Kwa Milioni 15 naweza kujenga nyumba ikakamilika na nikahamia?

Nyumba hata kama iwe kama kituo cha polisi yaani chumba na sebule tu inatosha ili nimkimbie Mama mwenye nyumba aisee

Hiyo hela inatosha kabisa.. unapata vyumba viwili na sebule..

Ila ni zile nyumba ndefu maarufu kama mabanda ya uani ( bati mgongo wa tembo ama nusu mgongo wa tembo style ).. hapo sebule inakuwa kati kati vyumba vya kulala ni pembeni ya sebule kushoto na kulia

Kwa hiyo hela unaijenga kali tu .. ya kuanzia maisha
 
Hiyo hela inatosha kabisa.. unapata vyumba viwili na sebule..

Ila ni zile nyumba kama ndefu kama mabanda ya uani.. hapo sebule inakuwa kati kati vyumba pembeni kushoto na kulia

Kwa hiyo hela unaijenga kali sana.. ya kuanzia maisha
Mpigie na hesabu ya Choo, shimo la Choo pamoja na kulijengea, pesa ndogo Sana hiyo, inaweza ikatoka lakin ambayo haijapigwa plasta wala sealing board, sakafu? Kifusi, hela ya ufundi? Maji?

Hembu orodhesha kila kitu pamoja na hela ya ufundi, kupaua na Choo nione hiyo kali Sana kwa hela hiyo inatokaje pamoja na madirisha na milango
 

Ni kweli hiyo hela inatosha kila kitu

Naongea kwa experience ya kujenga jenga hizo nyumba.

Huwa Ninajenga nyumba mara kwa mara.

Ninafanya biashara ya nyumba za kupangisha. Kama upo dar tembelea project zangu za nyumba ujionee

0754 003 715.
 
Kama kawaida yenu wajuaji jamii forum ambao bado mmepanga🤣🤣🤣
 
Kanunue ist yako uvimbe mjini, hizi nyumba za kujenga unahamia huku unaendeleza ujenzi sijuh Zina mapepo haziishagi alafu nyingi wanandoa hawaishi ugomvi humo ndani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…