Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Halafu mtu anaomba tumuombee, haombi tumshauri.
 
nyumbu wanajua kukosoa tu..

ukiwauliza utaratibu wa kumpitisha lowassa kuwa mgombea wao wanakuwa wakali hao..

au utaratibu wa mbowe kuwa mwenyekiti milele wanakasirika

Ndio tayari ni maDAS , hivi wakati mnamchagua Lowasa kuwa mgombea alitimiza vigezo vya kuwa Mgombea vilivyopo kwenye katiba yenu?, au kulikuwa na vimamruki vyenu nini mliviweka stand by?, acheni watu wafanye kazi
 
ila bado asingeteuliwa au kupewa hiyo nafasi, MNGEKUJA HAPA NA KUMSHUSHUA MWAMPAMBA KUWA KAKOSA HATA U-DAS

mnakula maneno yenu, hawa jamaa mnawapa promo nyie wenyewe

hayo uliyoandika hapa, yanaishia humu, hakuna mtu yeyote wa kubadili hilo

pole
 
najua nakufundisha vitu hapa ukawaeleze na wenzio. Katibu Tawala wa Wilaya anateuliwa lakini miongoni mwa watumishi wa umma
Mkuu Okw, kwa namna ulivyowaumbua si ajabu wakaibuka wakadai mteuliwa huyo alikuwa mtumishi wa umma idara ya usalama wa taifa!
 


Baadhi yetu tumekuelewa sana...pongezi kwa ufafanuzi uliotoa hapa...Hapa mimi nimeshangazwa mno...lakini mimi naishia kushangaa tu...kilichotokea ni HATARI...Nadhani wamedhamiria kumhujumu Rais...Ni kitu cha ajabu kimefanyika...
 
Nani kakudanganya? Msiishi kwa mazoea. Katika awamu hii, mtu sahihi huwekwa mahala sahihi.
Toa pumba zako hapa! Watu wanajadili jambo nyeti kwa mustakabali wa nchi wewe unaleta upuuzi hapa? Namna hiyo ndio nchi inavyoongozwa au kwa sababu unasaka buku mbili?
 
Sijui kama JPM hata anaelewa nini anafanya! Ana washauri kweli huyu??
jpm kajizungusha wanafiki wasioweza kumshauri zaidi ya kumwabudu, japo naye haashauriki kama walivo viongozi wa aina yake
 


Hoja yako kweli ni nzito....ipo haja ya kupitia upya UTEUZI wa ma-DAS...lipo tatizo kubwa...Uteuzi huu ni hujuma kwa JPM...
 
asante mkuu nimeweka sifa za majukumu yao kwa kina hapo juu
 
Huwezi kumuelewa huyu kwa vile hajui hata alichoandika. Hasira zote ni kwa vile Mtela Mwampamba kapewa UDAS
Mkuu Lizaboni wakati mwingine hizi siasa za "UKAWA NA CCM" tuziweke kando kidogo hata kwa saa moja...Kwanini tusijifunze hata kwa wenzetu kule wanakopigana siku kama ya leo ya Idd watu wanaweka silaha chini na kula "Pilau na harua" then ndio wanarudi "vitani"....Tuwe na break kwenye mambo ya pamoja mkuu wangu


Mkuu labda uwe hujafanya kazi kwenye utumishi wa Umma,lakini DAS na RAS ni watu muhimu sana kwenye utumishi wa umma sanaa tuu!!Hiki cheo hakiitaji siasa!Tutashangaa kesi zinajaa Mhakama ya Kazi au CMA(Commision for Mediation and Arbitration)

Cheo hiki si cha mwanaisiasa bali cha mtumishi ambaye ni Parmanent and Pensionable...anatakiwa mtu aliyekulia ndani ya utumishi wa umma hata kwa miaka kumi,mwenye uelewa wa "Organizational Culture" ya ofisi za umma hasa kwa upande wa utumishi,ni cheo kinachotokana na mtu aliye ndani ya utumishi anayepandishwa akiwa ndani ya utumishi wa umma

Hawa vijana wengi walioteuliwa hawajawahi kuajiliwa na serikali,hawa wote walikuwa Lumumba na CCM Makao Makuu Dodoma.Hawajafanyiwa usaili wa aina yoyote kuingia katika nafasi hizo,ndio maana unaona hata Utumishi hawana CV zao ndio maana wameambiwa waende nazo.Wanaenda kuongoza watu waliodumu kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu na weledi wa kutosha katika kanuni,taratibu na sheria za utumishi

Kifupi ni kuwa DAS au RAS ni sawa na Katibu Mkuu katika Wizara,na sio Waziri...Waziri anaweza kuja leo na kesho akashindwa uchaguzi akakosa hiyo nafasi,lkn Katibu Mkuu yupo pale pale,yeye ndio mwenye kujua haswaa Wizara na mahitaji yake,hatokani na siasa au vyama bali mfumo ndani ya utumishi wa umma.Sasa DAS ni kama Katibu Msaidizi na DC kama Naibu Waziri,Wakati RAS ni kama Katibu Mkuu na RC kama Waziri.DC na RC wanaweza hamishwa hamishwa sbb za kisiasa lakini si RAS na DAS

Hawa vijana wanaenda kukutana na watu wengine ndani ya ofisi ya DAS wenye uweledi kuwazidi,hawa wamedumu utumishi na wameingia kwa usaili na si kubebwa.Angeteuwa basi wale walio na weledi,uzoefu na ufahamu wa hii kazi na si hii "shukrani ya kisiasa"

Kwa hili sipo na JPM...hii ni upotofu,hii si sawa!!Fanyia siasa koooooote lakini si kwenye "Muundo wa Utumishi" wa umma unaoongozwa na Sheria,Kanuni na Taratibu!!Sasa nini Maana ya kuwa na "Government Standing Order?"
 
ila bado asingeteuliwa au kupewa hiyo nafasi, MNGEKUJA HAPA NA KUMSHUSHUA MWAMPAMBA KUWA KAKOSA HATA U-DAS

mnakula maneno yenu, hawa jamaa mnawapa promo nyie wenyewe

hayo uliyoandika hapa, yanaishia humu, hakuna mtu yeyote wa kubadili hilo

pole
Haaaaah haaaaa ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukikimbia ndio kabisaaaaa
 
Kwani Makatibu Tawala wa Wilaya wanateuliwa ama wanaajiriwa? Ukifanikiwa kujibu hilo nafunga mjadala
wanateuliwa kutoka watumishi wa umma au nafasi inatangazwa na usaili ufanyika...
 
Uongozi uchwara
 
We kijana tulia sasa ulitaka makada wa ccm waliopigania chama kuingia madarakani watoswe? Na bado ofisi zote za serikali mpaka hapo kwenye ofisi yako ya CAG Ma Auditors watakuwa makada wa CCM... We endelea kuzungurusha tu mikono
We are patiently waiting for viwandas !
 

kweli itafika mahali tutachagua moja kati ya haya...either tuhame nchi au tupambane kuwaondoa hawa makaburu weusi......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…