Kwa mtazamo wa Kidini. Je, mwanamke anaweza kuwa Rais?

Kuna jambo limejificha kwani hata mchakato wa kuteua mgombea wa chama fulani umekiukwa!
Ke wanachakarika sawa lakini usaidizi kwa Me unabaki palepale la sivyo yanayotokea ulimwenguni kwa sasa yamesababishwa na Ke kutokufuata mipango ya Muumba wetu! Usagaji, ushoga nk vimejitokeza hadi kupigiwa chapuo kwa sababu ya kubadilika kwa mfumo wa maisha kwa kipindi hiki.
 
Bas nchi tutampa mumeo aiongoze bibie!
 
Hatuongozwi kwa mitazamo ys kidini ambayo nikandamizi kwa mwanamke. Mtu yeyote bila kujali jinsia mwenye sifa za uongozi anaweza kuongoza
 
1 Timotheo 2:12 "Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume"
Binadamu siku zote ni mnafiki wa hali ya juu!
Kila siku utamuona na vistatus vya Mungu, ingia kwenye kumi na nane zake ni hatari kupindukia. Haya mambo ya dini siku hizi yamebaki kama mambo ya kujipea moyo mambo yakienda mrama, na sehemu tu ya kujumuika!
 
KATIKA NGAZI ZA KISEREKALI MWANAMKE ANAWEZA KUWA RAIS, LAKINI KATIKA NGAZI ZA KIDINI MNAWEZA KUMBAGUA!
 
Samia amefanya vizuri mno, kuliko hata wanaume na midevu yao kama mabeberu.
 
Kwa hiyo SSH hafahamu hayo yaliyomo kwenye kitabu chenu??? Maana angekuwa ni Mgalatia angeweza kusema hiyo Quran haimuhusu.
Sheikh anazungumzaa katika 'context' ya kiimani..wa Dola Kiislamu inayoongozwa kwa Sharia, hazungumzii katika mfumo wa uongozi wa kisekula..
 
Dini gani kitabu gani?
Kwa upande wa wakristo Hakuna katazo Hilo, mwanamke anaruhusiwa kuwa mtume, nabii, rais, askari nk sijui kwa Islamic ila wakristo ni sawa watu wanatafsiri vibaya maandiko
 
Tuwaulize wakristu, ni kwa nini mitume wa Yesu hapakuwa na mwanamke? Basi Yesu alionyesha kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi. Hata Mungu nae alitoa tu ubavu wa mwanaume na kumuumba mwanamke, alionyesha kuwa mwanaume ndiye anaemuongoza mwanamke.
 
Kwa vile nchi yetu haina dini, urais wa Tanzania, hatutafuti imamu wala kasisi, na kwa mujibu wa katiba yetu, binadamu wote ni sawa, mtu yoyote anaweza kuwa rais!.
P
 
Tuwaulize wakristu, ni kwa nini mitume wa Yesu hapakuwa na mwanamke? Basi Yesu alionyesha kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi. Hata Mungu nae alitoa tu ubavu wa mwanaume na kumuumba mwanamke, alionyesha kuwa mwanaume ndiye anaemuongoza mwanamke.
Kwa vile rais wa Tanzania, hatutafuti mtume, mwanamke anaweza kuwa rais wa Tanzania.
P
 
Aliyekuambia kuna mwanamke anaongoza nchi ni nani. Kama yupo basi yeye yuko pale kama remote na mkono unaoshika hiyo remote uko Msoga kwa mtaafu asiyetaka wala kukubali kustaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…