Usimdanganye mwenzio. Sababu yake kuu ya kukopa ni
NJAA, kasema mwenyewe.
Anataka akope mkopo wa juu zaidi kuweza kukopeshwa kwa sababu ana njaa.
Mtumishi unatakiwa ukope ukiwa na biashara au mradi wako ambao umefanya kwa hela za kudunduliza au hela ya kupata kwenye chanzo kingine ila sio mkopo wa riba. Ufanye kwa muda hata zaidi ya mwaka, uanze kupata faida na hasara uzoee hicho kitu, ukue uache kutumia hadithi na simulizi badala yake utumie uhalisia na uzoefu.
Baada ya hapo ukope ili
kuendeleza na
kukuza hiyo shughuli. Tena napo haukopi mkopo wa kiasi cha juu kabisa kinachowezekana.
Anza kufuga mbuzi au nguruwe, anza kununua mazao kwenye msimu, anzisha biashara ya miche ya miti na matunda, anzisha duka la spare parts au nguo au viatu au vyombo vya ndani, etc. Fanya kwa muda fulani mpaka uwe na uzoefu kisha ndio ukope benki kuanzia kiasi kidogo na unapanda taratibu.
Miaka kadhaa baadae utakuwa na uwezo wa kukopa hata 70M bila wasiwasi. Sio unapigwa njaa unakopa kujimaliza ili ununue sabufa na pikipiki used ya Sanya, na TV ya Aborder ukutani, hela inayobaki ukarabati nyumba.
mkarimani feki dunia sio mama yako, miaka minne ijayo hakuna atakayekuhurumia leo hii ukikopa kisa una njaa.