Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Hardware
 
Muheshimiwa kumbe njia unayoo
Kwanini usiingie kwenye nguo?
System unayokabisa apo
Au kuna changamoto ambazo umeamua kuachana nazo
Binafsi kama kwenye familia kuna system ni kheri upite nayo kuliko uanze moja
Asante, mzee anauza jumla hapo mwanza changamoto ya nguo ili update faida lazima ujikite kuuza kwa jumla rejareja inachelewesha sana, purchasing power ya kigoma ni ndogo mno na sioni wanaouza jumla hapa wengi ni rejareja watu ni wachache.
 
Sawasawa mkuu.
 
Kama Kuna ukweli hapo!
 
Kwa hiyo mkuu unadhani nidhamu aliyokuwa nayo mama yako miaka hiyo ndio utaipata kwa hawa wanawake wa sasa wenye tamaa wanaoshindana mitandaoni kununua vitu vya anasa?
Tofautisha wake wa zamani na wa sasa,wake wa zamani kwa mfano ilikuwa hata ukiwalisha ugali dagaa au ugali matembele mwezi mzima walikuwa wanaridhika je hawa wanawake wa sasa wanaweza kuvumilia ndani kuwe na hela halafu ale ugali na maharage kila siku?lazima atachota hela akale kuku na kununua vitu vingine vya anasa
 
Piga issue ya nafaka, tafuta mawakala, wewe ingia vijijini mara moja moja sana na hakikisha umeweka mawakala, utatoboa.
 
Wewe ndo huna akili, hapo ukute mwenzako kakopa ndo kapata huo mtaji, akiacha hio kazi, mkopo utajilipaje..? Mbona una akili kama za wauza utumbo
 
Piga issue ya nafaka, tafuta mawakala, wewe ingia vijijini mara moja moja sana na hakikisha umeweka mawakala, utatoboa.
Yeah Kuna mtu alinambia hii, mfano debe la maharage vijijini ni 2000 unamwambia wakala Kila debe unampa 500, Sasa ni speed yake kutafuta then Kila weekend unaenda kuchukua mzigo.
 
Teacher, nenda na biashara ya simu na vifaa vyake. Halafu unaongezea ndani yake na huduma za kifedha. Hakika utanishukuru kwa huu ushauri.

Na uzuri umekiri mwenyewe machimbo yote ya hivyo vifaa pale Kariakoo unayafahamu. Kwa hii biashara ni rahisi kwako kuisimamia.

Achana na biashara kichaa ya mazao, na pia hiyo ya hardware ambayo kuna wateja wanataka wapelekewe bure mpaka site, hata mfuko mmoja tu wa saruji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…