Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,057
- 10,367
Huyu jamaa anayeitwa "Lizaboni " sikuwahi kufikiri ni "bogus" wa kiwango hiki aisee.asante sana mkuu umeweka sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu jamaa anayeitwa "Lizaboni " sikuwahi kufikiri ni "bogus" wa kiwango hiki aisee.asante sana mkuu umeweka sawa
Mazoea yalikuwa ni kwamba mtu anawekwa kwa upendeleo bila kufanya interview. Ili kuondokana na mazoea, ikaanzishwa Public Service Recruitment Secretariat ambayo iliamua kuja na mfumo wa wazi wa ajira, na malalamiko ya 'kuwekana' yakapungua sana, ikabaki ni ushindani wa waomba ajira.Nani kakudanganya? Msiishi kwa mazoea. Katika awamu hii, mtu sahihi huwekwa mahala sahihi.
DAS hachaguliwi,heteuliwa miongoni mwa watumishi wa ummaNaombeni taratibu zinazotumika kuchagua hao DAS
DAS huteuliwa miongoni kwa watumishi waandamizi wa serikali tena waliosomea masomo ya sheria , utawala na fani zinazoendana na hizo sasa hii iliyotokea naona kama ni " surprise " haya twendeni lakini
Lizaboni, Lizaboni, Lizaboni! please usilewe siasa kiasi hicho, huyu bwana kaleta hoja ya msingi kabisa. Tusiruhusu ukiukwaji huu wa sheria za utumishi wa umma kwani ni hatari kwa afya ya nchi. Hata kama unapeda chama chako kiasi gani, wanapokosea bora ukae kimya kuliko kuchangia mambo yasiyoeleweka.Mmeumia sana kwa Mtela kupewa nafasi ya UDAS. Nikuulize swali mleta mada. Kwani Mkuu wa Wilaya ni Mtumishi wa Umma ama siyo?
All in allNaomba kunukuu Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa.
Mtumishi wa umma hateuliwi, mtumishi wa umma anapatikana katika namna ya ushindani ambapo mamlaka ya serikali iwe ni utumishi au mamlaka nyingine, hutangaza nafasi na zifa za mwombaji huanishwa. Usaili hufanyika na uchambuzi wa majina hufanyika hatimaye washindi huitwa kazini na kuwa watumishi wa umma ajira ya kudumu ''Permanent and Pensionable''.........
Sasa kati ya watumishi hao wa umma bila kujali ni kada gani huteuliwa kuwa ma-DAS ambao ni makatibu tawala wa wilaya ambao kimsingi majukumu yake ni kufanya shughuli za kiutawala katika ofisi ya mkuu wa wilaya.DAS huwa chini ya ofisi ya RAS-Katibu Tawala wa Mkoa.
Hivyo basi uteuzi wa DAS ni kama ulivyo uteuzi wa DED/MD/TEC Mkurugenzi wa Halmashauri, ni lazima awe mtumishi wa umma kwanza. Hii sio nafasi ya kisiasa.
Nimeonelea nitoe ufafanuzi huu baaada ya kuona jambo la ajabu sana kutokea jioni ya leo. Hatimae siasa zinanajisi utumishi wa umma. Tunaona Mwanasiasa Mtela Mwambamba na wenzake ghafla wameteuliwa kuwa ma-DAS. Sina hakika sana na wengine lakini ni dhahiri shahiri Mtela Mwampamba sio mtumishi wa umma.
Tunajua haja yenu ya kulipa fadhila makada, tunajua mnawarundika pale Ubungo ili kuikomoa UKAWA na Saidi Kubenea lakini kwa namna mnayofanya ni wazi mnaleta aibu kubwa sana. Tafadhalini fuateni utaratibu.
Naitaka mamlaka iliyomteua Mtela na wengine ambao hawakuwa watumishi wa umma itengue mara moja au itoe ufafanuzi ni kwa mazingira gani uteuzi umezingatia taratibu za kupatikana kwa watumishi wa umma
Nachosisitiza hapa ni kwamba KATIBU TAWALA WA WILAYA HUTEULIWA LAKINI NI LAZIMA AWE MIONGONI MWA WATUMISHI WA UMMA
Tafadhali sana Mods msiunge uzi huu. Kuna hoja nzito sana hapa,nawaombeni sana wakuu
Na lakini wenye mamlaka ya kushauri wajue kabisa watakuja kulumiwa VIBAYA..pia wale wenye ndoto za KUUKWAA hapo baadae kama hawajui watakuja kulaumiwa kwa kushindwa kushauri ipasavyo!Kwa sasa Raia Namba Moja wa Tanzania anafanya chochote atakachokukifanya kukifanya. Iwe kwa majibu wa Katiba au kinyume, anajifanyia tu.
Hakuna kuhoji.Ukihoji utahojiwa.Utazingirwa.
Kama Mkurugenzi anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya nafasi maalumu kwa makada wa CCM, istarajiwe tofauti kwauteuzi hata wa hao ma-DAS?
Katiba ya nchi kwa sasa ni ilani ya CCM....
Das ni mtumishi mostly ni afisa utawala au utumishi habari, tarafa, ambaye amefanya kaz kwa muda mrefu ndiyo anapelekwa kwenda kuendesha ofis ya mkuu wa wilaya na kuwa katibu wa kamat ya ulinz na usalama ya wilaya.Naombeni taratibu zinazotumika kuchagua hao DAS
angalizo muhimuAll in all
Huu uteuz wa madas barua haina logo ya serikal na imeandikwa bila kuzingatia maadili ya uandishi wa kaz za serikali no sahihi huu utakua mchezo wa vijana wa mjini.
Pia haiwezekani kuacha watendaji wote wenye uzoefu naona waliobaki hawazid kumi.
Na lakini wenye mamlaka ya kushauri wajue kabisa watakuja kulumiwa VIBAYA..pia wale wenye ndoto za KUUKWAA hapo baadae kama hawajui watakuja kulaumiwa kwa kushindwa kushauri ipasavyo!
najua nakufundisha vitu hapa ukawaeleze na wenzio. Katibu Tawala wa Wilaya anateuliwa lakini miongoni mwa watumishi wa umma
after five minutesAkirudi tena nitajua ni mwehu .
Mleta mada tuwekee sawa. Nijuavyo mimi ni kwamba Afisa Tawala wa Wilaya ni Dstrict Administrative Officer. Si nafasi ya uteuzi bali ni ya uajiriwa kulingana na mahitaji ya wilaya. Nafasi hizo hutangazwa na Mkoa kwa kufuata taratibu za ajira Serikalini. Si nafasi ya kisiasa hata kidogo na kama Mtela Mwampamba kapatikana kwa style hiyo basi hilo litakuwa doa kubwa kwa serikali yangu ya CCM.
P.K kutoka RwandaSijui kama JPM hata anaelewa nini anafanya! Ana washauri kweli huyu??