Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Toleo la 2019; Lema ametenda kosa (makosa) ya kinidhamu

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Toleo la 2019; Lema ametenda kosa (makosa) ya kinidhamu

Sijakusoma huko kwingine, lakini kutokana na mtiririko na mpangilio ulioanza nao huku juu, sina shaka yoyote kwamba hili ni andiko lenye uzito stahiki; tofauti kabisa na mijadala mingi zinazoanzishwa humu jamvini.

Kwa vile sijasoma huko chini, kwa sasa nina haya machache kueleza anachokifanya Lema.

Lema ni kama amekosa subira. Amesubiri sana kuona yale aliyoanzisha mwanzo kuhusu Makamu Mwenyekiti, lakini haoni hatua zikifuatia jambo lile.
Ni kama chama kimempuuza; mbinu ambayo nawasifu sana uongozi wa chama kutoiangukia harakaharaka ili mtafaruku utokee.

Wakati akishajuwa kwamba tayari nafasi yake ndani ya chama tayari ni tete, sasa kajitokeza kimoja, waziwazi, kama kuchokoza vile ili mpango uliosukwa kukivuruga chama wakati kiongozi mkuu hayupo utimie.

Pengine kwa sasa hivi mimi nitatofautiana kidogo na wewe juu ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya Lema kwa mara moja kwa kukiuka miongozo ya chamma kama ulivyo eleza.
Mimi napendekeza njia ile ile iliyomvuruga akili hadi kufikia hatua hii ya kujilipua, yaani waendelee kumpuuza kama hana athari zaidi ya huko kuropoka anakofanya maksudi ili achukuliwe hatua za kinidhamu.

Lakini kama chama kinapima na kuona kwamba kuendelea kwake kuwemo ndani ya chama kuna athari kubwa na hatari zaidi, ninakubaliana na wewe hatua za kuwajibishwa zichukuliwe haraka..

Kisichokuwa na mashaka yoyote tena, ni kwamba Lema sasa hivi anafanya chokochoko za wazi akiwa na matumaini kwamba hizo ndizo zitakazoanzisha vurugu ndani ya chama kwa manufaa ya anaoshirikiana nao kwa lengo hilo.

Lema is on a mission, there's no doubt about that.
Raha yake Lema hayuko peke yake, viongozi wengi ukitoa Heche na genge lake la wanaharakati wanamuunga mkono.
 
gentleman,
don't expose more how shallow you are in constitutional issues.

you better choose to stay quiet, or use other political ways to show up your hates against Godbless Lema's freedom of speech and opinions plz 🐒


Vipi nchimbi hakufanya freedom speech ?
 
Lema anapaswa kuliwa kichwa kwa mtazamo wangu.
He was being sacrificed a lot and a target man for wanaharakati

Ametuelewesha na amesimama kiume

Kama mlimsapoti Nchimbi, why LEMA aonekane msaliti?
 
Hakuna kosa lolote alilofanya, ameongea ukweli tupu
Haijalishi kaongea ukweli au uongo..

Kosa ni kuongea nje ya utaratibu akijua kuwa yeye si mwanachama wa kawaida bali ni kiongozi mkubwa ndani ya chama..

CCM ni wahuni na ni hayawani waliokubuhu lakini hakuna kiongozi anayeweza kufanya kama alovyofanya Lema na akabaki free..

Lema atakinywea kikombe alichokichagua Ili ajue kuwa hakuna mtu alliye juu ya taasisi...
 
Kama ni hivyo basi msimamisheni uanachama wa CHADEMA, kisha mumfukuze.
It will be done very soon..

Anajua kuwa kakosa lakini anajua Kuna shimo analolitegemea na ndiko alikojifichia...

We're digging it, and soon he will himself find into it..,
 
Anachofanya Lema,alichofanya Mbowe,Selasini,na Mrema,hizo ndio tabia halisi za wachaga
 
Raha yake Lema hayuko peke yake, viongozi wengi ukitoa Heche na genge lake la wanaharakati wanamuunga mkono.
Kwa mtu kama wewe kujuwa hayo unayosema haishangazi hata kidogo!
CHADEMA imekaa zaidi ya mwaka mzima bila kiongozi wake mkuu, bado Samia na Genge lake wakashindwa kukisambaratisha chama. Sasa hii dakika za mwisho ndipo mnaota kumtumia mamluki mmoja ambaye alijulikana toka mwanzo, mkadhani ndiye atakayemaliza kazi?

CHADEMA baada ya Mbowe, ni chama tofauti sana na ile takataka aliyokuwa akiitumia Magufuli.
 
Kwa mtu kama wewe kujuwa hayo unayosema haishangazi hata kidogo!
CHADEMA imekaa zaidi ya mwaka mzima bila kiongozi wake mkuu, bado Samia na Genge lake wakashindwa kukisambaratisha chama. Sasa hii dakika za mwisho ndipo mnaota kumtumia mamluki mmoja ambaye alijulikana toka mwanzo, mkadhani ndiye atakayemaliza kazi?

CHADEMA baada ya Mbowe, ni chama tofauti sana na ile takataka aliyokuwa akiitumia Magufuli.
Chadema hii inayoongozwa na Mange na Hilda Newton? Kuna mtu kaipigania chadema kama Lema? Lema amekaa jela muda gani kwa ajili ya chadema? Chadema haina kiongozi sasa hivi, CHADEMA inaongozwa na hoja za kiupuuzi za Mange na Hilda.
 
Tuanze kwa kuangalia MAKOSA YA KINIDHAMU kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA (2019).

Katiba ya CHADEMA inayoshughulikia nidhamu ni "SURA YA TANO, IBARA YA 7 na IBARA YA 8."

IBARA YA 7: NIDHAMU YA WANACHAMA
7.1 - Kila mwanachama ana wajibu wa:
(a) Kuitii na kuheshimu Katiba ya CHADEMA.
(b) Kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya chama
(c) Kulinda siri na mali za chama.

7.2 - Makosa ya Nidhamu
(a) Kukiuka Katiba na miongozo ya chama.
(b) Kuhujumu chama, kusambaza propaganda za kukichafua chama.
(c) Kugombea nafasi yoyote ya uongozi nje ya utaratibu wa chama au kupitia chama kingine
(d) Kutoheshimu / kupuuza msimamo wa chama Bungeni, Serikalini au Baraza la Madiwani
(e) Kujihusisha na vitendo vya rushwa, ubadhirifu, uhalifu wa kutia aibu.
(f) Kuanzisha au kuhamasisha makundi yanayolenga kuvuruga umoja wa chama.

HOJA YANGU
Kufuatia Press Conference ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Godbless Lema, aliyoifanya leo tarehe 01/11/2026, kwa kuitisha waandishi na kuzungumzia mambo yanayomhusu yeye na Chama/Wanachama na Viongozi wengine ndani ya chama; kwa uzito, matamshi na misimamo yake kwenye press conference hiyo; ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, vifungu vufuatavyo;

7.1 (a), Kuitii na kuheshimu Katiba ya CHADEMA.
7.1 (c), Kulinda siri na mali za chama.

Kwanini hajaheshimu Katiba; Lema (Kama Mjumbe wa Kamati kuu), anafahamu namna utatuzi wa migogoro na taratibu za utoaji wa maoni ndani ya chama.

Kwanini ametoa siri za chama; Lema amejadili kwa uwazi, mambo yanayohusu viongozi wenzake wa kamati kuu. Lema hakupaswa kutangaza kwamba, Mjumbe mwenzie (Joseph Mbilinyi), amekata tamaa ya kuwa kiongozi wa chama. Hapa anamsemea mbele ya umma, mtu mwingine ambaye pia ni kiongozi (Mjumbe wa Kamati kuu). Hili ni kosa, hii ilikuwa ni siri ya chama na siri ya viongozi hao wawili.
Hapa Lema anataka kutengeneza makundi, au kuonyesha anaungwa mkono na viongozi wenzie katika kutenda kosa lake.

Kosa hili lipo katika;
"Ibara 7.2 (Makosa ya Nidhamu), kifungu (7.2 (b), "Kuhujumu chama, kusambaza propaganda za kukichafua chama".

Na, ibara 7.2 (f) "Kuanzisha au kuhamasisha makundi yanayolenga kuvuruga umoja wa chama"

Utaona; Lema tayari anakusudia kuigawa kamati kuu, au kupata uungwaji mkono wa madai, misimamo na ushauri wake kwa kuwaingiza watu wengine, ambao hawakuwepo kwenye press conference yake. Ambao pia ni viongozi wa Kamati kuu.

MSINGI WA MAKOSA YA KINIDHAMU YA LEMA NI MSINGI WA UONGOZI

1. Huwezi ulalamikia uongozi ambao wewe ni sehemu yake.
2. Lema ni kiongozi (Mjumbe wa Kamti kuu, ambacho ni chombo cha mwisho kimaamuzi ndani ya chama. Kwa mantiki hiyo, Lema anabeba dhamana ya kutunza siri, kufuata katiba na misingi ya chama bila kujali press yake ina ukweli au malalamiko kiasi gani dhidi ya uongozi ambao yeye (Lema), ni sehemu yake kimaamuzi na kiuendeshaji.
Kamati kuu ndio inayoongoza chama, kwa hiyo kama kulikuwa na maamuzi, ambayo, anaonyesha kutoyakubali leo, basi yeye alikuwa sehemu ya maamuzi hayo; maana hakuna sehemu kaonyesha au kasema aliwahi kuweka pingamizi kwenye vikao halali ambavyo yeye anashiriki na akashindwa kwa kupigiwa kura.

3. Lema kama kiongozi wa juu, ana jukumu la kutunza msingi wa chama wa kikatiba, wa "kutatua migogoro kwa utaratibu wa kichama, ambao umetajwa na Katiba ya CHADEMA (Sura ya Tano) kupitia vyombo halali vya chama.

4. Lema kama kiongozi; Kama alikuwa na mgogoro/dukuduku/shutma dhidi yake alipaswa kufuata utaratibu wa kichama na kikatiba kutafuta la masuala hayo. Kuitisha press conference ni wazi, haukubali au kwa makusudi ameamua kuukwepa utaratibu wa usuluhishi wa migogoro ndani ya chama, na kwa makusudi anataka kuwa "Mkubwa kuliko chama".

5. Chama kina uongozi halali, ambao yeye (Lema) anawajibika kwake. Kitendo cha yeye (Lema) kutoka nje kujibu shutuma akiwa kiongozi.

6. Katika press conference yake; hajasema popote kama amewahi chukua hatua za kukihusisha chama dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwake. Hajaelexa ni kikao gani, amewahi shauri, kutoa maoni (aliyoyatoa leo), au kulalamika dhidi ya shutuma juu yake. Hapa tayari, anakuwa ametenda kosa la kinidhamu ambalo lina adhabu "punishable" kwa mujibubwa Katiba ya CHADEMA kama tulivyoona huko juu.

Tafsiri ya press ya Lema ni kwamba; Lema ametoka nje kukishauri chama, kukikosoa huku akiwa sehemu ya uongozi huo, huu ni usaliti dhidi ya uongozi.

Ni Kiongozi anaelalamika, anaeshauri dhidi ya uongozi wake mwenyewe. Kwa presss yake; haamini uongozi ambao yeye ni sehemu yake; hivyo kaamua kuupinga na kuushauri akiwa nje, huu ni usaliti wa wazi juu ya Kamati Kuu na chama ka ujumla, na kosa la kinidhamu la wazi kabisa kwa kiongozi wa juu kama yeye.

NINI KINAPASWA KUFANYIKA DHIDI YA LEMA.
Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Ibara ya "7.4 - Utaratibu wa Nidhamu (Due Process)"

Mara baada ya kuthibitika/kuibuliwa kwa makosa ya kinidhamu; Kamati ya Nidhamu inaketi mara moja kujadili suala hilo na utaratibu ni huu;

Ibara ya 7.4 - Utaratibu wa Nidhamu (Due Process)
Hakuna adhabu bila:
  • Mwanachama kupewa hati ya mashitaka kwa maandishi
  • Kupewa siku 14 kujibu / kujitetea
  • Kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu

KUHUSU ADHABU
Katiba ya CHADEMA inaelekeza adhabu zifuatazo kwa kadili Kamati itakavyoona inafaa.

7.3 - Aina za Adhabu*
Ibara 7.3.1 hadi 7.3.5:
1. Onyo
2. Karipio kali la maandishi
3. Kusimamishwa kushiriki shughuli / uanachama kwa muda usiozidi miezi 12
4. Kuvuliwa nafasi ya uongozi ndani ya chama
5. Kuvuliwa uanachama kabisa

7.7.16 (u) - Mamlaka Maalum:
Kamati Kuu ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kumvua uanachama Mbunge, Diwani wa Viti Maalum, na Kiongozi wa Taifa. Uamuzi wake ni wa lazima kutekelezwa mara moja lakini mhusika ana haki ya kukata rufaa._

MY TAKE; Lema anamakosa, lazima chama kiweke historia sawa. Chama hakipaswi kufumbia macho makosa kama haya ya makusudi ta viongozi, bila kujali uhuru wa maoni, unaoambatana na Katiba ya chama. Hakuna mtu mkubwa kuliko chama/taaasisi. Sheria ichukue mkondo wake. Lema asionewe haya, bila kujali chama kipo kwenye hali gani ya kisiasa, lazima chama kitunze misingi yake kwa nguvu na wivu mkubwa sana.
Ikiwa àtakùtwa n̈a hatia kwa mujibu wa katiba ya chama,ahùkumiwe na chaama kulingana na mazingira ya sasa ya taifa letu na muktadĥà wa siasa ndàni ya taìfa letu.Bila kupuuza habari za kùunuliŵa na kuùnga juhudi mķono.
 
Chadema hii inayoongozwa na Mange na Hilda Newton? Kuna mtu kaipigania chadema kama Lema? Lema amekaa jela muda gani kwa ajili ya chadema? Chadema haina kiongozi sasa hivi, CHADEMA inaongozwa na hoja za kiupuuzi za Mange na Hilda.
Hiyo CHADEMA unayoikumbuka wewe siyo hii inayowanyima usingizi nyinyi.

Njia zote za kuikabili CHADEMA ya sasa zimeshindikana, sasa mnabaki kupitia huko uchochoroni kwa wanaharakati mkifikiri mtafanikiwa.

Hata hivyo najuwa napoteza muda wangu bure kueleza chochote kwa mtu kama wewe.
 
Back
Top Bottom