za wajomba zake tuone.
Hapa inaonekana Wife alimwambia anafafanana ujombani. Mama alimkomalia ndio wife akaja ndani kuniuliza kama nina picha za shemeji zangu kwenye simu. Nikamwambia sina basi ikaishia hapo.
Niliendelea kuwaza na kuwazua. Nikifikiria nimefanya uwekezaji mkubwa kwenye familia yangu na msimamizi amekuwa yeye siku zote.
Sijawahi mwambia ila tangu hapo sina hamu naye kabisa. Ni miezi 12 sasa. Hata uwezo wangu wa kuchapa kazi sasa unapungua nina stress kiasi.
Nimejaribu kuvumilia nimeona nije hapa nipate mawazo mawili matatu nianzie wapi?