Kwa mshahara wa Tsh. 765,000/= nikizama benki naweza kopesheka kiasi gani?

Kwa mshahara wa Tsh. 765,000/= nikizama benki naweza kopesheka kiasi gani?

Biashara ni rahisi kwenye karatasi na sio field haupo mwenyewe.
Ukiloose kwenye businesses ndo utajua ujui.
Bora upoteze pesa kwenye ngono haumi kuliko kupoteza kwenye project utaumia maisha Yako yote.
Bora ukope utie kwenye ardhi Haina hasara unacheza na time TU mkopo ukiisha na ardhi imepanda thamani unapata faida mara mbili.
To be successful one has to fail several times... Unapoanguka kwenye biashara, kuna somo unalipata, ambalo litakufanya usirudie kosa. Ndiyo maana kama huna uzoefu na biashara don't start big, anza mdogo mdogo ili upate uzoefu. Huwezi anza biashara ya bodaboda kwa kuchukua mkopo na kununua bodaboda 4 kwa mpigo, ilhali huna hata uzoefu wa kusimamia bodaboda moja. Ukweli mwingine ni kwamba siyo kila mtu ana uwezo wa kufanya biashara. So kama ukiona biashara huwezi waweza kopa na kujenga hata fremu chache ukakodisha au kununua shamba ukawa unalima au kukodisha.
 
Nawishi kuchukua loan kozi life limekua likinichapa sana, wataalamu nipeni uzoefu sana.

Je, nitaweza kopesheka shingapi kwa benki ya CRDB kwa hio salary?
Ukitaka kutembea na 1 out of three CRDB utakopa 22m watakata bima, processing fee. Kodi utabaki na 19.5m halafu ukae kwa kutulia ulambwe 389000 Kilamwezi kwa miaka 8 JUMLA ULIPE 37m
 
Nilichosema take home hiyo huwezi kufanya hayo unayoyasema labda uwe na channel ya wizi.

Million 2 cash utaitowa wapi?
Usikalili mkuu,sio kila mtu aliyefanikiwa anaiba lakini pia sio kila aliye na mikopo na kubaki na 270K kama kipato cha mwezi ana maisha magumu,Tatizo mnajipa title za wasomi ila uwezo wa kupambanua mambo na kuyaweka katika uhalisia ni mdogo
 
Usikalili mkuu,sio kila mtu aliyefanikiwa anaiba lakini pia sio kila aliye na mikopo na kubaki na 270K kama kipato cha mwezi ana maisha magumu,Tatizo mnajipa title za wasomi ila uwezo wa kupambanua mambo na kuyaweka katika uhalisia ni mdogo
Tusiandikie mate, weka mchanganuo hapa wa 270k.
 
Huyu mtu akichukua mikopo 2 ya 25m akiwa kazini mpaka anastaafu atakuwa ametumia miaka 18 kulipa riba za mikopo

Mikopo ni wendawazimu
Miaka yote ya kazi anafanya kazi ya kulipa mkopo aliokopa 50m daah aisee riba za mikopo ni balaa ndio maana kutoa umasikini sio mchezo inatakiwa kujitoa kweli...
 
Back
Top Bottom