Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

acheni maneno mengi wazungusha mikono nyinyi... africa hakuna taaaluma wizi tu..

hao waliokuwa wasomi miaka yote wamefanya nini la maaana??

kazi gani ngumu ya das mtu mwingine ashindwe kuifanya???


yaani kazi ya das nayo inakunyima raha eti hadi awe proffessional... si ajabu hata bank officer anafanya kazi ngumu kuliko das..


na bank ofisa hasomei u bank ni anafundishwa tu mtu yeyote hata form 6 leaver...

na mwaka huu magwanda kazi mnayo...

magufuli hasikilizagi makelele yeye vitendo tu..

mmeanza kupinga tulia ackson proffessional na msomi... leo mmebadilika mnaanza pinga ma das
Wewe huna uelewa wowote, na hujawahi kufanya kazi serikali. Pia hujui kanuni na sheria za kuwa mtumishi wa uma.
 
Mkuu, hawa jamaa wanaumia sana. Mtela Mwampamba alikimbia kwenye lichama lao akaja CCM pamoja na Juliana Shonza. Juli amefanikiwa kuwa mbunge wakawa wanamsema sana Mtela. Leo kateuliwa wanajifanya kuokoteza hoja dhaifu kabisa
Ungekaa kwanza janaba likaisha ndo uje hapa! Huwa nakupenda sana Dada Eliza unavojibugi kama umekatwa kichwa!
 
Mkuu, hawa jamaa wanaumia sana. Mtela Mwampamba alikimbia kwenye lichama lao akaja CCM pamoja na Juliana Shonza. Juli amefanikiwa kuwa mbunge wakawa wanamsema sana Mtela. Leo kateuliwa wanajifanya kuokoteza hoja dhaifu kabisa
Ungekaa kwanza janaba likaisha ndo uje hapa! Huwa nakupenda sana Dada Eliza unavojibugi kama umekatwa kichwa!
 
haya sasa wewe mwenye uelewa bishana na rais..

ndio ameshachagua wana ccm na hamtafanya lolote zaidi ya kulalamika tu... hii ndio ccm

Wewe huna uelewa wowote, na hujawahi kufanya kazi serikali. Pia hujui kanuni na sheria za kuwa mtumishi wa uma.
 
haya sasa wewe mwenye uelewa bishana na rais..

ndio ameshachagua wana ccm na hamtafanya lolote zaidi ya kulalamika tu... hii ndio ccm
Kulalamika ni sehemu ya kufikisha Ujumbe, ndio maana wewe umenijibu, maana yake Ujumbe umefika.
 
Jamani mlipiga sana kelele.humu akumbukwe..sasa kakumbukwa mbona mnakasirika?
 
Ikitokea Nyerere amefufuka leo na kuyaona haya yanayo endelea, anaweza akafa tena kwa shinikizo la damu.
 
kama ni hivyo basi huu ni mwendo kasi wa MH 370 malaysia airline....
Huyo DAS mteule ni Professor au DR? Naona hata TIB board Chairman ametumbuliwa wameweka Professor Kabudi.
 
Huko tuendako kunahaja ya kuwa na chombo ambacho kazi yake kitakuwa ni kulinda maslahi ya Taifa na kutoa mwelekeo wa Taifa na ambacho kitakuwa hakina uchama, udini, ukabila, u classmate/u schoolmates, n.k. Na mambo haya yenye maslahi ya Kitaifa chombo hicho kiwe na uwezo wa kuyapitia na kuyaridhia ili kuanza kutumika kwa maslahi ya Taifa. Tusiruhusu mtu mmoja, kundi moja kutuamlia mwelekeo wa Taifa letu!.
 
Unajua hata mabasi ya City boy juzi inasemekana madereva walipoadhibiwa kabla ya ajali kwa "kukiuka sheria" wapo abiria waliowatetea na kuona ule mwendo ni sawa..

Lakini athari za ajali iliyosababishwa na ukiukaji ule wa sheria hazikuchagua dereva, kondakta wala abiria kimbelembele aliyekuwa anawashabikia...

Nchi inaendeshwa kwa sheria, na pale tunaposhabikia ukiukwaji wa sheria tusidhani athari zake zitawapata "wale" na kutuacha "sisi"...

Mtu unaweza kusema uteuzi tu wa DAS una athari gani... lakini mwanzo wa ngoma ni lele....

Eid mubarak...
 
katika hili washauri wa rais wametudondosha watanzania. walipaswa kufukuzwa kazi woote.
 
je rais sio mtumishi wa uma?? mbunge je?? nini maana ya uma?

kama sio mtumishi wa uma anawatumikia kina nani??? yeye mwenyewe anajitumikia au?
Shauri mbaya....wewe nawe???acha kujihaibisha basi...
 
Kila mara huwa wanaajiriwa makatibu tawala wasaidizi, na makatibu tarafa na hawa ndio hukaimu nafasi ya Das kama yeye hayupo.

Na mtu kuwa das, ni promo kutoka kwa wasaidizi wa DAS ambao wilayani wapo.

Sasa hawa wanasiasa wataenda kufanya nini? Haya buana, nchi ni yenu fanyeni kila mnaloona linawezekana. Yule RAS wa mwanza aliyegombana na Mulongo alikuwa anajua nn anafanya
 
Tangu amteue Amon Mpanju kuwa naibu katibu mkuu pale wizara ya sheria ambapo anachofanya pale wala hakijulikani, nimekuwa sizitilii tena maanani teuzi zake. Sioni jipya kwake tena ndo anaboronga kila analofanya!

Mtaani tunasema "bora Kikwete mara mia "
Alitaka tu kubalance mambo Mkuu wangu...hilo ndo lilikuwa lengo Na si vinginevyo...
 
Wana UKAWA mnatia sana aibu, nyie ndo mlıtaka mkabidhıwe nchi kweli?Kwanı Mkurugenzi na Wakurugenzi wa idara na vitengo ndani ya Wizara, nafası zao hutangazwa na ufanyiwa usailı?Je hawa si watumishi wa umma?Je makatibu wakuu wa wizara,RAS,DAS lini ukasıkia nafasi zao zikitangazwa?Usikali kijana, hao wote nafasi zao ni za teuzi na ni watumishi wa umma.Sio kweli kwamba kuwa mtumishi lazma afanyiwe usaili.
 
Naomba kunukuu Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa.

Mtumishi wa umma hateuliwi, mtumishi wa umma anapatikana katika namna ya ushindani ambapo mamlaka ya serikali iwe ni utumishi au mamlaka nyingine, hutangaza nafasi na zifa za mwombaji huanishwa. Usaili hufanyika na uchambuzi wa majina hufanyika hatimaye washindi huitwa kazini na kuwa watumishi wa umma ajira ya kudumu ''Permanent and Pensionable''.........

Sasa kati ya watumishi hao wa umma bila kujali ni kada gani huteuliwa kuwa ma-DAS ambao ni makatibu tawala wa wilaya ambao kimsingi majukumu yake ni kufanya shughuli za kiutawala katika ofisi ya mkuu wa wilaya.DAS huwa chini ya ofisi ya RAS-Katibu Tawala wa Mkoa.
Hivyo basi uteuzi wa DAS ni kama ulivyo uteuzi wa DED/MD/TEC Mkurugenzi wa Halmashauri, ni lazima awe mtumishi wa umma kwanza. Hii sio nafasi ya kisiasa.
Nimeonelea nitoe ufafanuzi huu baaada ya kuona jambo la ajabu sana kutokea jioni ya leo. Hatimae siasa zinanajisi utumishi wa umma. Tunaona Mwanasiasa Mtela Mwambamba na wenzake ghafla wameteuliwa kuwa ma-DAS. Sina hakika sana na wengine lakini ni dhahiri shahiri Mtela Mwampamba sio mtumishi wa umma.
Tunajua haja yenu ya kulipa fadhila makada, tunajua mnawarundika pale Ubungo ili kuikomoa UKAWA na Saidi Kubenea lakini kwa namna mnayofanya ni wazi mnaleta aibu kubwa sana. Tafadhalini fuateni utaratibu.

Naitaka mamlaka iliyomteua Mtela na wengine ambao hawakuwa watumishi wa umma itengue mara moja au itoe ufafanuzi ni kwa mazingira gani uteuzi umezingatia taratibu za kupatikana kwa watumishi wa umma

Nachosisitiza hapa ni kwamba KATIBU TAWALA WA WILAYA HUTEULIWA LAKINI NI LAZIMA AWE MIONGONI MWA WATUMISHI WA UMMA
Tafadhali sana Mods msiunge uzi huu. Kuna hoja nzito sana hapa,nawaombeni sana wakuu
Hata mimi nimeshangaa sana!!!! Sijui hii nchi inapelekwa wapi !!!!!
 
Back
Top Bottom