Mkuu samahani mimi nitaenda nje ya mada lakini ni kwa manufaa yako. Kwanza uelewe hakuna maisha marahisi huku duniani labda ushinde bahati nasibu. Kwa pesa uliyonayo hata kama ni take home usichukue mkopo labda kama una kipato kingine vinginevyo utaishi kwa aibu.
Sasa nashauri tafuta kitu cha ziada ufanye nje ya muda wa kazi au soma kozi fupi upate skills za kujiajiri nje ya muda wa mwajiri. Nakupa mifano ifuatayo.
1. Kuna rafiki yangu anafanya kazi CRDB mkoa X yeye wakati wa wiki end anafanya kazi ya landscaping kwenye nyumba za watu.
2. Nina rafiki yeye ni Mwalimu lakini alisoma kozi fupi ya hotel management kwa hivyo yuko hotel X anaingia usiku daily asubuhi yuko kwenye kazi ya umma ya serikali.
3. Nina mtu namfahamu aliwahi kufanya kazi kwenye kanisa X lakini usiku alikua Mlinzi kwenye Nyumba binafsi ya mgeni kutoka nje.
4. Soma graphic design tafuta digital marketing ujitangaze. Utafanya kazi zako baada ya muda wa mwajiri.
5. Mimi nilibahatika kusoma shahada ya pili enzi za ujana wangu kwa hivyo niliwekeza kwenye huduma ya research za shahada ya pili na ya tatu.
NB: usikope kama Huna kipato kingine utavaa kadeti iliyopauka hadi kwenye zipu.
Sent from my SM-A025F using
JamiiForums mobile app