Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Unaweza ukarudia kusoma ulichoandika hapo? Umeandika kwa sababu ya kuandika au unadata zake? Hata bila kuzunguka vijijini unaweza ukajiuliza kama kweli hao wananchi wa kijijini unaowazungumzia,tena bila ridhaa yao, kama kweli wanamaisha ya " kujitosheleza(pa kulala, chakula na nguo) " kwa nini kila siku wanakimbilia mijini hasa dsm wakati wamejitosheleza?
Anyway sina imani katika demokrasia hasa hii ya kiafrika, warudi CCM au waje CHADEMA hakuna jipya watakaloleta hawa wanasiasa, Tanzania yetu hii ni kama jamii ya kwenye allegory of the cave ya Plato, watu wasiojua kusoma na kuandika (wajinga), nchi inayozalisha sifuri nyingi kwenye mitihani, wananchi wanaoshinda kusoma udaku na ushabiki wa vyama vya siasa wana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kweli?
"Kwenye kijani hapo - kwanza tukubaliane kwamba wananchiwa vijijini kwa ujumla wao wanajitosheleza katika mahitaji ya msingi i.e. vijijini, mfumo wao upo dominated na subsistence economy; Tukija kwenye suala la pili sasa kuhusu kwanini wengi wanakimbilia mijini, huo ni mjadala mwingine kwani hao sasa wanageuka kuwa wapiga kura wa mijini, hivyo hatuna haja tena ya kuwajadili in the equation per asha dii's argument kuhusu mwenendo wa wapiga kura vijijini ambapo hadi sasa as we speak, not less than 70% ya watanzania bado wanaishi huko;
Habari ya kusema tukubaliane kwamba wananchi wa vijijini kwa ujumla wao wanajitosheleza kwa sababu ya subsistence economy naitilia shaka, ni theory iliyopitwa na wakati, tembelea huko vijijini uone kama hii subsistence economy inaexist.
Quote;
"Naunga mkono hoja, lakini muhimu zaidi ni kwamba kwa bahati mbaya haya hayawezi kubadilika ndani ya miaka mitatu, hence uzito wa hoja ya asha dii katika bandiko namba moja kule juu; je, kwa mtazamo wako, hali hii tunaweza kuibadilisha ili watanzania wafanye maamuzi ya maana ya kujileletea mabadiliko ya kweli, suala ambalo EMT hapo juu (tazama bandiko namba 14) amepinga kwamba haliwezi kutokea 2015? Binafsi naunga mkono hoja ya EMT, na naomba nieleweke kwamba haina maana kwamba naishabikia, bali naiunga mkono kwamba kwa mtazamo wangu, ipo sahihi;
Elimu ndio suluhisho la hili, uneducated angry mob wanaweza wakafanya mapinduzi makubwa tu,lakini wakipata madaraka huu utawala unaopigiwa kelele utakua na afadhali!
EMT tupe uzoefu wako unavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yako sijui ni sheria sijui ni uandishi wa habari,
Nguruvi tupe harakati zako halisi kutokea huko ulipo,
Mchambuzi tueleze uzoefu wako na harakati zako za sasa, kama kuna watu unawajenga wanafanikiwa wapi wanashindwa wapi....
Naungana na AshaDii, kuwa CCM inaweza kushinda tena uchaguzi kwa sabubu zifuatazo-
- Nguvu nyingi sana za makusudi za kutumia vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha CCM inashinda na inaendelea kukaa madarakani.
- Kutumia au kufuja fedha nyingi sana kuwapita wapinzani, rushwa, kununua vitambulisho vya kupigia, kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura vya watu ambao hawa'exist n.k
- Vyombo vya usalama kuingizwa katika siasa ya kuhakikisha ccm inashinda kwa mbinu yeyote....badala ya vyombo hivyo kulinda wanachi, kulinda mali zao....hivyo kutoa picha kuwa, hali ya umasikini iliopo, hali ya migogoro ya kidini inayo endelea, hali ya kuporwa rasilimali zetu, vyombo hivi vya ulinzi na usalama vinanufaika.
- Kuwatishia wapiga kura kutojitokeza kwa wingi ya kuwa; siku ya uchaguzi kunategemewa kuwa na vurugu, hivyo kuweka askari wengi wenye uniform na silaa za kivita.
- Vifaa vya kupigia kura kuchelewa kufika katika maeneo husika, kwa makusudi, hasa zile sehemu zenye ngome kubwa ya upinzani.
- Kuwakatisha tamaa wapiga kura kwa kuwaambia kumbukumbu za daftari ya mpiga kura jina lake halipo, au zinaonyesha ameshakufa.
- Tume ya uchaguzi kutokuwa huru, na inatia mashaka kuiamini inapotoa matokeo ya mshindi kama ni ya kweli au laa...tumeona zanbar, cuf walishinda...tume ilitangazaje...hadi leo kuna serikali ya uwk?! Kuna kipindi Zanzbr ilibidi nyerere aende ili yatangazwe tofauti na uhalisia.
Watawala wana kila kitu cha kuwafanya waendelee kutawala kupitia CCM, fedha zipo mikononi mwao, ulinzi na usalama upo mikononi mwao, tume za uchaguzi ni zao, bunge ni lao na wanam'remote tu spika na naibu wake watakavyo, vyombo vya habari wamevishika na vinavyoleta ubishi wanavifungia, mahakama zipo chini yao...nini kimebaki?
My take ni kuwa, until that day watawaliwa tutakapo amua (inaf is inaf) kwa kuandamana nchi nzima dhidi ya dhuluma za viongozi wetu wanaodhani nchi ni mali yao ya mfukoni. Lini sasa wananchi tutaamua kukiambia chama tawala kuwa inatosha, mimi nadhini itakuwa 2015 kama tume itaamua kutoa matokeo tofauti na maamuzi ya wananchi wote.
Nakubaliana nawe kabisa na kwa kuongezea tu ni pamoja na mikakati ya pamoja yenye lengo moja itakayofanywa kwa pamoja.AshaDii;5734117]Maandalizi na mikakati ya kushika Uongozi wa juu wa Serikali huwa ni mzito na wakimahesabu na kwa maandalizi thabiti yaliyo jipanga vyema. Maandalizi hayo hayafanywi kwa siku moja, hayafanywi in Isolation na wala hayawezi fanikiwa kwa kubahatisha. Inahitaji nguvu ya Chama, nguvu ya uongozi wa Chama na kubwa zaidi nguvu ya wanachama ambao ndiyo Umma na ndiyo wana wajibu wa kumweka mtu katika kiti hicho kwa njia ya kura wakati wa Uchaguzi.
AshaDii tatizo si kujiandikisha. Hebu tufikirie kuwa kama wamejiandikisha watu 100 wakapiga kura watu 30, tunasababu ya kuhamasisha wajiandikishe watu 500! Kinachotakiwa ni kufahamu kwanini hawa 70 hawakupiga kura. Kwa bahati mbaya serikali na CCM wanajua lakini wapinzani hawaonekani kuliona hili kama tatizo. Kunakitu kinaitwa voters suppression. Kule Marekani wakati Obama anaandikisha watu wanaoishi kwa hofu(walatino) Republican wakazuka na mkakati wa kusema Obama anataka kujua akina nani na wapo wapi ili baada ya uchaguzi warudishwe makwao. Hiyo ndiyo voters suppression kwamba waogope kupiga kura.KUNDI LA WAPIGA KURA
Historia Kujirudia (hasa ya 2005)
Kuna kila dalili kwamba historia ya 2005 inaweza kujirudia i.e. watanzania wengi watakuwa wamejiandikisha kupiga kura ila wachache watakaopiga kura. Hata hivyo izingatiwe kuwa hili linaweza epushwa ama kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kama: Kwanza iwapo Vyama pinzani, Vyombo Vya habari na Wanaharakai wa Demokrasia wataweza kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwa nguvu zaidi, na Pili ni kwa CHADEMA kuja na candidate mzuri, mashuhuri, mwenye experience ya kutosha ambaye ataweza himili na kushindana vyema na mgombea urais wa chama pinzani
Ni kwasababu vyama vya upinzani havijawa na mkakati wa kuwa na daftari la wapiga kura wao ili kuwafuatilia siku ya kupiga kura.Kutokujifunga kwa wapiga kura
Watanzania wengi ambao ni wapiga kura na wanao kuwa na vitambulisho vya kupiga kura kwa nia hiyo ya kujiandikisha hawapo katika chama chochote
Kama hakuna statistic na strategist uwezekano wa kufahamu wapi pa kwenda ni mdogo. Nitolee tena mfano wa Marekani. Obama alifahamu kuwa ili Romney ashinde ni lazima ashinde majimbo ya Ohio na Florida. Hata kama Obama angeyapoteza bado uwezekano wa kushinda ulikuwepo japo kwa ufinyu sana. Alichokifanya ni kwenda Ohio na Florida na kupiga kambi huko na Romney hakuondoka Ohio na Florida. Wakati hayo yakitokea Obama alikuwa na political capital maeneo mengine. As a result alimbana Romney asitoke Ohio na Florida na kumpiga huko huko ingawa alishashinda tena kabla ya Ohio na Florida kutangaza. Huu ndio mkakati wa kisiasa. Unasoma weakness za opponent unazigeuza kuwa mtaji.Tunaona CHADEMA nguvu ya kuongeza wapiga kura ipo katika kubanana na hao ambao tayari ni wanachama wa CCM na wale wasio na chama ambao wanawapata pia. Tokana na furaha ipatikanapo pale wanapo faulu kuwavuta wana CCM wengi kuja Chadema inapelekea kuonekana kana kwamba Strategy yao ipo katika kuhakikisha wanachama wa CCM wanahamia CHADEMA badala ya nguvu katika kuhakikisha wanajenga ‘loyalties' kwa kuwavuta wale wasio na chama
Kuna ushahidi mzuri tu wa kuonyesha kuwa Tanzania vijijini ya leo si ya jana. Haiwezekani mikoani wakaongoza kutoa wabunge wengi kuliko Dar es salaam. Hii maana yake ni kuwa kule vijijini sasa wanajitambua tena bila woga. Kilolo wanajenga ofisi ya CDM ambapo Ilala na Kindondoni hawawezi. Hali ipo hivyo kule Tarime na kwingineko. Wapinzani hawapaswi kudhani kuwa huko vijijini hakuna kura, ni kosa. Ni kosa hilo ndilo liliwafanya wasi kampeni Lindi na Mtwara leo tunaona kuwa kumbe huko ndiko kungekuwa salama kwao. Kama huna ujumbe mzuri hakuna atakayekuelewa awe mjini au kijijiniWoga wa MabadilikoKura nyingi zipo vijijini, na wengi wao ni CCM ingawa inaenda inapungua na ni kwa sababu sio tu kwa sababu hawana upeo au elimu ya uraia bali by default, watu maeneo ya vijijini huwa ni ‘conservatives'. Hawapendi mabadiliko na ni waoga wa mabadiliko, wapo katika hali mbaya lakini bado wana amini kuwa uongozi mwingine unaweza waangamiza zaidi na kabisa
Je, kulikuwa na ujumbe mahususi kwa wananchi? Kwa mwanasiasa makini siku zote huongea kutokana na mazingira. Leo mtu wa Mtwara ukimwambia kuhusu orodha ya mafisadi hatakuelewa kwasababu hiyo si shida yake. Shida yake ni chumvi, sukari na mafuta ya taa.Kama utaweza ku-connect with audience kwa kutumia ufisadi hilo ni jema lakini linahitaji charismatic and orator mzuri. Hivyo hoja hakiuwa orodha, hoja ni je walipokwenda Kigoma waliongelea reli, walipokuwa Songea waliongelea mbolea na walipokuwa sumbawanga waliongelea soko la mahindi?KUNDI LA CHAMA CHA MAPINDUZI Kwanza tujiulize ni kwa namna ipi CCM wame survive hadi hapo walipo?! Tuache yote hayo na tuanzie pale ambapo tulipata orodha ya "List of Shame" toka kwa Dr. Slaa, Orodha iliyotikisa na kusababisha viongozi hao wa juu kumaka kumfungulia kesi Dr. Slaa - suala ambalo halijafanikiwa hadi leo. Ile Orodha ilikuwa ni tosha kabisa kuwa hamasa kwa wananchi na wanaharakati kuing'oa CCM kwenye uchaguzi wa 2010. Lakini haikuwa hivyo...
Hapa niseme kuwa wapinzani wanashindwa kutumia udhaifu wa serikali iliyopo madarakani na CCM kwa ujumla. Matahalani, wiki mbili zilizopita CDM walikuwa na mkutano kwa kile walichosema ni mahakama ya wananchi. Nilitaraji kuwa hoja ya James Mbatia kuhusu ufisadi wa hela za rada kuhusu elimu ingeelezwa vizuri sana. Kwa maneno mengine walitakiwa wailazimishe serikali ijiseme yenyewe mbele ya umma. Kwa vipi? Hapa wangembana mgombea mtarajiwa Bernad Membe ambaye si tu alishindwa kutaja waliohusika bali pia alipigia sana upatu pesa hizo. Kungetokea confusion kali kati ya Membe na serikali yake na hapo kesi ingekuwa wazi.Na pia inafanya Serikali kutoa maamuzi ambayo kimsingi na kimantiki hayaeleweki; kama vile kuvunjwa kwa POAC. Ukichukulia uzito na umuhimu wa Kamati yenyewe ikiwa ilikuwa inaangalia na kufuatilia asset zenye thamani ya trillion za shilingi, inafanya kuamini kuwa ni mtu asiye na akili tu ndiyo anaweza futa ama kukubali ifutwe LA SIVYO zinatakiwa sababu za Msing sana kuwakilishwa.
Hapa nadhani CCM wapo defensive na CDM offensive. Tatizo ni uzoefu, kwamba katika wakati mgumu CCM wanajua wajikwamue vipi. Bahati mbaya CDM wameshindwa kusoma mazingira. Lakini nakuhakikishia kuwa kwa kiasi fulani CCM wanajihani.Wamejipanga VyemaKujipanga haijialishi ni njia ipi unatumia, kama ni chafu/safi, halali/si haliali, haki/siyo haki - inachojalisha ni mipango yako kuweza kufanikisha azma ya malengo ya mipango hiyo. Serikali ya CCM imekuwa hodari katika kuhakikisha inatengeneza mazingira wezeshi kwa wao kuweza kushinda uchaguzi mkuu ujao. Wamejitosheleza vyema katika Nyanja mbali mbali, tokana na vita baridi waliyo nayo dhidi ya wapinzani wao wakuu CHADEMA. Wamejikita katika kujizatiti kuwanyong'onyeza nguvu CHADEMA kwa kila namna inayowezekana hasa kwa kutumia madhaifu yao.
Viongozi wao wamekuwa wakijitahidi na kuweza kufanya kazi hiyo ya kwa bidii, Tumeona namna shutuma za CHADEMA kuingia mikataba na Wafadhili wa mabillioni ya shilingi (Sijui hii kesi iliishia wapi?); Tumeona suala la Kadi ya CCM ya Dr. Slaa vile ilisambaa katika vyombo vya habari ambayo mwanzo ilichukuliwa kwa wepesi na hatimaye kuweza ku ‘divert' attention ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwa kulitatua tatizo badala ya kuangalia mambo mengine ya msingi na yalo na tija kwa shughuli za Chama
Narudi kule kule kuwa hawakutumia mahakama ya wananchi kikamilifu. Pengine ilionekana kama tatizo la mtu na si chama na hivyo kutopewa umuhimu wa kutosha. Hili tu wangejipanga vema na kuueleza umma kwa kina wananchi wangewaelewa nasikitika kusema hawakuweza kufanya hivyo.Wapo juu ya Taasisi; Kumekuwa na sarakasi nyingi Bungeni hadi kupelekea lawama zilizo kithiri dhidi ya Madame Anne Makinda na ndugu Job Ndugai – tokana na matendo yasiyowaridhisha wabunge wengi na wananchi kwa ujumla. Kubwa kuliko hapa karibuni kumefutwa na kuvunjwa kwa Kamati mbili (1) Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje iliyokua inaongozwa na Edward Lowassa na (2) Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa inaongozwa na Zitto Zuberi Kabwe ambayo ilifutwa kabisa. Inaleta uwalakini sana ‘timing' ya events hizi hasa tokana na kuwa ripoti za kamati hizo zilikuwa zikae wiki chache baada ya tukio. Ikumbukwe ripoti ya mwisho ya Zitto ilipeleka kura ya kutokuwa na Imani kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na hivo kusababisha kusimamishwa kwa mawaziri 8.
Kupokea kwa Oil Chafu toka CCM
Ni ajabu sana kuwa CHADEMA wapo haraka sana katika kupokea viongozi toka chama kingine (hasa cha wapinzani wao wakuu CCM) kwa mbwembwe na matangazo. Utata unakuja pale ambapo huyo aliyejitoa CCM ni Kiongozi na akifika CDM anapewa uongozi… Hiyo ni hatarishi kama huyo mtu ni pandikizi, pia kwa namna moja ama nyingine kuwanyima haki wale ambao wanaweza hiyo nafasi nje ya huyo mgeni. ; Hili litatokea na ni moja ya mambo ambayo yataigharimu CHADEMA urais 2015; CHADEMA wanaweza kuepuka kuwa chama chakupokea wale wote ambao wanaogopa kusimama kama wagombea wa CCM e 2015 kutokana na nguvu ya CHADEMA
Bahati mbaya siyo kutokana na Mapenzi juu ya CHADEMA na taifa, bali kwa nafsi na ubinafsi wao. Ni muhimu CHADEMA wakaliangalia upya hili; pengine CHADEMA waje na tamko kwamba mtu yeyote ambaye atahama kutoka CCM dadika ya mwisho hatopata nafasi ya kugombea kwani ni kuwanyima haki loyalists. Chama kije na kanuni kwamba ni lazima ujiunge na CHADEMA miaka miwili kwa mfano before uchaguzi ili uweze kupata experience na chama etc
Habari wana Jf,
.....
My General Take
Hadi hapa naamini kuwa Kuna kila dalili kuwa CCM itashinda, hata kama itakuwa kwa asilimia 51% za kura zote; Tofauti itakayokuwepo katika ushindi huo ni kuwa CCM itashinda kwa margine ndogo kuko zote katika historia za Chaguzi Tanzania. Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshima Freeman Mbowe yeye kishajiapia kuwa ikishinda CCM 2015 atajiuzuru na naomba nimnukuu "Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa". Ni kauli ya kutia moyo ya kuwa Chama kimejipanga vipi, kuwa kina uhakika wa Kazi na nguvu zake na kuwa Chama kitaikomboa nchi ifikipo 2015.
Vile vile iwapo kutakuwa na ushindi wa CHADEMA kama vile wengi wa Watanzania, Wanaharakati na Viongozi wa Chama hicho wanavyo dhania na kuamini; basi ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hasa iwapo CHADEMA watapata kura nyingi ngazi ya Urais na wabunge wengi – ila nikiri kuwa tatizo ni kwamba suala la ndoa za vyama, CHADEMA walishajifunga na umma unajua fika na kwa kiasi kikubwa namna gani CHADEMA hawakubaliani a wazo la ‘Government of National Unity' kule ZNZ. Swali linabaki je ikitokea uwezekano wa GNU Tanzania bara na ikaonekana ndiyo suluhu pekee, CHADEMA watakula matapishi yao wenyewe? Hata hivyo naomba hili niliache hapa kwani ni mjadala mwingine mpya kabisa. Wanachadema... Hii nakala ni katika ku challengiana na kujitazama upya kuweza kufanikisha safari ya Ikulu.
Naomba nitumie hii nukuu ya vita from the Legendary Sun Wu. Naamini kuwa hii nukuu, inatumika vema na CCM katika tactics zake zake chafu za kisiasa hasa hizi za ‘Gutter Politics' ambazo ndio sababu pekee bado wapo hapo walipo. It is time Chadema start doing the same... (IMO)."If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected."
Pamoja Saana,
AshaDii.
Maadam bado wananchi bado wanaendelea kutafuta WATAWALA wa kuwaita WAHESHIMIWA basi itakuwa vigumu sana kuiondoa CCM madarakani. Yatizo sio Chadema, CUF wala NCCR bali watu wote nyuma ya vyama hivi na wananchi wenyewe tuna mtindio wa Ubongo unaoitwa kasumba ya mkoloni..
Mambo yoote yalokwisha tokea bado wananchi tumegawanyika na wengine wakiipigia debe CCM japo wanaumia ktk maisha. Ukiona nchi maskini ambayo inajengwa kutoka juu kwa kutumia mifumo inayokuza asilimia 1 kumiliki asilimia 90 ya Utajiri ilihali nchi hiyo watu wake ni maskini basi ujue hawa watu wana kasumba mbaya sana. je una sababu baina ya CUF na Chadema kuchukiana tena kisiasa vyama ambavyo havina hata nusu ya wabunge nchini? kuna sababu leo hii wananchi waislaam na wakristu kuchukiana hadi kufikia hatua tuliyopo?... na tujiulize mkoloni aliweza vipi kututawala?.. Sii kwa kupitia mambo kama haya?
Hivyo hadi siku wananchi wenyewe watakapo amka toka usingizi wa pono na kudai VIONGOZI badala ya WATAWALA na wakaijua tofauti baina na vitu hivyo ndipo tunapoweza kuona Upinzani wa kweli sio tu kwa vyama vya siasa bali hata wananchi wenyewe kujua tofauti baina ya UKWELI na MAMLAKA.
Binafsi yangu nimesha ondoa tumaini hasa baada ya kuona wananchi wenyewe tena hapa hapa JF wakikwaruzana kwa vitu walivyolengeshwa hata wasione ujinga ulotangulia nyuma yake.. Kwa mfano leo hii watu wanabishana na kuchukiana juu ya dini, na sii bure CCM wameondoa kabisa kasi ya watu kukichukia chama bali kuwagawa wao na waanze kuchukiana wenyewe...Leo watu wanazungumzia zaidi Uislaam na Ukristu na wapo tayari kuchukua hata silaha wauane, lakini wameshindwa kuelewa kwamba vitu hivi havitokei pasipo sababu na kuna mkono wa mtu..
Kanisa limechomwa Mbagala hadi leo hii hatuwajui walochoma isipokuwa watu wanashabikia kukamatwa kwa Sheikh Ponda ambaye ni bangusilo kuondoa hasira za wakristu lakini wahaini wenyewe are still at large, unsolved case watu wametulia. Yalipoanza kuiva bungeni tumeyaona ya Zanzivar, chuki inazidi baina ya watu wenyewe na sasa imefikia mahala ambapo tumegawanyika vibaya sana na hakika mwaka 2015 utakuwa kielelezo cha imani za watu, mshindi CCM...
AshaDii,
But the other side of the coin is the people's willingness to change for themselves. This is the clincher. This is where it gets really tough because despite how good it could be people are very rarely willing to change for themselves.
Sijasoma makala nzima ya AshaDii nataka kulala nitaisomna kesho, ila EMT acha mara moja ku under estimate Watanzania kiasi hicho, mimi na Familia yangu CCM haina kura hata moja, subilini tu lile bomu alilolisema Lowasa liotakavyofanya kazi yake vyema.
Wengi humu licha kuwa ni wachambuzi wazuri lakini mnashindwa kufanya calculation ya wapiga kura wa 2015 ni wa rika gani. hawa hawadanganywi kwa lugha ya amani na utulivu bali wanataka kuishi kama binadamu na siyo porojo za kwamba Chadema ni chama cha ukanda wa kaskazini wakati CCM ndio ina Wabunge wengi Kaskazini, this is ridiculous.
Naamka mapema kesho nitamsoma vizuri AshaDii ndio nitoe comment zangu.
Well....!
Sidhani kama nilitegemea uchambuzi wa tofauti sana toka kwako Bi. Asha hasa linapokuja suala la CDM.....
Kwa kulifafanua zaidi swali, ngoja niliweke hvi katika ule usemi wa "changes ni mimi na wewe, Twaweza" nafasi yako ni ipi kuelekea hiyo 2015? Hichi ndio kitu cha maana zaidi kuliko vingi mtu anaweza kukujibu, kama we huamini katika mabadiliko hayo ni vipi utayaona kwa wewe kuwa sehemu ya mabadiliko? Au ukiwa umekata tamaa kama EMT, ni nini utaona?
Hiyo ni mifano yangu binafsi (inayonivutia mimi) kujitosheleza kusema kuwa ufike wakati kila mtu kwa nafasi yake aziishi harakati halisi kuelekea mabadiliko tunayoyategemea. Leo wamejitwisha ufundi wa kuchambua na kukosoa masuala mbalimbali lakini mwishoni anajifanya neutral au ameficha gamba lake la CCM!
kwa msingi huo tutakuwa tumepotoka sana kama jamii.....
Ni jukumu la kila mtu kucheza nafasi yake kwa vitendo katika kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyatamani wote. Hizi mbwembwe za kuja na chambuzi ndeefu kila kukicha kwenye hzi kurasa na kuta hazitatufaa sana, mabadiliko tunayoyatamani ni makubwa sana kuliko kile tunachofanya kila siku.
Tubadili aina ya uchambuzi tuleteane case study, naelewa sio lazima wote tuwe wanasiasa japo tunajukumu moja la kuleta mabadiliko ya kisiasa kupitia kwenye kada zetu, EMT tupe uzoefu wako unavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yako sijui ni sheria sijui ni uandishi wa habari, Nguruvi3 tupe harakati zako halisi kutokea huko ulipo, Mchambuzi tueleze uzoefu wako na harakati zako za sasa, kama kuna watu unawajenga wanafanikiwa wapi wanashindwa wapi....
Ila narudia tena kushindwa kwa CDM haitakuwa aibu au kukomoka kwa CDM peke yao tu bali kwa kila anayeujua ukweli na aliyetamani mabadiliko fulani katika jamii yetu na hakuchukua na kucheza nafasi yake. Tuache na tupunguze mbwembwe za uchambuzi wa nadharia uliokithiri twende kwenye uwanja wa mapambano kila mtu achukue nafasi yake kujenga dhamira ya mabadiliko na watu wake kuelekea 2015.
CHANGES NI MIMI NA WEWE, TWAWEZA!
Hata CCM nao wanapokea OIL CHAFU SANA kutoka CHADEMA mfano Juliana Shonza na Masalia wenzake.