Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Utatoaje msaada bila kujijenga? Au unamaanisha kua na maghorofa, luxury cars,
Nikipata hata 20k tu huwa siwezi kuila peke yangu yote
Nacho maanisha hata wenye nia nzuri ya kuwasaidia wengine kuna muda wanakwama kwa sababu wsnaharakia kusaidia wengine kabla ya kujiimarisha.

Baadae mambo yakiends vibaya lawama zinakua nyingi bila mpango maalumu.

Ila mtu akijijenga kidogo na akaanza kusaidia hata mambo yakienda vibaya haiwi changamoto sana
 
Utatoaje msaada bila kujijenga? Au unamaanisha kua na maghorofa, luxury cars,
Nikipata hata 20k tu huwa siwezi kuila peke yangu yote
Aisee HUWEZI kutoa msaada bila kujijenga.
Kujijenga kunakokusudiwa ni kuwa na SURPLUS PRODUCTION.
Nadhani unafahamu Kuna kipindi uchumi wako una decline,hiyo 20k unayoipataga Kuna kipindi inakwama kabisa. Sasa kama hukujijenga na haukuwa na surplus utajikuta unakwama wewe na ndugu zako pia wanaokutegemea watakwama kupitia wewe.
 
Baba yangu alikuwa mkarimu mpaka ikawa shida. Nakumbuka nyumbani kwetu tulikuwaga idadi ya watu inafika 27. just imagine, ndugu ni wengi mpaka basi. Yaani watoto mnalala chini kwa sababu wageni ni wengi..

Unakuta mwanamke katiwa mimba huko ni ndugu yetu anakuja na mimba yake anazalia kwetu na analea mtoto wake hapo hapo kwetu baba yangu hasemi chochote. Yani atamuhudmia huyo mwanamke na mwanae utafikiri yeye ndio baba.

Nilipofika form six nikawa mkali, hakuna watu kuja nyumbani kukaa tu...mzee wangu alishaanza kuzeeka akawa ananiangalia tu lakini tulipunguza idadi ya wakaaji wasio na kazi..
 
Simpaka waone hiyo potential 🀣🀣🀣

Kwa tabia za wabongo jiandae kuwaambia kuwa una watumikisha halafu hauwalipi
 
Ndio uwaweke ndugu !? Ndugu wa kibongo ni changamoto kmmk watakuibia vibaya sana halafu kuwa wajibisha utakuwa unaogopa Kuchukua hatua kwa gharama ya kuogopa kuuvunja ukoo

BTW wazo zuri sana ila nimpaka pale ndugu hao wakiwa wanajitambua vyema
 
Akili kubwa nakubali
 
Nakubali wazo zuri sana
 
Yaani unapata cheap labour halafu hujui kuwatumia?

Hebu walete kwangu huku uone watakavyonifugia Hadi njiwa...
 
Ndio maisha mliojijengea tangu enzi na enzi.
Kuubadili ni ngumu na uanataka maamuzi magumu bila kuangalia Ndugu watasema nini
Yeah ukiwa hujawahi kusaidiwa umelelewa na wazazi wako we komaa kukataa ndugu kwako, ila wewe uwe na wewe ulilelewa na ndugu alafu ufanikiwe wakitaka uwalipe fadhila kwa kumsaidia mtoto wao ni ngumu kuchomoa hata nafsi yako itakataa
 
Shida sisi waswahili tunapenda utegemezi badala ya kuinuliwa kiuchumi.
Yani usikute hata ukimwambia suala la kumsaidia ajitegemee anaweza kukuona una roho mbaya sana.
 
Hakikisha kila anae kuja kwako anakuwa sehemu ya kuzarisha.

Wasikae tu. Tengeneza mtandao mzuri wa biashara kisha kila mmoja mpe kazi kulingana na utalam na akili yake. Hakikisha ndugu wanakuwa tu chini ya uangalizi sio kuwapa rungu la kuendesha hizo biashara.
 
Mkuu umetisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Kuna muda huruma ikizidi huzaa uzembe.
Yani hapo ndugu wanajua hata wakilemaa vipi Kuna mtu wa kuwalea kivyovyote vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…