Kwa muktadha huu "URAIS" ni wa CCM 2015...

Kwa muktadha huu "URAIS" ni wa CCM 2015...

Eh Asha, kwanza pole na pilika.... naona ulipotea hasa hadi mnakasha ukapoaaaa....

Haya karibu, tuendelee!

Nafasi yangu ipo Gwalu, this is one of them… Painting the picture as I see it whether kwa pen ama maneno. Ni watu wengi ambao wanacheza nafasi kubwa katika kuleta change waliogawanyika katika makundi ya wale ambao watajulikana kwa changes wanazochangia na wasiojulikana… Inaweza kuwa at a small scale but bado nafasi yake ipo.

Labda mapema kabisa niainishe kuwa ninaposema mabadiliko namaanisha nini!!
Namaanisha mabadiliko ya kimfumo wa kiutawala, kwa maana kwanzia kwenye uongozi wa kisiasa ambazo kwa sasa zinaongozwa na CCM.....
Na bila kumumunya maneno, kwa muenendo wa siasa zetu za sasa natangaza maslahi kabisa kuwa mabadiliko hayo ni kutoka CCM kwenda CDM....

Ok, sawa hii ndio nafasi yako, na mimi nilikuuliza baada ya kusoma thread nzima ipo katika mitindo ya uchambuzi wa siku zote kutoka kwa "vichwa" wetu wa siku zote lakini mwisho wa siku inakuwa ni maandishi tu ya mtu ambaye kama anaeleza as yeye hana cha kupoteza kwamba mabadiliko hayo yaje yasije kwake sio ishu sana maisha yanaendelea kama kawaida ....

Hii si sawa tena wapendwa, nchi ipo kwenye hali mbaya sana kuliko juhudi tunazochukua za kuandika tu na kukosoa tu, natoa wito twende mbele zaidi.

Labda sasa wewe unipe mwanga… Unaposema kuwa siyo haki kuyajadili mabadiliko na hali siyo mpanganaji wake na hapo hapo ukiamini kuwa Change evolves kila mmoja kucheza nafasi yake inakuwaje hapo? .

Bold Red: Hiyo ni kweli kabisa Asha, we unadhani ni haki kujadili kitu usichokiamini?

Na nimekuhukumu kama huamini katika mabadiliko ambayo wengi tunayatamani kutokana na andiko lako.....

Bold Blue: Hivyo ndivyo kanuni ya kijamii juu ya mabadiliko ya aina yoyote ndio maana nikakupa kibwagizo cha Twaweza, lakini kwa hiyo kuwa kanuni haimaanishi kuwa mara zote ndivyo inavyokuwa na mfano halisi ni jamii yetu ya Tz wengi wetu tunadhani kuna watu wanajukumu la kuhangaikia hayo mabadiliko huku wengine wakiwa mabingwa wa kukosoa tu...

Nadhani hapo umenielewa hapo!!
Take note, kila mmoja na kila part ina umuhimu… Mtendaji, Mtendewaji, Mkosaji, Mkosolewa; na hakuna kinachoweza boreshwa bila kukosolewa… hayo yote yanafanya uwepo wa kitu ambacho kinaguswa kwa kila namna kuwapa nafasi wale ambao wapo interested kuelewa kwa kina zaidi bila kujali kama ina matokeo hasi ama chanya.

Natambua hilo, tena sana!!
Ila kwa mda sana wachambuzi wetu naamini hawajatambua namna wanavyoweza kuiathiri jamii kwa maandishi yao...
Naamini katika kukosoa kwa kuboresha, na pia naamini katika kukosoa kwa kukatisha tamaa....

Katika hali yetu kama taifa, mbele ya mfumo wa chama tawala ulioshindwa kwa karibia miaka 55 (hadi 2015), ni tunakuwa watu wa ajabu kama tunaendelea na ukosoaji kukatisha tamaa hasa.

Matokeo hasi yanakuwa mabaya sana sababu wananchi wanawaamini sana waandishi na wachambuzi na hivyo wana nafasi kubwa ya kuyumbisha msimamo wa wananchi.

Kuna namna nzuri zaidi ya kukosoa bila kukatisha tamaa na kuwajenga wananchi kuwa ni wana nafasi zaidi katika kushiriki mabadiliko kwa kuviunga mkono vyama vya siasa mbadala (sio lazima iwe CDM)
Nikutahadharishe thou... Ukiliangalia hili bandiko kwa jicho la kusema kuwa "Hutegemei uchambuzi tofauti na huu toka kwa mtoa mada sababu inahusu tu CDM" then kwangu naona unapotoka kiasi. Sababu kama you have read it accordingly utaona haihusu CDM peke yake, inahusu CCM, CDM na Wananchi.

Well hapa Jukwaani tumetengeneza jamii yetu, hivyo tunafahamiana kwa sauti za maandishi yetu na michango yetu.....
Kwa bahati mbaya hilo na namna ya theme ya bandiko husika ikanihalalisha kusema nilivyosema...

Marazote ninaweza kutarajia aina ya michango yako hasa linapokuja suala la CDM, hiyo ni kweli kabisa wala siwezi kumumunya maneno Asha ila sidhani kama ni dhambi kwa wewe kuwa na huo mtazamo ulionao.....

Nimelisoma bandiko lako lote zaidi ya mara moja hivyo naelewa ninachojibu na namaanisha.
Pia umekiri kuwa kuna upande linahusu CDM hivyo hapo ndipo nilipoingilia.......

Ni kitu gani ambacho kinampa mtu ruhusa ya kuchambua kitu kisiasa ndiyo maneno hayo yapewe uzito? Hivi mfano haya mawazo yangu hayatakiwi kwa mtu ambaye ni mwana CCM atoe hadi awe CDM? Hizi shutuma za mtu "Kujifanya" kunawiana vipi na topic at hand (regardless ya hii ama nyingine? - Labada iwe ya kizushi ama yakucheza dimba); Siamini na wala sidhani kuwa we are pressured ni kitu gani ama upande upi tunasimamia. Kupata ujumbe vema na kutambua kama ni wa msingi ama lah usiwe affected na aliyetowa yupo upande upi... Uwe affected na uongozwe na mantiki.

Hapo labda hujanisoma, kikubwa wakati najenga hoja katika post yangu ya awali nilikuwa najaribu kuangalia kwa ujumla mwenendo wa wachambuzi wetu wa masuala yetu ya kisiasa, hivyo haikuwa na maana ya moja kwa moja kuwa ni wewe "unajifanya" japo labda nayo inawezekana....

Pole kama hapo ulikwazika buddy!

Pia ishu ya "kujifanya" inaweza ikahusika na mjadala husika kama mchambuzi akiwa na lengo la kukatisha tamaa na kuvuruga harakati zinazoendelezwa na chama asichokipenda - CDM-!!

Upande wa mtu anapotoka unaathiri mjadala sana tu ndio maana kuna case za watu kuwa bias kwamba kuna vitu vingi mtu ana-overlook either kwa kujua au kwa kutokujua sababu hana taarifa za kutosha kutoka upande wa pili ambao hana maslahi nao sana. Na hichi kimekuwepo kwenye mijadala mingi tu.
Ndio maana mwanzo nikasema sio haki kuhumu mabadiliko ambayo huyaamini au hukubaliani nayo!
Suala la kupotosha jamii… Kuna suala Matola kagusia hapo ambalo nimelipenda saana. Kuwa watu wanaelewa ni nini wanataka na huwezi kuwadanganya kwa kuwaambia kitu ambacho sicho kwa kufanya ndicho.

Enhe umemtaja Matola, afadhali, sababu hata mimi bandi lake nimelipenda sana na kuna kitu alinifurahisha pia...

Ngoja tuone Matola alisemaje:

Sijasoma makala nzima ya AshaDii nataka kulala nitaisomna kesho, ila EMT acha mara moja ku under estimate Watanzania kiasi hicho, mimi na Familia yangu CCM haina kura hata moja, subilini tu lile bomu alilolisema Lowasa liotakavyofanya kazi yake vyema.

Wengi humu licha kuwa ni wachambuzi wazuri lakini mnashindwa kufanya calculation ya wapiga kura wa 2015 ni wa rika gani. hawa hawadanganywi kwa lugha ya amani na utulivu bali wanataka kuishi kama binadamu na siyo porojo za kwamba Chadema ni chama cha ukanda wa kaskazini wakati CCM ndio ina Wabunge wengi Kaskazini, this is ridiculous.

Hapo kwenye bold red ndicho kitu ninachokitamani kukisikia kwa wachambuzi wetu, ni kwa kiasi gani umehamasisha mabadiliko hata ngazi ya familia yako tu??

Tunarejea kwenye hoja ya awali kabisa...

Mengine nadhani ndugu yangu Matola kaeleza vizuri sana wala sihitaji kuongeza maana nitaharibu
HATUWEZI na wala HAIWEZEKANI kutegemea mafanikio bila kujitafakari, kutafakariwa na wamazo wa watafakari hao kujulishwa bila kujali wame ku Criticise ama Lah. Suala la kuona mawazo yaliyowakilishwa ni mbwembwe sababu tu huyapendi ama kutoyakubali ni aina ya udhaifu wa kutotaka ona mabaya ya li/yale ambayo unataka yaonwe kwa uzuri tu. Kama uliweza kuyasoma mawazo ywa wanaharakati waliotowa uchambuzi kama huo wa Samson Mwigamba (as per your say) na ukavutiwa na kupenda, ni hivyo hivyo ambavyo inabidi utazame upande wa pili wa shilingi ikitokea hujapenda hayo mawazo.

Naamini katika kukosoa, nategemea sana tafakuri makini zote.....
Ila msisitizo wangu umekuwa kwamba lazima tuwe watu wa kupima zaidi, hebu tuwe na huruma na taifa jamani.....
Mfumo wetu wa utawala tulionao umetosha sasa tunataka hatari gani zaidi ili wote tuje pamoja kusema kuwa "kwa gharama yoyote ile CCM must go" ??

Wote kama taifa tukikubaliana kuwa acha tuipumzishe CCM kama anavyosema Dr Rwaitama, ndio tutajua kuwa ni aina gani ya ukosoaji kunahitajika bila kuathiri harakati za kupigania hayo mabadiliko!

Nimekuwa nikikubaliana na chambuzi nyingi tu na za aina mbalimbali, ila kwasasa nimebadilika natamani aina mpya ya uchambuzi, watu twende kwenye field tupime zaidi moja kwa moja kutoka kwa watu na sio chambuzi zinazotokana na kusoma machapisho na mabandiko tu ya habari.
JouneGwalu… Kuna mambo mengi sana nimegusia hapo. Naamini ningeelewa vema zaidi ungenijuza kabisa kua AshaDii, hapa sikubaliani napo kwa sababu hii…. But kwa kugeneralise kuwa there is no need of a long analysis…. Ni suala ambalo sikubaliani nawe. For kwa kweli ni suala ambali nitaendelea kufanya.

Nililenga kwenye uchambuzi kwa ujumla sababu umenipa platform pa kuanzia juu ya chambuzi za aina hii.....

Na wala sijaribu kukuzuia na chambuzi zako ila tu nilikuwa natamani uone namna mpya na nzuri zaidi ambayo itakuwa na msaada chanya kwa taifa kufikia mabadiliko...
Katika masuala ya mabadiliko... Hapo nilipo bold... Hivi imagine JouneGwalu said:
EMT[/B], Nguruvi3, Mchambuzi na mimi mwenyewe pamoja na wengine wote wahusika tukifanya hiyo kazi ya kuleta threads za kila mmoja kutoa maelezo ya change anayofanya na mafanikio... Itakuwa interesting kweli? Sijui, but mie naona sidhani... Zaidi watu hawatachelewa kusema you are braggin na siyo kweli.

Mpaka kufikia hapa ni lazima tukiri kuwa wengi wetu tuna vipaji vya uandishi, hivyo kwa vipaji hivyo kuna namna nzuri tu ya uwasilishaji namna ya kila mtu anavyoshiriki katika harakati zake na namna chanya zaidi ya kusukuma mwamko juu ya umuhimu wa mabadiliko, kuwa wananchi ndio wana nguvu, suala la kuitoa CCM madarakani sio ugomvi wala chuki ila ni mchakato muhimu tu wa kijamii kuwa wanaweza wakawaweka CUF/CDM/NCCR na wasipofikisha matarajio yao wakabadilisha tena na tena..... Hilo tu!

Na hakika itakuwa interesting sana sababu itabadilisha namna ya watu wetu kufikiri kuwa kuna watu wanajukumu la kuhangaikia mabadiliko na wengine ni wanasubiri tu na wengine wanakosoa tu na wengine wanakatisha tamaa.....

Na pia hapo sijamaanisha wote wawe wanasiasa ndio maana nikapambanua kila mtu na eneo lake, na chama chake cha siasa kama ni mwanasiasa na hata kama sio mwanasiasa ni sawa tu una cha kutuambia basi hata ngazi ya familia yako tu kama Mkuu wangu Matola alivyoonyesha hapo juu japo kwa udogo!!
Hii paragraph ya mwisho sasa ndiyo nimekupata vema kwa hapa. Umesha fanya conclusion kuwa bandiko linahusu kuwa Chadema ishindwe na kuwa nataka hivyo. Sincerely... Naomba soma upya the whole article toka neno la kwanza to the final fulstop.

Hapana kumbe hujanipata kabisa!

Kuna sauti inayosikika kwenye maandishi yakona wachambuzi wetu wengi kama mtu usiye na nafasi yoyote katika kupigania mabadiliko.
Na kweli hichi kitu ni tatizo la jamii nzima kuwa suala la mabadiliko linaonekana kama ni la CDM (au vyama vyote makini vya upinzania) peke yao, na kwamba wengine ni watu ambao wapo tu na kuwa hawana cha kupoteza, na hiki ndio kimekuwa kitu kingine kinachopelekea ugumu wa kuwatoa CCM pengine kuliko sababu nyingi ulizo eleza kwenye thread....

Narudia tena kusema kuwa nimesoma sana thread yako tena zaidi ya mara moja na nina uhakika na majibu ninayokupa, na nadhani ndio majibu nitakayokuwa natoa kwa chambuzi zote zenye urari wa namna hii popote pale nitakapokutana nazo.
All in all nakubaliana na wewe... Change ni mimi na wewe. And this is my part in this... Nadhani umesikia kuwa hata Mwenyekiti wa Taifa Chadema -Mheshimiwa Mbowe katangaza kuwa sasa hawapokei tena wanachama wa CCM kwa muda huu uliobaki hasa wenye niya ya kwenda huko sababu tu wanaona kuwa CCM wanachemka. (Not the exact words but same meaning); Hivyo ina maana yawezekana kabisa mimi kama mmoja wa wengi walio wa 'Criticize' CDM katika hilo tayari tumecheza nafasi yetu kama wapambanaji. Asantw kwa mchango wako.

Nashukuru kwa kukubali!

Sawa hii ni part yako, na una haki ya kuona inavyokupendeza ila jamii hii yetu ya watanzania inawatamani sana watu wenye bongo kubwa kama zenu. Ndio nimesema bongo kubwa, nakutaja wewe na nina amini unaweza kwenda mbele zaidi ya hapo na kuiponya hii nchi!

Sihitaji kujenga insha nyingine kukuonyesha jinsi taifa linavyoanguka katika nyanja zote karibia, nadhani kama watu tuliojaaliwa neema na Mwenyezi Mungu kuwa katika mwanga wa kuona Dunia inavyoenda basi tupo kwenye nafasi ya kuona kuwa kama taifa tunaelekea kuangamia zaidi kwa mwenendo huu wa uendeshaji mambo wa CCM.....

Sijui tunasubiri hatari gani zaidi ili tukubaliane kuwa tubadili mfumo wa utawala??

Sijaribu kukuambia uhamie CDM kama huo sio utashi wako kwa jinsi ulivyokifuatilia na kukiona, ila ninachokuomba ni kuwa mda wa kuamini katika CCM umetosha for the sake ya watoto na wajukuu zetu, hilo tu...!

Mmmmhhh unaona sasa? Mbowe alisema eti sababu huko CCM wanachemka???

Una haki zote za ku-critisize tu hadi mwisho ila kwa niliyoeleza nadhani unakubaliana na mimi kuwa sina tatizo na mtu ku-critisize ila nawashauri na nyie mpanue vyumba zaidi sababu mna uwezo zaidi ya huo na jamii inawasikiliza sana na mna nafasi katika kuwayumbisha.

Nashukuru kwa kupokea mchango wangu, pia nashukuru kwa kunijibu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,

Nakubaliana na yote uliyowakilisha… Umegusia masuala ya msingi sana… Masuala ambayo yanabeba suala moja la kutokujitambua kwa wananchi wenyewe. Mara nyingi huwa nasema kuwa tatizo siyo viongozi tu… Hata wananchi pia. Haiwezekani hata kidogo kuleta change kwa manufaa ya nchi na wananchi kwa kutegemea watu wacheche ambao ni viongozi. Wazee wa busara zao na wanaphilosophia wa mageuzi wanasema hayo katika maandiko yao juu ya mabadiliko kwa manufaa ya jamii. Hili naona limegusiwa pia na wadau mbali mbali katika hili bandiko.

Katika hili la ‘Udini’ ndiyo balaa kabisa! Wananchi hatuoni wala hatuambiwi, na wala hatutaki kutafakari inakuwaje tuna matatizo mengi ambayo yanaweza liangamiza taifa yakuwabana viongozi badala yake tupo busy kuchukiana na kushutumiana wenyewe na kuwapa Viongozi nafasi na unafuu wanao taraji.

Nina haya juu ya Udini ukipata nafasi naomba upitie (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...katika-nafsi-na-nafasi-zetu-juu-ya-udini.html), na naomba nirudie maneno niliyo yanukuu hapo ya Mahatma Gandhi kuwa "The most heinous and the most cruel crimes of which history has record have been committed under the cover of religion or equally noble motives"

Taking the above in consideration unakuta kuwa with a combination of all the disadvantaging factors I mean it on the topic head of the thread.
 
Last edited by a moderator:
Nimeona masuala kadhaa kwenye mada ila la kusema Mbowe atajiuzulu ccm ikishinda sidhani kama ni sawa. Nilivyomuelewa mimi ni kuwa 'kama cdm ikipungua Bungeni...' Na huo ushindi wa ccm utatokana na wingi wa kura au rafu kipindi cha kuhesabu kura? Hapo dada hukutolea ufafanuzi.
 
AshaDii;

Je kuna uwezekano wa kupatikana kwa serikali ya mseto au umoja wa kitaifa mwaka 2015? Kwa maoni yangu naona kama ushindi wa 51% unaweza kuleta ubishi wa matokeo iwapo wapigaji kura wa miji mikubwa watapigia upinzani.

Kama vyama vya upinzani vinaweza kupata 60% DSM, 70% Arusha, Mwanza 70% n.k. Sidhani kama ushindi wa 51% unaweza kuisadia CCM.

Mkuu Zakumi,

Kama nilivyogusia hapo chini kwa kiasi kikubwa yote yatategemeana tokana na Uamuzi wa upinzani (in this case assumption kubwa ipo reliant na Chadema). Sijaelewa wao Chadema wanaweza kuwa wamejipanga vipi na maamuzi yao yanaweza kuwa vipi. Hapa option zinakuwa tatu;

  1. Kukubali matokeo na kupotezea - Na tukumbuke kuwa kwa Chadema Uraisi; it's either 2015 or likely never.
  2. Kukataa matokeo na pengine kushtaki tume itakayosiamamia matokeo (ambayo I really hope itakuwa huru katika marekebisho haya ya katiba) kama alivyofanya Odinga - but everybody knows hapo inakuwa suala la Uraisi kuukwaa kwa wakati huo inakuwa imetoka.
  3. Kukataa matokeo on the condition kuwa iwe serkali ya iwe Serkali ya Umoja - na kukubali kula matapishi yao wenyewe.

However again tatizo linatokea hivi:

Chadema walishakana wazi suala la GNU wakiliweka hilo wazi kabisa pale ilipokuwa kama mbadala kwa Zanzibar pale CCM na CUF walipounda umoja huo kwenye uchaguzi mkuu uliyopita. Hiyo sababu siyo siri na tumekuwa tukiona mara kwa mara baadhi ya wadau wa CDM wakiita muungano huo kama ndoa (ya mke na mume); CCM wanaweza chukua advantage na kuonesha ni wapenda 'Amani' kwa ku propose muungano huwo na Chadema (Take note: Endapo tu CCM watapata kura kati ya asilimia 50-58/60).
 
Labda mapema kabisa niainishe kuwa ninaposema mabadiliko namaanisha nini!! Namaanisha mabadiliko ya kimfumo wa kiutawala, kwa maana kwanzia kwenye uongozi wa kisiasa ambazo kwa sasa zinaongozwa na CCM..... Na bila kumumunya maneno, kwa muenendo wa siasa zetu za sasa natangaza maslahi kabisa kuwa mabadiliko hayo ni kutoka CCM kwenda CDM....

Nashukuru saana Pal. Na kwa mara nyingine tena nimechelewa tena J Kikubwa ni kuwa tufike, siyo lazima kwa haraka but we will reach the destination.

Gwalu, nimekuelewa sasa. Nashukuru... Naomba nigusie kuwa huo mfumo wa kiutawala na kuendeshwa kwa mambo ndiko kunanipa wasi wasi mkubwa kwa upinzani kuweza shika nchi wasipokuwa makini sana na kuongeza strategies huku wakijitafakari nafasi, uwezo, nguvu na Jitihada zao katika kuhakikisha wanachukua nchi. Kwa mfano; Hakuna sababu yoyote ya kutokuwa na Tume huru ya Uchaguzi... Kwa kweli hakuna. Ikitokea katiba ikarekebishwa na hiyo entity haijaguswa wala kurekebishwa for the better na upinzani ukakubali uchaguzi ufanyike vivyo hivyo; watakuwa wameonyesha udhaifu mkubwa na there is no way wanaweza shinda uchaguzi kwa kura za kuchakachuliwa.

Ok, sawa hii ndio nafasi yako, na mimi nilikuuliza baada ya kusoma thread nzima ipo katika mitindo ya uchambuzi wa siku zote kutoka kwa "vichwa" wetu wa siku zote lakini mwisho wa siku inakuwa ni maandishi tu ya mtu ambaye kama anaeleza as yeye hana cha kupoteza kwamba mabadiliko hayo yaje yasije kwake sio ishu sana maisha yanaendelea kama kawaida .... Hii si sawa tena wapendwa, nchi ipo kwenye hali mbaya sana kuliko juhudi tunazochukua za kuandika tu na kukosoa tu, natoa wito twende mbele zaidi.

JouneGwalu, sikubaliani kuwa ni maandishi tu. Hilo nakataa… Kuna baadhi ya mambo ambayo ni magumu kujua ama kuelewa vinaathiri namna ipi iwe positively ama negatively. Tupo katika Uwanja ambao wanapita watu wa kila namna, kila sector kwa nafasi mbali mbali. Hivyo unaweza wewe JouneGwalu ukaweka wazo lako hapa na likafanyiwa kazi, na pengine likawa moja ya lililochangiwa utatuzi bila wewe ama mtu yeyote kujua zaidi ya Yule ambaye ndiye kagusa hilo suala lako.

Gwalu, sehemu kubwa ya post yako sija quote sababu nimekubaliana na mengi uliyo elezea hapo. Pamoja Saana.
 
Sijasoma makala nzima ya AshaDii nataka kulala nitaisomna kesho, ila EMT acha mara moja ku under estimate Watanzania kiasi hicho, mimi na Familia yangu CCM haina kura hata moja, subilini tu lile bomu alilolisema Lowasa liotakavyofanya kazi yake vyema.

Wengi humu licha kuwa ni wachambuzi wazuri lakini mnashindwa kufanya calculation ya wapiga kura wa 2015 ni wa rika gani. hawa hawadanganywi kwa lugha ya amani na utulivu bali wanataka kuishi kama binadamu na siyo porojo za kwamba Chadema ni chama cha ukanda wa kaskazini wakati CCM ndio ina Wabunge wengi Kaskazini, this is ridiculous.

Naamka mapema kesho nitamsoma vizuri AshaDii ndio nitoe comment zangu.

Ku-understamate Watanzania? The fact kwamba CCM haitapata hata kura moja kutoka kwako na familia yako, haina maana kuwa itakosa kura kutoka kwa familia nyingine. Kwa sababu gani? Jibu umetoa wewe mwenyewe hapo chini na kupewa like na watu kama 15 hivi:

Dar waambie kuna promosheni ya bia ukinunuwa moja unapata mbili bure uone wanavyojazana, ni mji uliojaa walevi, wazinzi na mateja.

Hawa huwezi kuamini kama wanaishi kwenye mji mkuu ila wao ni hodari wa kushabikia chaguzi za nchi nyingine (Interesting....)

Siku ya uchaguzi mkuu kama kuna eneo unaona haukubaliki wewe kawanunulie pombe kwa wingi na hakuna atakayethubutu kwenda kupiga kura aache pombe, hiyo ndio Dar DSM.

Kwa hiyo, kama wewe na familia yako hutaipigia kura CCM, tayari unawajua jinsi wapiga kura wengine walivyo na nini kinaweza kufanyika siku ya uchaguzi. Vingenevyo utakuwa una-overestimate Watanzania kwa kutumia kipimo cha familia yako.

Siyo familia zote zinazokula chakula cha aina moja. Wapo wanaokula ugali kila siku, wengine nyama mara moja kwa miezi sita, wengine hawali kabisa pamoja na kuwa wajafunga. Lakini wapo wengine wamenenepeana kwa sababu msosi kwao ni abaundant.

Nimesoma hata Lissu akilalamika kuwa ameitisha mkutano Dar lakini wahudhuriaji walikuwa wachache. Kunaweza kukawa na sababu mbalimbali za mahudhurio kuwa hafifu, but my view has always been that ni Watanzania wachache sana, wakiwemo wewe na familia yako, wanye kiu ya mabadiliko. Wengine bado hawajawa tayari.

Sijui ni Sikonge au nani alisema hapa kuwa ni mpaka tuzichape wenyewe kwa wenyewe kwanza ndipo tutashikishana adabu. I'm not condoning watu kupigana lakini kwa sasa inaonekana wazi kabisa kuwa nobody cares, kwa sababu, pamoja na wewe na familia yako kuamua kutokipigia kura CCM, wapo walio na uhakika kuwa wataendelea kukipigia CCM kura and there is nothing you can do about it.

Kwa hiyo, I can't see any change in the foreseeable feature, unless the unexpected happens. Sorry for being too direct, but it is better to face the reality than trying to avoid it every now and then halafu baadae unakuja kuwa so disappointed for something you should have realised so easily.
 
Tubadili aina ya uchambuzi tuleteane case study, naelewa sio lazima wote tuwe wanasiasa japo tunajukumu moja la kuleta mabadiliko ya kisiasa kupitia kwenye kada zetu, EMT tupe uzoefu wako unavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yako sijui ni sheria sijui ni uandishi wa habari, Nguruvi3 tupe harakati zako halisi kutokea huko ulipo, Mchambuzi tueleze uzoefu wako na harakati zako za sasa, kama kuna watu unawajenga wanafanikiwa wapi wanashindwa wapi....

Kila mtu ana nafasi katika kujenga na kufikia hayo mabadiliko tunayoyataka wote, hayo sio mabadiliko ya CDM ila tu kwa baadhi yetu tunaamini tu CDM kama njia au msingi mpya wa kujenga tena kinachobomoka!
Mchambuzi amekujibu vizuri kwenye post 27. Siyo watu wote ni wanasiasa. Pia sio kada zote zinahusiana na mambo ya kisiasa.

Hata kama tungekuwa wanasiasa au kada zetu zingekuwa zina uhusiano wowote na siasa, kuleta case study ili kueleza uzoefu watu jinsi tunavyopambana na mabadiliko huko kwenye kada zetu sidhani kama itasaidia zaidi ya kuendelea ku-politicise kila jambo tunalofanya.

Kila Mtanzania anawajibu wake kwa taifa kulingana na nafasi yake aliyonayo kwenye jamii. Lakini sidhani kama CDM ndiyo msingi mpya wa kujenga kilichobomoka. Vingenevyo utakuwa unajaribu kushift responsibility ya matatizo tuliyonayo kwenda CCM.

Ukweli ni kwamba walio-mess up siyo CCM, bali ni Watanzania kwa ujumla. Kwa hiyo msingi upo kwetu sisi Watanzania, na siyo CDM. CDM is merely a political party. Kinaweza kufa hata miaka michache ijayo lakini taifa litaendelea kuwepo.

Naamini zaidi katika utaifa kwa sababu utaifa haufi. Ni vigumu kubadilisha utaifa kuliko kubadilisha chama. Hata Chilisosi atakuambia hili. Kama taifa the day tutakayo-realise kuwa we have messed up really bad and that we need to fix these problems, then sidhani kama tutawahitaji CDM, CCM, CUF or whatever. We, the people of the United Republic of Tanzania, are the sovereign of this nation.

Lakini kama bado unasizitiza kutaka kujua uzoefu wangu wa jinsi ninavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yangu, subiri kidogo kabla ya kuaga dunia nitahakikisha kifo changu kinatangazwa hapa JF ili uweze kuhudhuria mazishi yangu ambapo wasifu wangu utasomwa. And, I'm serious about this.
 
I am in consent with almost all of your post… And I think this part I have quoted is one of the most problematic issue.

EMT… I have said it before like I will say it now. For an improved, better and developed Tanzania plus a better future for all Citizens of this generation and the next; Changes does not only rely on the Government alone, there has to be change in lot of entities, of the whole system itself… Most importantly the people's improvement of negative attitude of fear, insecurity and selfishness for the better. That is to say… It does not really matter if CCM is thrown out 2015, if we as the people of this nation will have the same attitude.

There are two things involved in expected Change by the majoriy; all these changes based on the Optimistic side rather than Pessimism.

1. That Chadema's victory come 2015 is inevitable – Which at this moment am not yet convinced.
2. The second one is dependent on the fact if indeed Chadema is the Victor of the Uchaguzi Mkuu. That peoples life will transform for the better… I am not convinced with this one either…

Yea, wapo wanaoamini kuwa kama Chadema ikishinda mwaka 2015, basi Tanzania itakuwa karibu na mbingu if not like a heaven. Lakini kama alivyosema Synthesizer kwenye thread yake ambayo imekosa hata mchangiaji mmoja https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzania-ni-watanzania-wenyewe-na-wewe-pia.html. Niongezee hapo, na mimi pia.

Nitajaribu kuelezea hili kwa msaada wa articles mbili za gazeti la Raia Mwema. Kwenye makala yao ya gazeti la Raia Mwema, Lula wa Ndali Mwananzela, wanadai kuwa tatizo la msingi ni CCM. Lakini wanaendelea kusema kuwa "Watu wanaogopa kusema hivi kwa sababu wataambiwa "wanapandikiza chuki dhidi ya chama tawala na Serikali" lakini wakati wa kukwepa kuita ukweli ukweli umeshapita. Lakini kweli hapo tatizo ni CCM au uoga wa watu wa kuhoji? Raia Mwema - Tatizo ni CCM

Lakini kwenye gazeti hilo hilo toleo la nyuma, liliandika kuwa "tatizo si CCM, bali ni la Watanzania wote." Mwandishi anahoji "kwa nini tunakubali kutawaliwa na fedha badala ya kuongozwa na busara, hekima, uadilifu, uzalendo na ujuzi wa mambo?" Mwandishi anatoa mfano wa watu watatu aliokutana nao hivi karibuni. Ni makala ndefu nita-extract tuu vitu ninavyotaka kusema.

Mwandishi anasema "Hivi karibuni nilikutana na watu watatu tofauti. Tofauti zao hazikuwa katika maumbile wala sura. Walikuwa na tofauti ya maoni. Bahati nzuri nilikutana na watu hawa kwa nyakati tofauti. Kinyume na hapo labda wangetoana macho au roho maana wote walikuwa na hoja za nguvu.

Mtu wa kwanza alikuwa mpinzani wa CCM – kwa maoni yake, CCM ni chama cha majambazi, ni chukua chako mapema, ni chama cha rushwa, ufisadi nk. Anaamini kwamba uozo wote nchini ni kazi ya CCM: Rushwa ni kazi ya CCM, kutowajibika ni kazi ya CCM, ukabila na udini ni kazi ya CCM, majanga yote yanayotokea nchini ni kazi ya CCM; anasema kwamba hata ukimwi ni kazi ya CCM.......

Wa pili ni mwana CCM. Alikuwa hana hata kandambili, alivaa matambara; aliniomba shilingi elfu mbili kumpeleka mtoto hospitali. Alikuwa anaisifia CCM kwa nguvu zake zote. Ilani ya Uchaguzi ya CCM ilikuwa mikononi na kichwani mwake. Alikuwa ameikariri yote! Alisema CCM ni chama cha kuleta maendeleo, chama cha watu na ndicho chama cha mapinduzi ya kweli. Ukiangalia kweli Ilani ya CCM ni nzuri lakini tatizo ni utekelezaji……….

Wa tatu ni mwanamageuzi. Huyu kama yule wa kwanza haipendi CCM. Imani yake ni kwamba ili nchi hii ifikie mapinduzi ya kweli, maendeleo yenyewe, ni lazima itawaliwe na chama cha upinzani. Ushawishi wa mtu huyu ulikuwa mzito kiasi cha kukubaliana naye kwamba aliyokuwa akiyasema yote ni kweli……."

Baada ya hapo Mwandishi alibaki kufikiri peke yake: " Mtu wa kwanza aliyoyasema ni ya haki na ni sawa. Mtu wa pili naye aliyoyasema ni ya haki na ni sawa. Pia mtu wa tatu naye alisema ya haki na sawa". ….

.....nilipokutana na watu wangu watatu ninaowaongelea katika makala hii,...... walisema ya kweli na haki. Nisichokubaliana ni kule kusema kwamba uozo wa nchi hii ni kazi ya CCM. Inawezekana CCM imechangia kiasi fulani, lakini chimbuko la tatizo letu si CCM!..."

Mwandishi anaendelea:

"Nina rafiki yangu ambaye ni Mtanzania. Amesomea nje ya nchi tangu akiwa kijana mdogo hadi utu uzima. Nina hakika kabisa kwamba yeye CCM haijamwathiri kiakili na kiutendaji. Baada ya masomo yake aliandika andiko zuri sana la udaktari wa falsafa [Ph.D] katika historia. Andiko lake lilikuwa changamoto chanya kwa watu wenye mtazamo wa kisasa na changamoto hasi kwa watu wenye mtazamo wa kizamani.

Nilipoisoma kazi yake nilimwandikia barua ya kumpongeza; pamoja na barua hiyo ya kumpongeza niliambatanisha orodha ya mambo yaliyojitokeza kwenye andiko lake yaliyohitaji utafiti zaidi na malumbano ya wazi ya hapa na pale. Sikupata majibu ya barua hiyo hadi leo! Kwa bahati nzuri nilikutana na rafki yangu huyo kwenye sherehe. Tulipokutana, uso wake haukuonyesha kukaribisha majadiliano kati yangu na yeye kuhusu andiko lake na barua yangu. Nilivyohisi, kama si kuwa na hisia mbaya juu yake, alitamani hata kulikana andiko lake.

Nililazimisha majadiliano. Jibu lake lilikuwa fupi na mkato: " Andiko langu nililiandika kutafuta cheti tu!" hakupenda kuongea zaidi ya hapo. Leo hii rafiki yangu huyo ana cheo kikubwa. Na kazi yake kubwa ni kukilinda cheo chake hicho kisimponyoke; hata kama kazi ya kukilinda cheo hicho itamgharimu kuitelekeza taaluma yake…….

Rafiki yangu wa pili ni mwanasheria, huyo naye kasomea nje ya nchi, hivyo naye nafasi ya kuathiriwa na CCM ni mdogo sana. Baada ya masomo naye aliandika andiko zuri. Aliandika juu ya utii, aliutukuza utii na kuupamba; kwamba kila jamii utii ni kitu bora, na ni kitu muhimu, ni tunu na zawadi ya pekee kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kosa la kwanza alilolifanya mara baada ya kumaliza masomo yake na kurudi nchini ni kushindwa yeye binafsi kuwatii viongozi wake. Aliutukuza utii, akashindwa kuishi utii! Tanzania yetu tunao watu wengi wanaofanana na rafiki yangu mwanasheria. Wanasema hili na kutenda kinyume: Wanashinda kwenye majukwaa wakikemea rushwa kumbe wao ndio wala rushwa wakubwa! Wanawakemea wakwepa kodi kumbe wao ndio wakwepa kodi wakubwa! Wanapiga vita vitendo vya ngono na ukimwi kumbe wao ndio wenyewe, huu ni uozo - hivi uozo huu ni kazi ya CCM?

Rafiki yangu mwingine ni fundi. Huyu ni fundi stadi wa kushona suti za kike na kiume. Ana wateja wengi na familia yake inaishi kwa kipato hicho. Yakiingia makambi ya maombi na miujiza ya uponyaji, rafiki yangu huyu anafunga kazi zaidi ya mwezi mzima. Hakuna tena cha wateja wala familia. Anashinda na kulala kwenye maombi mwezi mzima hadi miwili na wakati mwingine anazunguka na vikundi hivi vya maombi kwa kipindi cha miezi sita! Wateja wake wanaikosa huduma ya kushonewa suti na familia yake inakosa matunzo maana kipato kinapungua kwa vile anakuwa hafanyi tena kazi ya kuzalisha.

Rafiki yangu wa nne amepoteza watoto watatu kwa kutokuwa na imani na dawa za hospitali. Yeye anaamini katika sala na miujiza ya uponyaji. Miujiza haiwezi kutibu malaria, ni lazima kunywa dawa vinginevyo mtu anakufa!......

Ipo mifano mingi. Lengo langu katika makala hii ni kuonyesha kwamba si kila uozo unachimbuka CCM na si kweli kwamba tukibadilisha chama nchi yetu itajaa neema tele. Kuna kazi kubwa iliyo mbele yetu. Zambia walibadilisha chama lakini uozo wa Kiafrika bado ni ule ule: rushwa, uporaji wa mali ya umma, upendeleo katika kugawa vyeo, ukabila na udini. Ugonjwa ni ule ule Malawi na nchi nyingine za Afrika, ambazo zimebadilisha uongozi kutoka chama kimoja cha siasa kwenda kingine."

Chanzo: Raia Mwema - Tatizo letu ni kubwa zaidi ya CCM

P.S – Please; apologies on the delay in response.

No worries AshaDii
 
Mchambuzi amekujibu vizuri kwenye post 27. Siyo watu wote ni wanasiasa. Pia sio kada zote zinahusiana na mambo ya kisiasa.

Hata kama tungekuwa wanasiasa au kada zetu zingekuwa zina uhusiano wowote na siasa, kuleta case study ili kueleza uzoefu watu jinsi tunavyopambana na mabadiliko huko kwenye kada zetu sidhani kama itasaidia zaidi ya kuendelea ku-politicise kila jambo tunalofanya.

Kila Mtanzania anawajibu wake kwa taifa kulingana na nafasi yake aliyonayo kwenye jamii. Lakini sidhani kama CDM ndiyo msingi mpya wa kujenga kilichobomoka. Vingenevyo utakuwa unajaribu kushift responsibility ya matatizo tuliyonayo kwenda CCM.

Ukweli ni kwamba walio-mess up siyo CCM, bali ni Watanzania kwa ujumla. Kwa hiyo msingi upo kwetu sisi Watanzania, na siyo CDM. CDM is merely a political party. Kinaweza kufa hata miaka michache ijayo lakini taifa litaendelea kuwepo.

Naamini zaidi katika utaifa kwa sababu utaifa haufi. Ni vigumu kubadilisha utaifa kuliko kubadilisha chama. Hata Chilisosi atakuambia hili. Kama taifa the day tutakayo-realise kuwa we have messed up really bad and that we need to fix these problems, then sidhani kama tutawahitaji CDM, CCM, CUF or whatever. We, the people of the United Republic of Tanzania, are the sovereign of this nation.

Lakini kama bado unasizitiza kutaka kujua uzoefu wangu wa jinsi ninavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yangu, subiri kidogo kabla ya kuaga dunia nitahakikisha kifo changu kinatangazwa hapa JF ili uweze kuhudhuria mazishi yangu ambapo wasifu wangu utasomwa. And, I'm serious about this.

Nimekusoma Mtu Mzima....

Naamini sikueleweka sawia juu ya suala uandishi wa mifano halisi katika kusukuma mabadiliko tunayoyatamani, ila sikumaanisha kila mtu awe mwanasiasa.

Naelewa nchi/jamii inajengwa na kada tofauti-tofauti sana lakini pamoja na hilo kila kada inajukumu katika kuhakikisha kuwa jamii haiangamii, bila kujali huo uangamizi unaletwa na watu gani..

kitu cha ajabu hapa kwetu inaonekana wanasiasa wanavuruga nchi na haionekani kama kuna kada nyingine inaweza kuzuia hilo au hata kupambana na hilo, hapo sijui shida yetu ipo wapi hasa!!

Narudia tena sikumaanisha wote tuwe wanasiasa ndio maana kama ukinisoma nilipotaja jina lako nilijaribu kubashiri aina ya shughuli zako nikasema iwe ni "sheria" au "uandishi wa habari"... yote hii nilikuwa najaribu kukwepa tafsiri hii kuwa wote nawasukumia kwenye siasa.

Na pia ndio maana nilitangaza maslahi na imani yangu mapema ila haikumaanisha nataka wote tuwe na imani moja, natamani kila mtu awe na imani tofauti ila katika kuikomboa Tanzania yetu japo kila mmoja wetu apigane na adui wetu namba moja ambaye ni mfmo wa utawala na uongozi.....

Hicho ndicho nilichokimaanisha Mkuu wangu, kama hamna hadithi ya kutusimulia nalo ni sawa tu ila kwa upande wangu nimeona aina hiyo ya uandishi na uchambuzi wa vitu case study umekuwa mzuri sana na kuvutia hisia na una nafasi sana katika kuathiri hadhira kwa haraka zaidi katika kile unacholeanga kuwaambia sababu itakuwa wazi sana kuwa sio tu unaijua nadharia bali pia unaijua na changamoto za kimazingira halisi ya hicho unachokieleza!

Pia naamini katika Utaifa, na sijajitilia shaka juu ya uzalendo wangu juu ya Taifa hili, naipenda sana nchi yangu Tanzania.

Lakini Bro, wote tunajua kuwa katika jamii yoyote ile hata wanyama kuna kuwa na mfumo mahsusi wa kujisimamia na kujiongoza katika masula yote yahusuyo tamaduni zao, mipaka yao, imani zao na rasilimali zao katika kujenga namna tarajiwa ya kila mwanajamii husika atatarajiwa kuenenda, huu mfumo ndio unaozaa kitu kinaitwa siasa.
Lakini kitu cha kusikitisha sana hapa kwetu kwasababu ya siasa mbovu tu za fitina, mizengwe, ufisadi na ubabaishaji wa siasa zetu zinazoongozwa na chama tawala CCM basi kumekuwa na kundi kubwa sana la watu (hasa wasomi)ambalo haliamini tena siasa kwa ujumla na wala hawataki kusikia kitu juu ya siasa..... Mi sikubaliani na hicho kitu na huwa naishiwa nguvu kabisa ninapokutana na mtu wa mitazamo hiyo.

Hata Baba wa Taifa alipata kusema ili taifa liweze kusonga linahitaji vitu 4 ie Watu, Ardhi, Utawala bora na Siasa safi.....

Sasa hebu niambie Bro, huo utaifa unaousema unasimamia kitu gani pasi na siasa??

Mfumo wa siasa haukwepeki sababu ni kitu amabcho chenyewe ni kinaelezea utaratibu wenu tu.
na pia mfumo wa sasa wa dunia ni kuwa vyama vya siasa ndio vinaongoza harakati za kisiasa sasa labda hapo baadae kama utakuja utaratibu mpya wa bila vyama vya siasa na kukawa na utaifa tu (hata mimi sipati mantiki hapo)......

Siasa mbovu zimedumaza taifa hili na ni Siasa Safi tu ndio zitakazo tukomboa toka hapa, na sisemi kuwa CDM wataleta siasa safi hapana ila nina imani jamii hii ya kitanzaia ikifundishwa kuwa yenyewe ndio yenye nguvu ya kuvibadili vyama vya siasa kwa utashi wao kwamba kesho wawaweke CDM, kesho kutwa CUF, mtondogo NCCR nk nk nk huo ndio muelekeo wa kujenga siasa safi maana vyama vitauogopa umma.

Hizi ndio hatua za kitaifa zaidi wazalendo tuzichukue badala ya kususa na kuamini katika nadharia zinazoelea tu!!
 
Mkuu Zakumi,

Kama nilivyogusia hapo chini kwa kiasi kikubwa yote yatategemeana tokana na Uamuzi wa upinzani (in this case assumption kubwa ipo reliant na Chadema). Sijaelewa wao Chadema wanaweza kuwa wamejipanga vipi na maamuzi yao yanaweza kuwa vipi. Hapa option zinakuwa tatu;

  1. Kukubali matokeo na kupotezea - Na tukumbuke kuwa kwa Chadema Uraisi; it's either 2015 or likely never.
  2. Kukataa matokeo na pengine kushtaki tume itakayosiamamia matokeo (ambayo I really hope itakuwa huru katika marekebisho haya ya katiba) kama alivyofanya Odinga - but everybody knows hapo inakuwa suala la Uraisi kuukwaa kwa wakati huo inakuwa imetoka.
  3. Kukataa matokeo on the condition kuwa iwe serkali ya iwe Serkali ya Umoja - na kukubali kula matapishi yao wenyewe.

However again tatizo linatokea hivi:

Chadema walishakana wazi suala la GNU wakiliweka hilo wazi kabisa pale ilipokuwa kama mbadala kwa Zanzibar pale CCM na CUF walipounda umoja huo kwenye uchaguzi mkuu uliyopita. Hiyo sababu siyo siri na tumekuwa tukiona mara kwa mara baadhi ya wadau wa CDM wakiita muungano huo kama ndoa (ya mke na mume); CCM wanaweza chukua advantage na kuonesha ni wapenda 'Amani' kwa ku propose muungano huwo na Chadema (Take note: Endapo tu CCM watapata kura kati ya asilimia 50-58/60).

AshaDii;

Nimekupata kwa ufafanuzi huu. Lakini nadhani makamanda wakipata nafasi, watajiunga kwenye GNU. Kwa nchi kama Tanzania yenye kuendesha kwa mashinikizo ya wahisani, sidhani kama watakuwa tayari kususa.

Kwa wenzetu mliopo viwanjani, je uchaguzi ukifanyika leo ni asilimia gani ya watu watapigia chadema katika kila mji mkubwa kama vile DSM, Mwanza, Arusha, Mbeya n.k.
 
Raia Fulani... Nimetafuta saana hiyo makala na nimetoka kapa. Ilikuwa ni Juni mwaka jana katika gazeti la Mwananchi. Hiyo habari ipo siyo kwamba nimebahatisha. Hata hivyo nitaendelea kutafuta nikiipata naipachika hapa.

EMT... Nimekusoma pal... Thanks for your insightful input of which most I agree on.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kauli ya mbowe kuhusu kujiuzulu iwapo ccm itashinda 2015 ilitoka kwenye gazeti la mwananchi early june 2013 kwani nilikuwa arusha kipindi hicho na nakumbuku nilisoma gazeti hilo..nadhani nakala pia ipo kwenye google.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kauli ya mbowe kuhusu kujiuzulu iwapo ccm itashinda 2015 ilitoka kwenye gazeti la mwananchi early june 2013 kwani nilikuwa arusha kipindi hicho na nakumbuku nilisoma gazeti hilo..nadhani nakala pia ipo kwenye google.

Mkuu Mchambuzi, mie nimeitafuta sana sijafanikiwa. Ukipata nafasi haijalishi ni lini tafadhali naomba msaada wa link hiyo iwe kwa manufaa ya wote ambao wapo interested. Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:
Asha Dii we chama gani? Usije ukasema uko objective kwenye hili unalozungumzia
 
I am in consent with almost all of your post… And I think this part I have quoted is one of the most problematic issue.

EMT… I have said it before like I will say it now. For an improved, better and developed Tanzania plus a better future for all Citizens of this generation and the next; Changes does not only rely on the Government alone, there has to be change in lot of entities, of the whole system itself… Most importantly the people's improvement of negative attitude of fear, insecurity and selfishness for the better. That is to say… It does not really matter if CCM is thrown out 2015, if we as the people of this nation will have the same attitude.

There are two things involved in expected Change by the majoriy; all these changes based on the Optimistic side rather than Pessimism.

1. That Chadema's victory come 2015 is inevitable – Which at this moment am not yet convinced.
2. The second one is dependent on the fact if indeed Chadema is the Victor of the Uchaguzi Mkuu. That peoples life will transform for the better… I am not convinced with this one either…

P.S – Please; apologies on the delay in response.
AshaDii, napenda nichangie post hiyo ya mkuu EMT kama ulivyomnukuu hasa point 1 na 2 hapo chini.

1.
A)Kuhusu ''CDM victory is inevitable'' nadhani kwa hali ilivyo hilo sasa halipo. Halipo kwasababu CDM kama chama cha upinzani na chama kikuu cha pili nchini kimeshindwa kuonyesha kuwa kinaweza kwenda katika uchaguzi kikiwa kimebeba sera zake vema. Sera za CDM zinaelezwa na viongozi na wanachama. Kwasasa kuna Majemadari wawili au watatu na sijui wapi jeshi liliwahi kwenda vitani likiongozwa na Majemadari tofauti wenye maono tofauti.
Kwa vile CDM imeshindwa kujisahihisha yenyewe kwanza, hiyo ni fursa nzuri kwa CCM kuwamaliza.

B) CDM wameshindwa kubeba agenda zinazotoka kwa wananchi. Mfano ni suala la katiba ambalo kwa nguvu ya wananchi CDM walipewa jukumu. Nadhani tunajua kuwa wameshindwa kulisimamia na hivyo kukasimu madaraka kwa CCM
Huu ni uchungu mkubwa kuusikia lakini ndio ukweli na usemwe.

C)CDM imeshapoteza confidence ya wananchi kwa kiasi kikubwa sana. Sijui nani anaweza kuamini suala la CDM kupambana na rushwa kubwa ikiwa imeshindwa kutia nidhamu ndani ya chama chao wenyewe kama suala la vijana wa sekondari kukiyumbisha chama kana kwamba hakina uongozi.

2.Kuhusu hoja kuwa CDM wakishinda maisha ya watu yatabdilika hili naomba kutofautiana sana.
Sidhani kama kuna silver bullet ya kusafisha uchafu uliopo kwa miaka 2 au 3. Hivyo ni ukweli kuwa maisha yanaweza yasibadilike katika kiasi kilichotarajiwa.

Muhimu si maisha, nadhani kwanza ni kujenga msingi wa kubadilisha maisha. Msingi huo ni kuondoa monopoly,bureaucracy and status quo ambayo ni kikwazo kikubwa sana cha kiubadili maisha ya watanzania.
Bila kujali chama gani kitaiondoa CCM nadhani kuiondoa CCM ni muhimu sana na hilo lazima tusimame nalo.

Kuna mifano mizuri sana. Zambia wamejaribu na sasa wamefaulu. Hawakufaulu kubadili maisha wamefaulu kutoa ujumbe kuwa uongozi ni dhamana na wala si haki na hatimiliki ya kikundi fulani katika jamii. Leo kiongozi wa Zambia anajua kuwa kinyume na matakwa ya wananchi, he or she is out. Na wananchi wa Zambia waliokuwa waoga kama wa Tanzania wameona kuwa it is poosible kuwa na serikali taofauti bila kuathiri uslama na amani ya nchi.
Hili lazima tuliingize katika bongo za Watanzania kwanza.

Na mfano mwingine ni wenzetu Kenya. Licha ya matatizo yanayowakumba lakini wamefanikiwa na hakika wanapiga hatua kweli kweli. Serikali iliyoko madarakani inajua fika wakati unakuja they will either remain or voted out.

Nimalizie kwa kusema kwangu mimi nani atatawala siyo muhimu sana than breaking the back of camel.
Sasa hivi nchi ipo katika vegetative state, na ili kuweza kuwa na evolution lazima kwanza tuondoke katika hali ya vegetative. Hatuwezi kuondoka katika vegetative state kama CCM itaendelea kuwepo madarakani.
 
... Tactics Chafu?
... AshaDii, Why call them Chafu? Is it real?!
 
Nakubaliana na kipengele hiki kabisa. Na ni kipengele ambacho ningependa kusikia wadau wa Chadema hapa jamvini kama Petro E. Mselewa, Sikonge, Mwita Maranya na wengine wanauchukulia vipi maoni haya.

2.Kuhusu hoja kuwa CDM wakishinda maisha ya watu yatabdilika hili naomba kutofautiana sana.
Sidhani kama kuna silver bullet ya kusafisha uchafu uliopo kwa miaka 2 au 3. Hivyo ni ukweli kuwa maisha yanaweza yasibadilike katika kiasi kilichotarajiwa.

Muhimu si maisha, nadhani kwanza ni kujenga msingi wa kubadilisha maisha. Msingi huo ni kuondoa monopoly,bureaucracy and status quo ambayo ni kikwazo kikubwa sana cha kiubadili maisha ya watanzania.
Bila kujali chama gani kitaiondoa CCM nadhani kuiondoa CCM ni muhimu sana na hilo lazima tusimame nalo.

Kuna mifano mizuri sana. Zambia wamejaribu na sasa wamefaulu. Hawakufaulu kubadili maisha wamefaulu kutoa ujumbe kuwa uongozi ni dhamana na wala si haki na hatimiliki ya kikundi fulani katika jamii. Leo kiongozi wa Zambia anajua kuwa kinyume na matakwa ya wananchi, he or she is out. Na wananchi wa Zambia waliokuwa waoga kama wa Tanzania wameona kuwa it is poosible kuwa na serikali taofauti bila kuathiri uslama na amani ya nchi.
Hili lazima tuliingize katika bongo za Watanzania kwanza.

Na mfano mwingine ni wenzetu Kenya. Licha ya matatizo yanayowakumba lakini wamefanikiwa na hakika wanapiga hatua kweli kweli. Serikali iliyoko madarakani inajua fika wakati unakuja they will either remain or voted out.

Nimalizie kwa kusema kwangu mimi nani atatawala siyo muhimu sana than breaking the back of camel.
Sasa hivi nchi ipo katika vegetative state, na ili kuweza kuwa na evolution lazima kwanza tuondoke katika hali ya vegetative. Hatuwezi kuondoka katika vegetative state kama CCM itaendelea kuwepo madarakani.

Katika suala la maisha bora, hilo halipo. Hali ya nchi sasa ni mbaya sana na ipo mahututi kila mahala. Kwa ungozi wowote ambao unaweza kufanikiwa kuchukua nchi watakuwa na kazi ngumu sana ya kuweza kuiweka sawa na kuwa katika mstari uliyo nyooka; na si kwa kupatikana tu kwa uongozi mpya, bali kwa kuwa na nia ya dhati ya kuifanya Tanzania na jamii yake yote kuwa sehemu nzuri kuliko ilipo – hii ikisukumwa na Uzalendo wa Uongozi mpya.

Zambia ni moja ya nchi ambayo wananchi na Uongozi wafanana sana, na katika suala la Uongozi tofauti ipo tu kuwa Kenneth Kaunda (kupitia chama chake cha UNIP) kilipinduliwa siku nyingi na hali CCM bado imengangamala. Mfanano upo hasa kwa attitude ya wanachi… Kama tulivyo wa'Tanzania ndiyo hivyo hivyo walivyo wa'Zambian towards politics. Ushabiki ni kwa mbaali na si kwa kujihusisha kwa karibu. Ninaweza sema afadhali hata sisi tunabadilika for the better.

Kwa mtazamo wangu what we can learn from Zambian Politics;

- Upinzani kushinda uchaguzi katika Demokracia za Ki'Afrika; hakuna jipya! Mambo huwa vile vile au huwa worse. Ila naomba nisisitize kuwa ni kheri kupatikana kwa uongozi mpya ili jamii ielewe kuwa tatizo si uongozi tu mpya, tatizo ni attitude ya wananchi kwa Viongozi wao hao. Kuna usemi ukichekea nyani utavuna mabua!

- Uzalendo kwa viongozi wetu ni mdogo sana no matter atakuja na maneno yepi ya kujifanya he is for the people. Tunaona vile marehemu Chiluba alipo mpindua KK na UNIP jinsi wananchi wa Zambia walivyokuwa na furaha kuwa sasa maisha yatakuwa nafuu katika sector mbali mbali. It was not to be… Matokeo yake Chiluba hadi sasa ana rekodi ya kuwa Raisi worse, akiwa kajilimbikizia mapesa kibao ambayo ni halali ya wananchi. Pesa ambazo naamini nyingi sana zimepotea katika Overseas accounts kama ilivyokwa kwa Mobutu inapotokea vifo vyao.

- Tunasikia kila siku wimbo wa ‘Ufisadi' na kuwa kuna pesa nyingi sana zimelimbikizwa nje – ikiwa ni halali ya wananchi wa Tanzania. Kama ilivyokuwa Zambia, Chiluba alikuwa na kashfa hiyo na akafunguliwa case but ikaja ikakosa nguvu sababu tu alikuwa ni mgonjwa… Absurd. Huo ukiwa moja wa mfano I gurantee kuwa hata uje uongozi mpya HAKUNA litakalofanywa dhidi ya Uongozi mpya ama dhidi ya kurudisha pesa ambazo viongozi hao wa sasa walizoficha. Kwangu the best way would be to ensure all those watuhumiwa wawe accountable! Na that is only possible if we have a leader who has guts.

Mkuu Nguruvi3, I have this topic on Historia za Siasa za Afrika kujirudia katika nchi nyingine sina hakika kama umewahi isoma… Tafadhali pitia… https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...an-politics-historia-itajirudia-tanzania.html.

Upande wa Kenya – Naomba niseme tu kwa ufupi kuwa Kenya wapo walipo sababu ya wananchi na siyo sababu ya Viongozi tu. Tunarudi pale pale kuwa sisi kama wananchi tunastahili kubadilisha attitude zetu for the better else siku zote tutachezewa na viongozi wetu. Na mfano wa Kenya ni mzuri sana na naomba hapa nim' CC jouneGwalu kumsisitiza mtazamo wangu juu ya nafasi ya mwananchi kwa uwajibikaji wa Viongozi. Like he said ‘Change ni mimi na wewe'.
 
Last edited by a moderator:
... Tactics Chafu? ... AshaDii, Why call them Chafu? Is it real?!

Aj where have you been Pal? Siasa za Nape for instance how would you grade them aside from gutter politics? Haijalishi ni kweli ama uongo but still the same thing. Take note I stand to be corrected.
 
Ha ha ha! Bana... Does it matter? Sina chama Raia. 🙂
Kuna popote ulishaandika lolote kuhusu madhaifu ya ccm? Na ni kwa nini ccm ishinde wakati unajua fika (au hujui?) kuwa hawana tena uhalali wa kuongoza hii nchi?
 
Back
Top Bottom