Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

Mkuu ukiwa na shida huna choice
 
Hata mm niliona hilo tangazo nilisikitika sana.. na serwkali ipo!
 
kuna mishahara miwili kwa wahindi, mshahara wa kwenye payroll ndo huo hapo umetangazwa, then mwisho wa mwezi unachukua mwingine kwa cashier then 130,000 unapelekwa bank then unajazia. hii inafanya kodi ya mwajiriwa kuwa ndogo na kumpunguzia mwajiri utitiri wa kodi.
 
Duh jamani hata mfanyakazi wa ndani anayelala na kula chakula anachokula bosi wake.. wala hapokei mshahara huo mdogo..

Na ile ya ujanja wa kupenya kwenye matundu ya sheria haikugusa nayo ina huhu..

Inasikitisha huyo tena na kazi ya udereva kwenda kulipwa kiasi hicho.. huku madereva wa watu binafsi wanaopata na mengi zaidi hadi lunch hawanunui wao kuanzia 350,000. Na wakifanya usiku au overtime pesa inaongezeka na Jumapili nayo mtu analipwa zaidi akihitajika.. kwa mwezi hata 500k mtu anabeba
 
Yaani ni shida
 
Huyu hastahili kuwepo hata Kwenye orodha ya matajiri wa wilaya yake. Labda Kwenye orodha ya wauaji kisaikolojia
 
usitudanganye na uafrica wako wa kinyonyaji! bora uwe na wafanyakaz wachache unaowalipa vizuri kuliko wengi unaowalipa kidogo! dhambi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…