Naomba kunukuu Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa.
Mtumishi wa umma hateuliwi, mtumishi wa umma anapatikana katika namna ya ushindani ambapo mamlaka ya serikali iwe ni utumishi au mamlaka nyingine, hutangaza nafasi na zifa za mwombaji huanishwa. Usaili hufanyika na uchambuzi wa majina hufanyika hatimaye washindi huitwa kazini na kuwa watumishi wa umma ajira ya kudumu ''Permanent and Pensionable''.........
Sasa kati ya watumishi hao wa umma bila kujali ni kada gani huteuliwa kuwa ma-DAS ambao ni makatibu tawala wa wilaya ambao kimsingi majukumu yake ni kufanya shughuli za kiutawala katika ofisi ya mkuu wa wilaya.DAS huwa chini ya ofisi ya RAS-Katibu Tawala wa Mkoa.
Hivyo basi uteuzi wa DAS ni kama ulivyo uteuzi wa DED/MD/TEC Mkurugenzi wa Halmashauri, ni lazima awe mtumishi wa umma kwanza. Hii sio nafasi ya kisiasa.
Nimeonelea nitoe ufafanuzi huu baaada ya kuona jambo la ajabu sana kutokea jioni ya leo. Hatimae siasa zinanajisi utumishi wa umma. Tunaona Mwanasiasa Mtela Mwambamba na wenzake ghafla wameteuliwa kuwa ma-DAS. Sina hakika sana na wengine lakini ni dhahiri shahiri Mtela Mwampamba sio mtumishi wa umma.
Tunajua haja yenu ya kulipa fadhila makada, tunajua mnawarundika pale Ubungo ili kuikomoa UKAWA na Saidi Kubenea lakini kwa namna mnayofanya ni wazi mnaleta aibu kubwa sana. Tafadhalini fuateni utaratibu.
Naitaka mamlaka iliyomteua Mtela na wengine ambao hawakuwa watumishi wa umma itengue mara moja au itoe ufafanuzi ni kwa mazingira gani uteuzi umezingatia taratibu za kupatikana kwa watumishi wa umma
Tafadhali sana Mods msiunge uzi huu. Kuna hoja nzito sana hapa,nawaombeni sana wakuu