Kwa mliooa tukutane hapa

Kwa mliooa tukutane hapa

Preference zako kwa mahusiano ni tofauti na za wengine, vigezo vyako vya mke bora haviwezi kuwa sawa na vya mwingine kwa hiyo cha kukushauri wewe anglia unaeona anakufaa na amekidhi vigezo vyako weka ndani

Ukisema kila mtu aseme experience yake hapa, mwingine atakwambia alipenda tu kucha akaamua kuoa, mwingine atasema amempendea tabia, mwingine atasema amependa macho yake, mwingine atakwambia mke wake ana akili kwa hiyo ameoa ili apate watoto wenye akili na kuna wanaume wa dar watakwambia wife kwao wana uwezo kwa hiyo ameoa ili apate urahisi wa maisha


Sijui umeelewa lakini, au niongeze sauti
Anyways, wenye wake zao wanakuja
[emoji16]anyway atakua aeelewa lkn
 
Kijana karne hii unaoa ili iweje.!???

Yafaa nini kuweka furaha yako rehani na kukaribisha stress...

Anyway mambo yenu nawaachia wenyewe
 
Kwenye kusaka mwenza utata ni mwingi Sana. Unaweza fika mahali ukahisi kuchoka kuchunguza tabia za wale unaowachunguza ili kupata alie Bora, matokea yake wote unaowachunguza kwa lengo zuri la kuoa unakutana na sintofaham mbalimbali ambazo ukizifikiria kwa undani unaona kabisa baadae unaweza kupata changamoto nyingi endapo utaridhia kukamilisha taratibu za uchumba na kuoa.

Wakati mwingine utakutana na watu watakwambia usichunguze Sana hakuna aliyekamilika na tena anaweza kuongezea kabisa kwamba ukimchunguza Sana Bata huwezi kumla na kwamba hakuna aliyekamilika.

Je mlioingia kwenye mahusiano ya mume na mke "anyway" yaani unamashaka lakini unahisi Kama umechoka kuchunguza mana kila unayeanzisha nae mahusiano Ni hola, then ukaamua tu kuoa ivo ivo mnasemaje kuhusu hili ?

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
Hiyo "anyway" kwenye ndoa haipo na haitakiwi kuwepo kabisa kwasababu kuoa/kuolewa kunamaanisha maisha yako, Kuna maanisha familia yako ambayo unaianzisha, Kuna maanisha furaha yako, na amani yako ukifikiria hivi utagundua Hilo neno "anyway" halina pa kukaa, na ukichagua mwenza kuangalia vigezo hivyo hautampata huyo "anyway"

Shida inakuwa kwenye vigezo tulivyojiwekea, tumejiwekea vigezo vya kimwili zaidi ooh nataka mweupe, ooh mwenye mguu wa bia, oooh mwenye makalioo, na Hawa dada zetu ooh nataka mwenye mwenye ABC mwisho unaishia kwenye hiyo "anyway" na hapa sijasema hivyo usiviangalie lakn unapoviangalia hivyo vigezo usisahau furaha, amani yako, Kuna mtu unamuangalia wa kawaida anakupa furaha ukiwa na yeye anakufariji, yaani unakuwa na amani wasiwasi na mashaka ya kuchapiwa huna anakupa kujiamini, kwa huyo utawaza kuitengeneza familia kuliko mambo mengine. Lakini ukioa ambaye umemuangalia kwa vigezo vya mwilini nakuambia utaishi maisha ya digidigi hata kama uchumi wako uko vizuri, maana kuna wengine "wajinga wajinga" wanafikiri eti ukiwa na Hela ndio ndoa yako itatulia nakuambia hela yako itatumika kuwanunulia boxa wengine na cha kufanya utakuwa huna

HAVE A GOOD DAY
 
Majuzi ijumaa nilienda kumuona babu akaniambia mbona unachelewa kuoa nikamwambia bado namchunguza akacheka sana akaniambia huwezi kumchunguza mwanamke maana hutaona baya kwa sasa ila ukishaoa ndo utajua ukweli wake halisi kama sio mke kutoka kwa Mungu utaimba hallelujah tu kikubwa omba mke mwema basi kumchunguza mtu ngumu.
Babu kamaliza.
 
Back
Top Bottom