Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,770
- 5,423
Nimejaribu kuichunguza Nchi yetu inavyoongozwa na mikakati tuliyonayo najiridhisha kuwa ni vigumu sana kupata maendeleo ya maana hata kwa miongo mitatu ijayo yaani comes 2050!
Sababu zangu ni hizi;
1. Elimu yetu ni duni sana kwa maana ya maudhui (contents) na inazalisha watu wenye maarifa madogo sana ambao hawajitambui na wasio na uwezo wa kuona mbali.
2. Viongozi wetu walioko katika nafasi za uongozi katika taasisi mbalimbali wana maarifa madogo sana (sisemi hawana vyeti) na hawana uwezo wa kuiangalia Tanzania baada ya miaka 50 au 100 ijayo ambapo tunakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 120.
3. Hatuna itikadi ya maana inayotuongoza katika mwelekeo wa Nchi yetu na viongozi wengi hawalijui hili ndo maana unaweza kukuta leo mwanasiasa huyu yuko chama hiki na kesho amehamia chama kile na unaona kabisa hakuna anachokiamini au kukisimamia ni bora kunakucha na ugali wake unaupata basi!
4. Tumezidiwa maarifa na mataifa yenye nguvu kiasi kwamba sasa wanatupangia hadi ni vitu gani tunapaswa kuvifikiria.Nguvu kazi ya Taifa (hasa vijana) haiko katika uzalishaji iko katika ku-bet na kujadili mambo ambayo hawana uwezo wa kubadili chochote kama mipira inayochezwa ulaya n.k.
5. Tumeshindwa kujenga mifumo imara inayoweza kujiendesha yenyewe bila kuingiliwa na watu wenye nia mbaya au malengo binafsi.