DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Unaishi Tanga!?Mimi nina mshahara kama huyo jamaa ninaishi,niko kwangu,nina nyumba mbili, Sijawahi kulala njaa, mwaka huu january napeleka mtoto wangu English medium school,karo 2M,mwaka jana ndani ya miezi miwili nimekamilisha nyumba ya 13M.
Take home yangu ni 270K
Acha kuogopesha watu, jamaa kama anajiweza akope
[emoji122][emoji122][emoji2962][emoji2962][emoji3447]Mnaomshauri akope 25M
Mwambieni pia atalipa 47,318,177.1(47M),
Mwambieni katika hio 25M cash atakayopata ni 22.5M.
Mwambieni atakatwa 438,131.27 kila mwezi kwa miaka 9.
Mwambieni jumla ya riba atakayolipa ni
22,318,177.1.
Mwambie katika 47M atakayolipa,
Yeye atachukua 22.2M na 24.5M anawaachia Bank.
Mwambieni ni sawa kutoa 226,851 kila mwezi kwa miaka 9 kulipa riba tuu.
Mwambie hio pesa Akiamua kujitunzia mwenyewe angetumia miaka 4 kuipata, huku ⅓ ikibaki pale pale.
Akili Kukichwa.
noted champ, japo sina access na matichaKupitia hiyo salary jibane Sana u save mil 1 then anzisha biashara ya kuwakopa walimu wenzako laki moja kwa elfu 20 na laki mbili 40 Ila ukiwa na muda wekeza katika biashara ya mazao kuwa middle broker .
Katika hizo biashara zako ukiona zinaenda vizuri basi kachukue mkopo bank ambao sio mkubwa na ambao hautaathiri mshahara wako Sana. Then bust biashara yako.
Kuhusu kujenga usijenge kipindi hiki ambacho haujawa na financial freedom , bali anza kujenga kipindi ambacho utakuwa unaingiza hela kila siku. Ila waweza Ku-invest katika viwanja tu.
Hahahahaaa[emoji12][emoji12][emoji12] kama huna pesa kuliko kuvaa kadeti bora utimbe zako Yale masulu kama ya wahindi yaliyokaa kama fuko la mashine yaani pajama sio pajama halafu chini raizoni,
Bora uonekane hamnazo.
Sio wahuni mkuu,wanasaidia Sana wafanyakazi mbona.Daah Bayport apogee kabisaa wale si wahuni tu au
sio poah afsaSio wahuni mkuu,wanasaidia Sana wafanyakazi mbona.
Unapochukua mkwanja,ni nderemo na vifijo.
Kurudisha Sasa ndo pale unaanza kupiga miayo.
Kiufupi mkopo ni mkopo tu,kikubwa mnalindwa na salary.
270k kwa mwezi? Unaweza kutufunza vionjo vya bajeti yako ya siku?Mimi nina mshahara kama huyo jamaa ninaishi,niko kwangu,nina nyumba mbili, Sijawahi kulala njaa, mwaka huu january napeleka mtoto wangu English medium school,karo 2M,mwaka jana ndani ya miezi miwili nimekamilisha nyumba ya 13M.
Take home yangu ni 270K
Acha kuogopesha watu, jamaa kama anajiweza akope
Huyo ni kada kindakindaki wa ccm wala usihangaike. Anakula keki ya nchi hiyo 270k ni zuga tu270k kwa mwezi? Unaweza kutufunza vionjo vya bajeti yako ya siku?
Gross au basic salary ni the same mkuu!Haujafafanua kinagaubaga kuwa hiyo 765k....ni basic salary!?, nett pay!? ... Ama gross pay!?
Khahahaha,mkuu hakuna mkopo nafuu Wala mbovu.sio poah afsa
Biashala = BiasharaKhah
Khahahaha,mkuu hakuna mkopo nafuu Wala mbovu.
Mazingira tu mkuu.
Ila mikopo sio mizuri labda uwe unaifanyia biashala.
Mkuu Kiswahili ni lugha yetu ya mawasilisno na hapa sio darasani mkuu.Biashala = Biashara
Asome vizuri kisha akueleweUsimdanganye mwenzio. Sababu yake kuu ya kukopa ni NJAA, kasema mwenyewe.
Anataka akope mkopo wa juu zaidi kuweza kukopeshwa kwa sababu ana njaa.
Mtumishi unatakiwa ukope ukiwa na biashara au mradi wako ambao umefanya kwa hela za kudunduliza au hela ya kupata kwenye chanzo kingine ila sio mkopo wa riba. Ufanye kwa muda hata zaidi ya mwaka, uanze kupata faida na hasara uzoee hicho kitu, ukue uache kutumia hadithi na simulizi badala yake utumie uhalisia na uzoefu.
Baada ya hapo ukope ili kuendeleza na kukuza hiyo shughuli. Tena napo haukopi mkopo wa kiasi cha juu kabisa kinachowezekana.
Anza kufuga mbuzi au nguruwe, anza kununua mazao kwenye msimu, anzisha biashara ya miche ya miti na matunda, anzisha duka la spare parts au nguo au viatu au vyombo vya ndani, etc. Fanya kwa muda fulani mpaka uwe na uzoefu kisha ndio ukope benki kuanzia kiasi kidogo na unapanda taratibu.
Miaka kadhaa baadae utakuwa na uwezo wa kukopa hata 70M bila wasiwasi. Sio unapigwa njaa unakopa kujimaliza ili ununue sabufa na pikipiki used ya Sanya, na TV ya Aborder ukutani, hela inayobaki ukarabati nyumba.
mkarimani feki dunia sio mama yako, miaka minne ijayo hakuna atakayekuhurumia leo hii ukikopa kisa una njaa.
Unapokosea halafu mtu akusahihishe ni jambo la busara sana.Mkuu Kiswahili ni lugha yetu ya mawasilisno na hapa sio darasani mkuu.
Sawa msomi.
Mikopo mingi ina riba, ndio faida kwa hiyo kuepuka riba kwenye mikopo ni ngumu sanaAsikope kwasababu ana idea ya biashara .....hapa ndipo watu wengi wanapofeli katika mikopo.Kopa ili kuikuza au kuitanua biashara ambayo tayari unaendelea kuifanya, inakulipa vizuri na una uwezo wa kuzikabili changamoto zake.
Unakopa ili kuongeza uzalishaji au uingizaji wa bidhaa sokoni. Usikope ili kuanzisha biashara utakuja kukutwa na kitu kizito hutoamini.
Mfano labda ulikuwa unaingiza mzigo mchache unauzika kwa wakati na bado kuna demand kubwa ya uhitaji wa bidhaa yako kwa wateja. Hapa unaweza kukopa ili uwe na uwezo wa kuingiza mzigo mkubwa zaidi ili uongeze faida pia.
Ukifanya hivyo fasta utaweza kuulipa mkopo na utaona manufaa ya mkopo. Mwisho kabisa nakushauri uepukane na mikopo yenye Riba.
Kumbuka RIBA sio faida. Riba ni laana . Wengi wamefeli katika biashara kutokana na kujihusisha na mikopo yenye riba.