Kwa muktadha huu "URAIS" ni wa CCM 2015...

Ni kweli CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. ushindi wake utatokana na sababu mbalimbali ikiwemo the fact kwamba chama kikuu cha upinzania, chadema, kinaendeshwa kwa misingi ya ulaghai...
 
Kuna popote ulishaandika lolote kuhusu madhaifu ya ccm? Na ni kwa nini ccm ishinde wakati unajua fika (au hujui?) kuwa hawana tena uhalali wa kuongoza hii nchi?

Kuna kitu watu wengi wanashindwa kunipata.... HASA ambao hawataki hata kidogo kusikia kuwa CCM inaweza endelea kubaki madarakani. Mie maoni yangu yanaelemea mtazamo wangu na si Mapenzi. Siwezi thou nikaongopa na kusema nina mahaba na CHADEMA... Kama nisivyo na mahaba na Wanasiasa wengi kwa kiasi kikubwa sana sababu ukweli unabaki kuwa ni wabinafsi! Na tunaposema wanasiasa waongo kwa hapa nchini wanaongoza ni CCM mana wao ndio wanashika nchi... Kwa hilo utaamua mwenyewe uniweke kwa kundi lipi.

Pamoja na kuwa sina mahaba na CHADEMA, Natambua umuhimu wa CCM kuachia nchi na sikwepi kuona ukweli kuwa kwa sasa tukitaka Uongozi mpya uje kuwatoa wana CCM tegemezi pekee ni CHADEMA kwa sasa (Thou anything can happen in the remaining time hadi Uchaguzi Mkuu).

Sina haja ya kuongea madhaifu ya CCM - Yapo wazi kila mahala! Kuna asiye jua masakata ya EPA/Buzwagi/Melemeta (to mention but a few); Regardless kuwa CCM wana madhaifu makubwa ambayo ni janga kwa taifa, iwe nchi na wanajamii sikwepi kuona ukweli kuwa wana CCM wanatumia kila namna kuweza ku maintain nafasi ya Uongozi waliyo nayo na juu ya hayo wana vingi vinavyozidi kuwabeba kama vile vipengele vingi vya katiba ya sasa inavyokumbatia Uongozi ulipo madarakani.

Kuweza kuwashinda CHADEMA ama chama chochote ile cha Upinzani WAJIPANGE! Wajitazame na wakubali madhaifu yao ili kuweza yarekebisha! Najua wengi maneno kama ya thread yangu (Hasa wa fuasi wa Chadema wasiotaka kusikia mapungufu aidha kwa kujiamini sana OR kwa kuona kuwa hawana kabisa mapungufu) hawapendi na wala hawataki kusikia habari hizi. Cha kusikitisha wao kama wadau wa Chama ndiyo wana nafasi na influence kubwa kwa vyama vyao kufanyia kazi yale yanayostahili kufanyiwa kazi.

Call me CCM or not.. Kwa kweli I don't really care. Ninachojali ni kuwa ujumbe umefikishwa kwa kuwakilsha 'Perspective' yangu on the matter. BTW naomba niongezee kuwa Kenya kama majirani zetu ni somo zuri sana kwa wao... Kuwa maneno ya wadau na wingi wa maoni hayo kwa uzuri juu ya chama siyo ambacho huweka Kiongozi kwenye kiti. Mwish wa siku 'Kura' ndiyo determinant ya mwisho... In other words katika Uchaguzi wa majirani zetu ilikuwa inaonekana kuwa Odinga ni kipenzi cha wengi na kuwa majority ndiyo wanamtaka na kuwa angeshinda kwa urahisi ukilinganisha na Kenyatta... Kazi bado ni kubwa sana! Uzuri tu tu kuwa bado ni mapema na inawezekana kwa kujipanga vema!
 
Ni kweli CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. ushindi wake utatokana na sababu mbalimbali ikiwemo the fact kwamba chama kikuu cha upinzania, chadema, kinaendeshwa kwa misingi ya ulaghai...

Mkuu ZeMarcopolo, naomba utolee ufafanuzi... Kusema kuwa CCM itashinda Uchaguzi Mkuu 2015 sababu tu CHADEMA kinaendeshwa kwa misingi ya 'Ulaghai' na hali 'Ulaghai' huo huo ni part and parcel ya CCM - Haitoshi.

Kama hutajali naomba ufafanuzi...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZeMarcopolo, naomba utolee ufafanuzi... Kusema kuwa CCM itashinda Uchaguzi Mkuu 2015 sababu tu CHADEMA kinaendeshwa kwa misingi ya 'Ulaghai' na hali 'Ulaghai' huo huo ni part and parcel ya CCM - Haitoshi.

Kama hutajali naomba ufafanuzi...

Mkuu AshaDii,

Habari za Siku Nyingi?

Naomba kwanza nifanye marekebisho madogo kwenye swali lako.
Kwenye post yangu sijasema CCM itashinda kwa sababu TU chadema inaendeshwa kilaghai ila nimesema hiyo ni mojawapo ya sababu.

Wakati chadema inapata umaarufu, kilikuwa kiahubiri kupiga vita rushwa na ufisadi kila kukicha. Hii ilifanya watu wengi waamini chadema ina malengo ya dhati ya kupinga ufisadi. Hata hivyo tangu 2010 mpaka sasa chadema imehusishwa na ufisadi mwingi wa moja kwa moja ndani ya chama kuliko chama chochote cha siasa nchini. Hii imewaondoa chadema mioyoni mwa walioiamini na imesababisha chadema kubakia na makundi ya bendera fuata upepo na wapenda vyeo.

Ukipata fursa, tafadhali pitia kwenye thread iliyoelezea hali ya uungwaji mkono wa chadema ilivyo hivi sasa hapa
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/415932-chama-cha-kilaghai-tanzania.html

Asante kwa swali lako na tuendelee kuwa pamoja katika mjadala huu...
 
Mkuu ZeMarcopolo, naomba utolee ufafanuzi... Kusema kuwa CCM itashinda Uchaguzi Mkuu 2015 sababu tu CHADEMA kinaendeshwa kwa misingi ya 'Ulaghai' na hali 'Ulaghai' huo huo ni part and parcel ya CCM - Haitoshi.

Kama hutajali naomba ufafanuzi...
Pamoja sana Asha....

Nimelipenda bandiko lako....

Nitarudi...

Bala.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZeMarcopolo... Nimependa sana hilo bandiko lako. Naona kuna michango ya kutosha... Nitaisoma vema michango ya wadau wote kwa nafasi... Na kama hutajali nimeona niliweke hapa pia kwa manufaa ya wengine sababu inashabihiana sana na hoja niliyowakilisha hapa.

CC: EMT, Mkandara

 
Reactions: EMT

Sawasawa AshaDii, tuko pamoja.

Utakapokuwa unasoma michango ya wadau, usipitwe na jibu dhaifu la Mzee Mtei linalothibitisha jinsi alivyokataa kushiriki harakati za kupigania Uhuru na jinsi alivyokataa kujitolea kuijenga nchi baada ya uchumi wa nchi kuyumbishwa na vita vya Uganda mwaka 1979 - akajiuzulu.

Wikiendi njema ndugu yangu...
 

Habari ya siku ni nzuri Mkuu... Mambo yanaenda 50/50 hivyo Inshaallah namshukuru Mungu ni mwema. Nilienda kwanza kwenye Link... Nashukuru kwa kuiwasilisha hapa... Naamini kuwa nikiisoma nitapata mengi sana juu ya mada hii na zaidi ya hapo.

Nimekusoma kuhusu Chadema... Na ndiyo maana nikagusia kuwa pengine ilikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda Uchaguzi ulio pita kuliko hata uchaguzi huu. Hata hivyo 'Time' pekee ndio dawa ya yoote haya... Lets wait and see.


Huyo member uliye mtaja kwa "Mtei" naamini kuwa unamaanisha Mzee Edwin Mtei... Akiwa kama mzee mmoja wapo wa zamani, siamini kuwa hoja zake zinaweza kuwa dhaifu kiasi hicho... Yes; pengine mmepishana mitazamo na level za uelewa katika mada yako, but siyo kwenye udhaifu. Nitasoma, na kuangalia pande zote kwa kuamini kabisa kuwa nitajifunza toka kila upande wa member aliye changia.

Nakushukuru sana mkuu wangu... Nikutakie weekend njema na wewe pia. Pamoja Saana.
 
Pamoja sana Asha....

Nimelipenda bandiko lako....

Nitarudi...

Bala.

Balantanda... Genuinely huwa unapotea sana. Upo kama haupo. Nimefurahi kukuona na nafurahi zaidi juu ya acknowledgement zako juu ya bandiko. Hivyo nitasubiri kwa hamu input yako. Pamoja saana.
 
Last edited by a moderator:

Unafikiri disaini ya watu ambao ZeMarcopolo amewataja hawapo CCM pia?

CCM hakuna watu wanaofuata upepo?

CCM hakuna wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za kisiasa za kitaifa?

CCM haijafanya mambo ambayo yanakiondoa chama hicho usoni na moyoni mwa Watanzania wanaotaka chama kinachopinga ufisadi?

Kama hayo yanafanyika ndani ya Chadema, basi yatakuwa pia yanafanyika ndani ya vyama vingine kama CCM.

Vyote ni vyama vya siasa na wafuasi wa hivyo vyama ni Watanzania wale wale.

Kwa hiyo, suala linabaki pale pale kuwa tatizo siyo Chadema, CCM au CUF, bali ni Watanzania wenyewe.

Wachawi ni sisi wenyewe wala siyo CCM au Chadema.

Simple as that.
 

Uliyoandika yote ni sahihi, lakini umesahau kitu kimoja. In any state at any time t there can never be power vacuum. Hii inamaanisha kwamba ni lazima chama au watu fulani wawe incharge katika kuendesha nchi.

Watu hao kwa hivi sasa ni CCM. Chadema wanatafuta njia ya kuwatoa CCM ili wao waingie. Kwahiyo iwapo chadema watakuja cheaply na kutaka kuiga yanayofanywa na CCM, watawanyima wananchi sababu ya kutaka kuitoa CCM. Kadri Chadema inavyozidi kufanana na CCM ndio jinsi inavyozidi kupunguza uwezekano wa kuishinda CCM.

Angalia mfano wa footbal. Simba na Yanga. Azam ni timu nzuri na pengine hakuna kitu ambacho Simba au Yanga inafanya tofauti na Azam, lakini iwapo Azam inataka kupata washabiki wa aina ya Simba au Yanga itatakiwa kufanya kazi ya ziada.
Chadema imeshindwa kutambua hilo au kama imelitambua basi ubinafsi wa viongozi wake umetawala over jukumu walilo nalo.

Labda nitoe mfano mwingine wa mpangaji ambaye yuko kwenye nyumba inayovuja. Anataka kuhama kwa sababu hataki tena kunyeshewa na mvua. Kabla mkataba wake haujaisha na kabla hajasign mkataba wa kule anakotaka kuhamia anagundua kuwa nyumba anayotaka kuhamia nayo inavuja na mwenye nyumba awali alimwambia kuwa nyumba hiyo haina tatizo ni nzuri. Mpangaji huyu atakuwa na sababu kweli ya kubeba vitu vyake kwenda kwenye nyumba nyingine inayovuja?
 

Kwa hiyo kwako Watanzania ni wapangaji na wenye nyumba ni vyama?
 

Nakubaliana na hili... Na kwa mara nyingine nakubali kuwa tatizo ni sisi wa'Tanzania wenyewe... Poor attitudes ndiyo life style yetu.

Hata hivyo EMT it should be noted kuwa pamoja na kuwa Wananchi ndiyo tatizo kubwa, nje ya hapo vyama vya Siasa vina nafasi yake kubwa tu katika lawama; hasa katika kumchezeiya mwananchi.

From you point of opinion... Unadhani kuna hope ya kubadilika kwa attitudes za sie wa Tanzania? Unadhani ni akina nani wanatakiwa kutuamisha ili tutambue kama unavyotambua wewe kuwa tatizo kubwa ni sisi na siyo viongozi peke yake? What do you think should be done?
 
Kwa hiyo kwako Watanzania ni wapangaji na wenye nyumba ni vyama?

Hahahahahahahahahahahahahahaha mkuu huko siko kabisa.
Nimesema kuwa hakuwezi kuwa na power vacuum.
Watanzania hawawezi kuwa wapangaji ila wao ndio wanaamua chama gani cha kukiajiri.
Kama wameshakiajiri chama kimoja na kinakuja kingine kutaka kukitoa kile walichokiajiri, wanahitaji kuona added value kwenye hiki chama kipya. Wasipoiona tutaishia kwenye ile methali ya "zimwi likujualo,..."
 

Kuhusu vyama kuchukua share ya lawama sawa, lakini hivyo vyama ni artificial persons wanaongozwa na real persons ambao ni Watanzania vile vile. Au unataka kuniambia viongozi wa vyama ni foreigners?

Kuhusu kubadilika kwa attitudes za Watanzania inawezekana kabisa kama wakiamua kufanya hivyo. Lakini itabidi kubadilisha attitudes za kila kitu. Tunatakiwa kuchange attitudes zetu siyo kisiasa tuu bali kwa kila kitu.

Kuhusu ni akina nani wanatakiwa kutuamsha ili tutambue kuwa tatizo kubwa ni sisi na siyo viongozi peke yake, ni sisi Watanzania wenyewe. Tusitegemee kabisa kuwa someone will come from somewhere to rescue us. Never.

Kama nilivyosema mwanzoni watu wengi wanaamini kabisa kuwa things have fallen apart and "It is no Longer at Ease". But either they're doing nothing because they strongly believe that "A Man of the People" will come and rescue them or that "The Beautiful Ones are not yet Born".

Lakini the majority of us are afraid of "The Petals of Bloods". We're still afraid to face "The Trial of Dedan Kimathi". Kwa hiyo hata akitokezea mtu kutoka sayari nyingine atakuta wengi tayari wameshaamka lakini wanaogopa kutoka nje kwa sababu kuna kiubaridi.
 

Kwa hiyo ulikuwa na maana gani ulipotumia mfano wa mpangaji na mpangishaji.

Kisiasa unaweza kuwa sahihi kusema kuwa hakuwezi kuwa na power vacuum, and, in deed, some politicians become untouchable because of fear of any backlash occurring in a power vacuum situation. But who posses that power anyway? Politicians or the people?

Power vacuum is a myth. There is no such thing as a power vacuum that must be filled by political power. Social power, the kind made up of peaceful interactions and exchanges, is more than sufficient to create social order.

As philosopher Roderick Long wrote, "if by ‘politics' is meant the legalised oppression practiced by governments, then certainly libertarians are fighting for the abolition of politics."
 
Mkuu,

Hayo ni mawazo yangu... Nitaheshimu yeyote atakae sema sina hoja kwa hoja lakini si kwa hoja ya vioja kama uliyo acha hapa.

"Emancipate yourselves from Mental Slavery,
NON but Ourselves can Free our Minds"
- Bob Marley (Redemption Song)

 
Uchaguzi wa 2015 CHADEMA au Wapinzani hawawezi kuishinda CCM hata iweje, hata kama Uchaguzi uwe free & fair kuliko yote Duniani, bado hakuna Chama kinaweza kuishinda CCM kwa kura hapa Tanzania 2015 ni mapema mno, mimi kama kuna kitu ningeweza kuwashauri CHADEMA ni kuwekeza nguvu zote kwenye Udiwani na Ubunge, wahakikishe wanapata Madiwani wengi zaidi ili waweze kuongoza Halmashauri na Miji mingi zaidi, na hapo sasa ndio waonyeshe mfano kwa kuhakikisha Halmshauri na Miji wanayoiongoza inakuwa Mifano ya kuigwa ukilinganisha na Halmashauri za CCM, hapo ndipo sasa wanapoweza kuwapata Wananchi wengi sana na kuwahakikishia Ushindi 2020 au 2025, kwa maana watakuwa na cha kuongelea na kulinganisha!

Ila kwa hali ilivyo sasa wanaongea tu, mara Bw. Lowasa fisadi, mara sijui CCM Mafisadi, wananchi wengi wanasema hawa wanasema hivi kwa kuwa wako nje hata wao wakiingia watafanya hivyo hivyo, lkn kama wakiwa na Halmashauri labda zenye shule bora Tanzania, zinaongoza kwenye matokeo, au zinazosimamia mapato yetu vizuri, basi watakuwa na cha kutambia, bila hivyo hamna miujiza!

Kwenye Wabunge wahakikishe kwamba 2015 wana double idadi ya Wabunge wao, na hilo litawasaidia sana kuanzia 2015 kwenda 2020 kwa maana watakuwa na Sauti Bungeni na wanaweza kukwamisha mambo mengi sana yenye maslahi kwa umma Bungeni hata kuiangusha Serikali ikibidi!

Vinginevyo wakiwekeza sana kwenye kushinda Uraisi na wakaja kushindwa ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA kama tuijuavyo, kitu ambacho sio kizuri kwa Demokrasia yetu!

Na ushahidi wa haya ninayosema utaonekana kwenye Chaguzi 2014, tutaona jinsi CCM itavyoshinda kwa kura nyingi yetu macho!
 
"Emancipate yourselves from Mental Slavery,
NON but Ourselves can Free our Minds"
- Bob Marley (Redemption Song)


Have No fear for a atomic energy, 'coz NONE OF THEM CAN STOP THE TIME! How long shall they kill our prophets, while we stay aside an' look..."

UKOMBOZI WA FIKRA. Komboa FIKRA ZA MTU na miguu yake itafuata automatically! Werevu walishaona hlo zamani... Nilitaraji leo MIJADALA MIKUBWA IWE NI KWA NAMNA GANI TUTAKOMBOA FIKRA ZETU, lakini ajabu bado tunahangaika na miguu yetu wakati FIKRA MFU. Hata kama miguu itakuwa imara kiasi gani, wapo wenye imani zao watakaoliwa na simba pasi kukimbia wakiamini Muujiza utatokea simba atageuka kuwa mwanakondoo. FIKRA MFU!

Tunahangaika na kubadili viongozi wakati FIKRA za raia wengi ni Kuchukua chao mapema? Tunahangaika na kuwekeza kwenye viwanda, wakati fikra za walio wengi ubora wa bidhaa yoyote ni lazima itengenezwe na mzungu (iwe imported). Tunahangaika na mikataba mizuri ya madini, wakati Fikra za wengi ni aje atajinufaisha binafsi? Kesho huyu wa mgodini, akihongwa Vx aseme madini yaliyopatikana ni gram 10 wakati ni zaidi g 50, akatae kwa fikra zipi wakati zilizopo ni za chukua chako mapema na thamani ya mtu ni KITU chake? Je, chini ya huo mkataba mzuri hatujaibiwa bado? Kwani wanaoruhusu twiga kusafirishwa nje si watanzania sisi wenyewe? Je, ni FIKRA za wangapi haziwezi kufanya hlo? Si labda 5% tu? Wanaowinda FARU na TEMBO wetu si sisi wenyewe?

Tofauti yetu ni huyu ataiba TEMBO huyu Sungura, kulingana na nafasi zetu. Lakini wote ni sawa tu, FIKRA ZETU MFU wote ni Wabomoa Taifa, HATUJENGI! TUKOMBOE FIKRA ZETU KWANZA. Tukiwekeza 50% ya jitihada zetu katika kupigani UKOMBOZI WA FIKRA, baada ya miaka 10 tutaona tulipofika.

Tukiendelea kuimba nyimbo za Wanasiasa, mara Maisha bora kwa kila mtanzania, Nguvu ya umma, Haki sawa kwa wote, Kilimo Kwanza, Serikali ya Majimbo, Muungano wa Mkataba, n.k tutakuwa TUNAWACHEKEA NYANI SHAMBANI, atakayeshangaa kuvuna mabua anastahili KUNYONGWA.

Huwezi kuishangaa CDM leo, pasi kuishangaa CCM, na huwezi kuishangaa CCM leo, pasi kuishangaa CDM. Kwangu wao si chanzo cha Utumwa wetu wa Fikra, ila ni miongoni mwa waendelezao utumwa huo.

UKOMBOZI U MIKONONI MWETU, MIMI NA WEWE. Ni SISI.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…