Well....!
Sidhani kama nilitegemea uchambuzi wa tofauti sana toka kwako Bi. Asha hasa linapokuja suala la CDM.....
Ok sitaki kwenda sana huko ila baada ya kuwa nimewasoma sana wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa hapa JF na kwingine huko, nataka nianze na wewe kwa swali dogo tu. Wewe nafasi yako ni ipi katika "mabadiliko" au vyovyote itakavyokuwa hapo 2015??
Kwa kulifafanua zaidi swali, ngoja niliweke hvi katika ule usemi wa "changes ni mimi na wewe, Twaweza" nafasi yako ni ipi kuelekea hiyo 2015? Hichi ndio kitu cha maana zaidi kuliko vingi mtu anaweza kukujibu, kama we huamini katika mabadiliko hayo ni vipi utayaona kwa wewe kuwa sehemu ya mabadiliko? Au ukiwa umekata tamaa kama EMT, ni nini utaona?
Hizo ni pembe mbili zinazotosheleza kuwatoa kwenye uwanja wa mapambano. Sio haki kuyajadili mabadiliko ambayo wewe sio mpambanaji wake. Baada ya kuonja aina mpya ya uchambuzi wa masuala ya siasa za kwetu nimeona kitu cha tofauti sana,
nimesoma maandiko ya Samson Mwigamba na baadae nkasoma maandiko ya Anserbeth Ngulumo. Wote ni wanaharakati na viongozi wa CDM katika mikoa yao, nilichojifunza kwao ni kwamba hao ni watu wanaoueleza ulimwengu kile walichokuwa wanakisikia ila sasa wanakifanya, jinsi wanavyoshiriki kujenga mabadiliko ambayo wengine mnayatarajia kuyapima tu.
Kwenye andiko la majuzi Ngulumo alikuwa akiwapongeza makamanda wenzake wa huko kijijini kwake jinsi walivyofanikisha ushindi wa CHADEMA kwa vitongoji vya kwao huko, alieleza mengi na mpaka mwenzao mmoja aliuawa katika mapambano ila mwishoni CDM ilishinda karibu asilimia 80 au zaidi ya viti vya vitongoji huko Bukoba vijijini sijui wilaya gani hasa.
Na kuhusu Samson Mwigamba, ni mwenyekiti wa CDM mkoani Arusha, miongoni mwa hadithi yake ya kusisimua ni mjadala aliowahi kuwa nao na Mwanakijiji juu ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki, masisimuo yanapatikana kwa majibu ya Mwigamba anavyoelezea mchezo wa siasa unavyochezwa na jinsi gharama wanazoziingia katika kugharamia hayo mabadiliko ambayo watu mnakuja kuyapima.
Kwanini nimewataja watu hao??
Hiyo ni mifano yangu binafsi (inayonivutia mimi) kujitosheleza kusema kuwa ufike wakati kila mtu kwa nafasi yake aziishi harakati halisi kuelekea mabadiliko tunayoyategemea. Leo wamejitwisha ufundi wa kuchambua na kukosoa masuala mbalimbali lakini mwishoni anajifanya neutral au ameficha gamba lake la CCM!
Sasa katika namna hyo tutajadili mabadiliko kweli?
Kwa kufupisha maneno mengi ninachotaka kusema ni kuwa Tanzania/Tanganyika ni yetu sote either uwe huna chama au hupendi siasa na wanasiasa, ni ukweli kuwa nchi yetu ina hali mbaya sana kama alivyosema EMT, hvyo suala la mabadiliko ni la lazima ili kuinusuru nchi yetu kuangamia kwenye mfumo ulioifikisha hapa na ni wazi mfumo huu unaipeleka nchi pabaya, hvyo sio sahihi kufikiri suala la kufanya mabadiriko linawahusu CDM peke yao tu, na kuwa kama 2015 CDM ikishindwa basi eti itakuwa imekomoka yenyewe tu (hizi ndio fikra za wengi),
kwa msingi huo tutakuwa tumepotoka sana kama jamii.....
Ni jukumu la kila mtu kucheza nafasi yake kwa vitendo katika kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyatamani wote. Hizi mbwembwe za kuja na chambuzi ndeefu kila kukicha kwenye hzi kurasa na kuta hazitatufaa sana, mabadiliko tunayoyatamani ni makubwa sana kuliko kile tunachofanya kila siku.
Tubadili aina ya uchambuzi tuleteane case study, naelewa sio lazima wote tuwe wanasiasa japo tunajukumu moja la kuleta mabadiliko ya kisiasa kupitia kwenye kada zetu,
EMT tupe uzoefu wako unavyopambana na mabadiliko huko kwenye michakato yako sijui ni sheria sijui ni uandishi wa habari,
Nguruvi3 tupe harakati zako halisi kutokea huko ulipo,
Mchambuzi tueleze uzoefu wako na harakati zako za sasa, kama kuna watu unawajenga wanafanikiwa wapi wanashindwa wapi....
Kila mtu ana nafasi katika kujenga na kufikia hayo mabadiliko tunayoyataka wote, hayo sio mabadiliko ya CDM ila tu kwa baadhi yetu tunaamini tu CDM kama njia au msingi mpya wa kujenga tena kinachobomoka!
Ila narudia tena kushindwa kwa CDM haitakuwa aibu au kukomoka kwa CDM peke yao tu bali kwa kila anayeujua ukweli na aliyetamani mabadiliko fulani katika jamii yetu na hakuchukua na kucheza nafasi yake. Tuache na tupunguze mbwembwe za uchambuzi wa nadharia uliokithiri twende kwenye uwanja wa mapambano kila mtu achukue nafasi yake kujenga dhamira ya mabadiliko na watu wake kuelekea 2015.
CHANGES NI MIMI NA WEWE, TWAWEZA!