PreGE2025 Kwa mujibu wa taarifa alizopewa Maria Sarungi, ni kwamba watekaji wanamuwinda Askofu Gwajima

PreGE2025 Kwa mujibu wa taarifa alizopewa Maria Sarungi, ni kwamba watekaji wanamuwinda Askofu Gwajima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni kweli ila siyo sana kama yako unayemwabudia huyo tapeli gwajima. Kwani muda wote alikuwa wapi na mbona wakati wa Magu aliyemuumba kisiasa aliufyata? Msiandike kama hamna kumbukumbu wala bongo jamanini.
Hii ilikuwa 2015 akiwapa machawa wa CCM vidonge vyao,wakati wa Jiwe pia alikemea utekaji wa Roma Mkatoliki wakati huo wewe uko Ikungulyabashashi Simiyu ndanindani huko
 

Attachments

  • Mgonja97_1929202059678462337(144P).mp4
    645 KB
Gwajima atakuwa ni mpumbavu sana wakati huu akikaa kizembe.

Kuna kila sababu ya kumpata Gwajima ili uwe mfano mzuri katika wakati huu wa saa mbaya kabisa kwao.

Wakimpata Gwajima, watakuwa na nguvu ya kuwatisha wengine wote wanao elekea kuiga mfano wake.

Na kwa uhakika watatikisa sana hali iliyopo sasa kuelekea Oktoba.
 
Kwanini wasijibu HOJA za Gwajima?!
Mtumishi wa Mungu Josephat Gwajima ni Mpakwa Mafuta wa Bwana. Hagusiki. Amgusaye, kwa lengo la kumdhuru ajue anagusa mboni ya jicho la Mungu. ZEK 2:8.
“Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.
”
— Zekaria 2:8 (Biblia Takatifu)

Shetani alishashindwa zamani sana.

maombi ya kufunga na kuomba ya siku saba yaendelee.
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Maria Sarungi kupitia mtanda wa X siku ya leo ambapo Maria pia ame- post taarifa kutoka chanzo chake anachodai huwa kinampa taarifa za uhakika.

Wadau, habari ndio hiyo kwa ufupi. Kwahiyo wacheni tusubiri muda utaongea. .

Kwa Jina la Yesu hawataweza kumteka,Bali watatekwa wao na kutupwa kuzimu. Amen
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maelezo ya Maria Sarungi kupitia mtanda wa X siku ya leo ambapo Maria pia ame- post taarifa kutoka chanzo chake anachodai huwa kinampa taarifa za uhakika.

Wadau, habari ndio hiyo kwa ufupi. Kwahiyo wacheni tusubiri muda utaongea. .

Kama walifanikiwa kwa Kitima,Gwajima ni cha mtoto

CCM haijawahi kushindwa
 
1: Mm ni mmojawapo wa wale ambao sijauamini huu mchongo wa Gwajima.

2: Inshu yake imekuja kwa kuchelewa sana.

3: Kwanini wakati huu? Miezi kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu. Ni kweli tumesahau propaganda za hawa jamaa?

4: Ziko agenda muhimu sana zilizokuwa zinaendelea kabla ya hili jambo, lakini cha ajabu, tumeacha kuimba wimbo wetu na sasa tunampambania Gwajima🤔

5: Hivi tukiwaacha waparurane wao kwa wao mpaka watakapoishia, sisi tutapungukiwa nini?

6: Sikuona sana wanashadadia majibizano ya G55 na Chadema, bali waligusia kwa mbali huku wakiendelea na agenda zao.

7: Hawa ni mabingwa wa kuandaa mambo, tena kupitia watu tusiotarajia ila tunaowaamini. Tukizolewa na upepo mpaka tuje turejee huwa wameshapitisha mambo yao au wameshatuchelewesha kwa baadhi ya mambo yetu muhimu cause tuliacha yetu tukafata yao😀

8: Kwani, Gwajima kama Askofu, kwanini anatishia kusema ukweli kwa kuwataja watekaji na badala yake anarefusha mambo? Nimemtaja kama Askofu kwa cheo chake ambacho kinamtaka Daima kusema kweli, maana kuusema ukweli ndani ya chama sio rahisi. (Yohane aliusema ukweli mbele ya Herode na ukweli huo ukamgharimu maisha yake) Askofu wetu Gwajima hawezi kuifia kweli anayoihubiri kanisani?

9: Watekaji amewajua hivi karibuni? Alikuwa wapi kukemea utekaji tangu habari za utekaji zilipoanza kusikika na kushamili kwa kasi?

10: Ameona hakuna uwezekano wa kurudi Bungeni hivyo kaona atishie nyau ili wamrudishe kwenye mchakato? Yeye anajijua hakuwa wao, nao wanamjua hakuwa mtu wao (hata juzi wamemtaja kutomtambua). Nawasihi hata Chauma wasimpokee.
 
Back
Top Bottom