Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Hii habari ya uteuzi wa ma-DAS ni ya kutunga tu kututoa kwenye reli.Hata kwenye website ya utumishi haipo!
 
Inawezekana kumetokea mabadiliko katika kada hii ambayo huko nyuma ilikuwa ni kwa civil servants (watumishi wa serikali) wenye ujuzi, uzoefu na utaalam wa utawala wa umma (public administration & finance). Equivalent wao kwa ngazi ya mkoa ni Regional Admnistration Officers (RAO). Wao ndiyo washauri wakuu wa kitaalamu katika masula ya utawala chini ya maafisa masuluri wa wilaya zao (DEDs) ambao kwa kawaida si watalaamu wa utawala. Hawa ni professionals wa utawala katika wilaya kama walivyo afisa mifugo, elimu, kilimo, afya nk wa wilaya. Zamani walijulikana kwa jina la Mabwana shauri. Wizara yao mama ni Wizara ya utumishi wa umma. Unaweza pia kuwaita maafisa utumishi wakuu wa wilaya. Si wanasiasa na hawapasi kuwa wanasiasa kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma.

Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni wanasiasa wakimuwakilisha rais katika maeneo yao. Kunapotokea mabadiliko ya rais nao hubadilishwa kwa rais mpya kuteuwa watu wake anaopenda na kuwaamini wakamuwakilishe maeneo hayo ya wilaya na mikoa.

Nadhani yote haya yalizingatiwa kwenye uteuzi huu. Kuingiza wapya kwenye utumishi wa umma na kuwateua kwenye nyazifa kama hizi ni jambo la kawaida na mifano ni mingi eg Balali kwenye Bank kuu. Ni haki ya kila mtanzania mwenye sifa na uwezo. Kuwapata watu wa namna hii unaweza kutumia search committees, siyo lazima utumike utaratibu ulioutaja wa ushindanishi. Kwani si wakurugenzi kibao wameteuliwa kwa njia za search committees na hamukulalamika?
Unajiita Dr alkili kumbe hakuna kitu kichwani.

Kuna tofauti kati ya wakurugenzi wa mashirika ya umma na watumishi wengine. Wakurugenzi wa mashirika ya umma ni watumishi wa serikali lakini utaratibu waao wa kuajiriwa ni tofauti na watumishi wengine. Wale ni uteuzi wa rais kutoka kokote awe mtumishi serikalini au nje ya serikali lakini hufanya kazi kwa mkataba maalum.

Wao huteuliwa na rais na huondolewa na rais au mkataba wao utakapoisha rais hatoi kibali cha kurejesha mkataba wao au wengine ikifika muda wao wa kisheria kustaafu hustaafu.

Lazima ujue taratibu za kuajiri watumishi wa umma wa serikali kuu, serikali za mitaa na mashirika ya umma na wakuu wa mashirika au taasisi za umma.
 
Kama mh mtukufu Rais anateua wana siasa anawaacha watu walio jitoa kuhudumia watumishi kwa miaka mingi, wameenda na kuongeza elimu. Tanzania yenye neema inakuja, ok sawa. Ngoja niendelee na mambo mengine.
 
Naomba kuuliza kama mtu akiwa yuko TISS, hawezi kupewa huo u DAS?
 
Nchi inaendeshwa kwa matakwa ya mtu Mmoja bila kujali matakwa ya Sheria. Ingawa DAS ni kacheo kadogo ambako kama mtu akipewa anakuwa hajaula, lakini sio kazi ya kisiasa ya kuweka mwanasiasa. Hapa Raisi ameshauriwa vibaya Sana. Sidhani kama kwa mtindo huu tutafika salama 2020
 
hujaelewa kipi hapo.umeuliza waliokuwa ma-DAS wameenda wapi, nimekujibu kuwa inawezekana wamestaafu, kufariki au wamerejeshwa kwenda kada zao awali.nimekuelewesha kuwa kabla mtumishi wa umma hajateuliwa kuwa DAS anakuwa mwalimu, muhasibu, afisa utumishi etc ect,
Sunzu, impossible to have all, in all districts in Tanzania being seconded from their respective departments you have mentioned. I remember well these people were well conversant with Human management issues and were mainly graduates of Mzumbe and other Administration/management higher learning institutions! Yes, some might be from those you have mentioned !
 
Mkuu Sunzu
Watu wamejitoa ufahamu haswa kwa hii Serikali ya Mwendokasi ambayo akili yao kuamzia Rais hadi mjumbe wa Serikali ya mtaa wanataka kuanza kila kitu kwa kijiti. Hawa watu wnaovaa nguo za kijani wnafikiri kwamba makada WA CCM ndio wenye akili kuliko Watanzania wote na kwa ujinga wao wakijipanga kwenye nafasi zote za uongozi they can turn around this country bila ya kumtambua Kiwango cha Maendeleo kilichofanywa kwa awamu Nne zilizopita. This is a big problem. Mambo anayofanya Magufuli yanaturidisha 50 years back na TANU. Unateua watu bila kuwa na scope of work or clear Job Description. The administrative cost is huge ukizingatia wanaopewa hizo nafasi wnapewa kama a birthday cake! Hii ni Hatari kubwa huwezi kumtoa mtu barabarani ukamkabidhi madaraka ya kuwa DAS kazi ambayo kimsingi inahutaji taaluma, na uwezo. The learning curve ya mtu Kama Makonda is a disaster. Kwa mfano Rais anasema atatoa elimu bure na kupiga marufuku michamgo kutoka kwa Wazazi lakini hapo hapo Wateule wa. Taasisi za Serikali pamoja na makampuni binafsi wanahamasishwa kuchangia madawati! Unatoza kodi ili ukalipie gharama za elimu ambazo kimsingi ni jukumu la wazazi. Hakuna nchi iliyofanya ujinga kama huo ikafanikiwa kwani sio endelevu( sustainable) Let us wait and see!
 
Wanaajiriwa kama watumishi wa umma tena kwa usaili kama maafisa tawala daraja la II then baadae miongoni mwao kuna wanaopata uteuzi kuwa MADAS mkuu Lizaboni.
Kinachonishangaza mimi ni lini hawa wamefanyiwa usaili?
 
Kwani Makatibu Tawala wa Wilaya wanateuliwa ama wanaajiriwa? Ukifanikiwa kujibu hilo nafunga mjadala
Hoja ni kuwa wanateuliwa Kutoka wapi? Wakiwa katika ajira serikalini au ni makada wa chama? Usikwepeshe hoja.
 
Mkuu ameshaanza kuonyesha rangi yake... nanuku kampeni.... mimi nitakuwa mkuu wa wote duu leo
 
Stop being too negative. Wewe unawafahamu sana wateuliwa kuliko mamlaka zao za uteuzi? Wakati mwingine tuache kufikiri kwa mazoea, tubadilike!
 
Kama "uteuzi'' huu ni wa kweli basi watumishi watakaokuwa chini ya hao wateuliwa wa jiandae kupelekwa puta ki - chama chama na siyo kwa misingi ya utumishi wa umma. Subiri utasikia kama si kuona kabisa.
 
Mmeumia sana kwa Mtela kupewa nafasi ya UDAS. Nikuulize swali mleta mada. Kwani Mkuu wa Wilaya ni Mtumishi wa Umma ama siyo?
Mkuu wa wilaya si mtumishinwa umma, nafasi yake ni ya kisiasa na si ajira. Mtumishi wa uma ni yule anayejaza mkataba wa kudumu permanent and pensionable term. Mkuu wa wilaya sio pensionable.
 
Ninadhani na wao watasoma na kuelewa japokuwa ni vichwa ngumu lakini ujumbe umefika
 
mwaka huu ndio mtaijua ccm...

na wamemleta magufuli makusudi kunyooosha wazembe na wavivu..

nini das.. hata ofisa wa kawaida akiamua anateua tu..

rais ndio mtumishi wa uma namba moja.. na ndio bosi wa watumishi wote... katiba inamruhusu kufanya chochote...

na bado huu ni mwanzo tu... endeleeni kuzungusha mikono
 
je rais sio mtumishi wa uma?? mbunge je?? nini maana ya uma?

kama sio mtumishi wa uma anawatumikia kina nani??? yeye mwenyewe anajitumikia au?

Mkuu wa wilaya si mtumishinwa umma, nafasi yake ni ya kisiasa na si ajira. Mtumishi wa uma ni yule anayejaza mkataba wa kudumu permanent and pensionable term. Mkuu wa wilaya sio pensionable.
 
Tangu amteue Amon Mpanju kuwa naibu katibu mkuu pale wizara ya sheria ambapo anachofanya pale wala hakijulikani, nimekuwa sizitilii tena maanani teuzi zake. Sioni jipya kwake tena ndo anaboronga kila analofanya!

Mtaani tunasema "bora Kikwete mara mia "
 
acheni maneno mengi wazungusha mikono nyinyi... africa hakuna taaaluma wizi tu..

hao waliokuwa wasomi miaka yote wamefanya nini la maaana??

kazi gani ngumu ya das mtu mwingine ashindwe kuifanya???

yaani kazi ya das nayo inakunyima raha eti hadi awe proffessional... si ajabu hata bank officer anafanya kazi ngumu kuliko das..

na bank ofisa hasomei u bank ni anafundishwa tu mtu yeyote hata form 6 leaver...

na mwaka huu magwanda kazi mnayo...

magufuli hasikilizagi makelele yeye vitendo tu..

mmeanza kupinga tulia ackson proffessional na msomi... leo mmebadilika mnaanza pinga ma das

Back
Top Bottom