Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Hapana kiongozi HAUPO SAHIHI. Katiba inamruhusu Rais kumteua mtanzania yeyote katika cheo ambacho Rais anateua, mfano mnenguaji wa bendi, Dj , Hawala, au mchezaji wa mchezo wowote anaweza kumteua kuwa mkuu wa wilaya au katibu tawala ili mradi tu AONE INAFAA
 
umesema mwenyewe katika cheo ambao rais anateua!mimi nimeleta miongozo,wewe umeleta nini?
 
Mkuu Sunzu shukran sana kwa kuweka nondo penyewe. Lakini ujue hali halisi ya nchi ni kuwa kauli na uamuzi wa rais ndio sheria kuu ya nchi. Yeye ndiyo anajua kilicho bora kwa nchi. Bila shaka huwa unasikia wengi wakijieleza wanatekeleza matakwa ya rais - sio sera, sheria wala katiba. Si kuhusu madawati, elimu bure, kulipa kodi, kuanzisha viwanda, n.k.

Hivyo, usipoteze sana muda na vilivyo katika makaratasi labda kwa kutaka kutuelimisha kama ulivyofanya hapa. Tuna safari ndefu sana kufikia mfumo wa utawala unaoenda kwa sheria na kanuni maalum badala ya kutegemea utashi wa mtu binafsi.
 
Hivi mmesahau kuwa wakati wa kampeni mahali fulani mkuuu wa kaya aliwaomba wana CCM wasigombane kwenye kura ya maoni kwani akishinda urais kazi zipo nyingi tu kwani yeye ndie atakuwa mkuu wa kaya?
 
umenipatia ushauri mzuri,i admit
 
Sijawahi kuona nafasi ya DAS ikitangazwa magazetini. Hao waliokuwepo walipatikanaje? Kama waliteuliwa, basi uteuzi ni uteuzi tu. Mtu anaweza kuteuliwa kutoka nje akaingia kwenye utumishi wa umma. Sidhani kama sheria inamzuia mteuaji kuwa lazima ateua miongoni mwa watumishi wa umma. Labda hilo ndo ulitakiwa kuliweka wazi. Hata hivyo sikuwahi kuona nafasi ya DAS au RAS ikitangazwa kwa ajili ya kupata watu wa kuajiriwa ngazi hiyo!!
 
hata hivyo hongera sana mkuu kwa kupata uDAS,muombe Mungu jamaa wasijishtukie,wazibe masikio la sivyo watakutengua.Makosa yaliyofanywa kwa Amoni hajawezi kuhalalisha makosa ktk uteuzi wako.Usitulaumu sisi,laumu kanuni na sheria
Umeishiwa hoja sasa unaanza kuhisi hisi watu hovyo. Maswala ya huyu ni fulani hayaruhusiwi hapa JF. Rudi kasome kanuni ambazo tumejiwekea hapa jukwaani.
 
Ukiachilia standing order Kuna muundo wa utumishi (scheme of service) ambao unaainisha sifa na vigezo vya kushika nafasi husika. To the best of my knowlede uteuzi wa baadhi ya Ma DAS akiwemo: Siyantemi, Casilida, Mtera, Asenga na wengine wenye kufanana na hao kama wapo ni batili kwa mjibu wa muundo wa utumishi


Ingeleta Maana sana wale wakurugenzi wa halmashauri walioteuliwa U-DC Hivi karibuni wakashika nafasi za U-DAS alafu hawa Vijana wakapewa U-DC

Tukiwaruhusu wanasiasa wakaharibu taratibu za utumishi wa umma tutakwama tu kama nchi.
 
nafasi ya DAS haitangazwi ni nafasi ya uteuzi. Ila mpaka ufikie kuteuliwa Kuna vigezo ambavyo Lazima uwe navyo kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa mtumishi wa umma. Usiliangalie hili kwa mtazamo wa kisiasa hapa Kuna kosa la kikanuni limefanyika
 
Baadhi yetu tumekuelewa sana...pongezi kwa ufafanuzi uliotoa hapa...Hapa mimi nimeshangazwa mno...lakini mimi naishia kushangaa tu...kilichotokea ni HATARI...Nadhani wamedhamiria kumhujumu Rais...Ni kitu cha ajabu kimefanyika...
Muelimishe na " lizaboni' naona bado kalala
 
nafasi ya DAS haitangazwi ni nafasi ya uteuzi. Ila mpaka ufikie kuteuliwa Kuna vigezo ambavyo Lazima uwe navyo kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa mtumishi wa umma. Usiliangalie hili kwa mtazamo wa kisiasa hapa Kuna kosa la kikanuni limefanyika

Siasa mbali na mimi. Hiyo kanuni inayosema kuwa mtu kabla ya kuteuliwa kuwa DAS ni lazima awe mtumishi wa umma kwanza ndo hujaiweka hapa. Ukiangalia pale penye qualifications ulizoziweka hapo juu hakuna mahali pamesemwa kuwa lazima huyo mtu awe ameshakuwa mtumishi wa umma kwa kipindi kadhaa au at all.
 
Mkuu kote ni mchemsho tu hata kwa huyo mpanju. rais anavunja sheria , kanuni kwenda mbele.
 
nafasi ya DAS haitangazwi ni nafasi ya uteuzi. Ila mpaka ufikie kuteuliwa Kuna vigezo ambavyo Lazima uwe navyo kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa mtumishi wa umma. Usiliangalie hili kwa mtazamo wa kisiasa hapa Kuna kosa la kikanuni limefanyika

Madaraka ya rais wa Jamhuri kwa mujibu wa katiba iliyopo hayana mipaka. Anao uwezo wa kumfanya mtu yeyote ambaye hakuwahi kuwa mtumishi wa umma - kuwa mtumishi wa umma. Kisha akamteua kwenye nafasi yoyote anayoitaka. Angalia kuna precedence kibao tu huko nyuma ambako watu wametokea nje ya kazi za umma wakateuliwa kuchukua nafasi ambazo wengi tulitarajia watu wapande kuzifikia. Hilo sioni kama ni jipya! Aliowateua wote wana qualifications? Sidhani kama unaweza kutumia sheria kupinga uteuzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukashinda; iwe mahakamani au kwenye vyombo vya habari!!
 
Hv ni nani hata hivyo anaweza kuthibitisha kuwa huyo mteule hakuwa mtumishi wa umma?Mtu aweza kuutumikia umma kwa namna nyingi.Unaweza kumwona n mvuvı, mkulima,mchuuzı,mzururuji n.k lakn akawa bado n mtumishi wa umma.
Teh teh the mkuu naona umebanwa kila upande unatafuta pa kutokea. Kubali wamechemsha hapa.
 

mkuu nilipoisoma hii post yako, nikamkumbuka Rev Mtikila (rip). yule bwana alikuwa sometimes ni nuisance kwenye opposition camp lakini nilipenda alivyokuwa anautumia mhimili wa mahakama in a very effective way.

I think it's time opposition waunde jopo la kudumu la wanasheria ambao jukumu lao liwe consistently kuzi-challenge all these illegal and illegitimate actions za serikali kupitia mhimili wa mahakama. some of those cases will be lost but am sure a sizeable number are likely to be won.
 
Basi ni hatari sheikh wangu manake rais anaweza kulala akaamka na kumtangaza rafiki yake kuwa jaji mtu ambaye hana utaalamu wa sheria huoni kwamba hiyo ni hatari? Tufuate miongozo jamani kuendesha nchi kwa akili zako tutakuja kujuta.haya
 
Umeishiwa hoja sasa unaanza kuhisi hisi watu hovyo. Maswala ya huyu ni fulani hayaruhusiwi hapa JF. Rudi kasome kanuni ambazo tumejiwekea hapa jukwaani.
kanuni zimezingatiwa,sijakutaja jina na pia sijakuhisi!ID yako sio fake ID,teh teh,nakuona umeanza kuwa smart,ktk maandalizi ya uDAS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…