Kwa mwaka 1 na miezi 9 Serikali ya Samia imeokoa Trilioni 20

Kwa mwaka 1 na miezi 9 Serikali ya Samia imeokoa Trilioni 20

Ni kwa sababu mikopo mingi umechukuliwa kwa mda mfupi ikiwemo Ile ambayo ilizuiliwa enzi za Jiwe imekuwa disbursed awamu hii so imekuza Deni kwa haraka..

But natarajia kuanzia next year Deni litaanza kupungua kidogo kidogo kwa Serikali kukopa kidogo na kulipa kingi.
Waweza tuwekea mfano wa hiyo mikopo iliyozuiwa Tofauti na wa WB?
 
Chukua makusanyo ya robo ya kwanza afu gawanya kwa 3 utakuta Ni wastani wa 2T..

Pia Kama October yamefikia 2T Ni wazi disemba yatafikia 2.5T hivyo kuja kufidia miezi mingine..

Mwisho hata makusanyo ya Halmashauri yanakua zaidi kuliko hapo awali na kupunguza mzigo kwa Serikali kuu.
Bajeti ya Tanzania ni 41 Tril

Makusanyo yake tukiweka 2T kwa mwezi inakuwa ni 24
Hiyo Deficit ya 17 inatoka wapi?
 
Mhh kumbe marehemu alikuwa anakopa mbona alisema hakopi Bali anatumia fedha za ndani? Ule uongo ulikuwa ni kwa faida ya Nani?
Yeye ma wafuasi wake ni tatizo.

Pia yeye ndo sababu deni letu linakuwa sababu alianzisha miradi mikubwa mingi ambayo huwezi izuia kwani itabidi umlipe mkandarasi, hivyo hawa nao wameona wakope wamalize tu
 
Maana yake Deni la Tanzania ni Asilimia 57 ya Pato la Taifa

Maana Pato la Taifa ni appro Tril 160
Deni ni Tril 91
Ukigawa Deni kwa GDP inaleta 56.87% ambayo appro yake ni 57%

Na hapa hatujaweka alizokopa jana.
Tukiziweka inakuwa Tril 94
 
Ukisoma mwenendo wa makusanyo yetu ni wastani wa shilingi trilioni 2 kwa Mwezi Kwa mujibu wa Taarifa ya Wizara ya Fedha.

Wastani wa matumizi kwa mwezi ni bilioni 570 Mishahara na matumizi mengineyo ya uendeshaji wa ofisi za Umma (OC). Na Fedha zinazobaki wastani wa 500bilioni zinaenda kwenye miradi ya Maendeleo na nyingine ni akiba pamoja na kulipa madeni yaliyo iva.

Sasa tujiulize hizo Fedha zinakopwa zaidi ya 20trilioni kwa miezi 21 zimetumika kwenye miradi ipi?

Ndiyo hivyo vyoo pamoja na vyumba vya madarasa vinavyojengwa? Isije kuwa tunakopa Fedha nyingi hizo kumbe zinaingia kwenye mifuko binafsi ya watawala.

Vinginevyo tuoneshwe matumizi ya hizo hela, it doesn't make any sense mahela yote hayo alafu hakuna miradi tangible ya kuonekana zaidi ya Miradi iliyoachwa na JPM
 
Bajeti ya Tanzania ni 41 Tril

Makusanyo yake tukiweka 2T kwa mwezi inakuwa ni 24
Hiyo Deficit ya 17 inatoka wapi?
Sikiliza wewe, Serikali unakusanya Pesa kutoka taasisi kadhaa sio TRA peke yake..

Unakusanya Pesa kutoka TRA, Halmashauri, Kampuni zake za Biashara na Mamlaka zingine zinazojiendesha au kujitegemea mfano Bandari na Mamlaka za Maji..

Baada ya hayo makusanyo yote deficit hufidiwa na mikopo na misaada ya wahisani.👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221018-111551.png
    Screenshot_20221018-111551.png
    153.1 KB · Views: 3
“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 61 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi). Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo nayo sawa waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo namna ya ku-run nchi (kuongoza nchi) hivi sasa deni letu ‘seventy trilioni’ (Sh70 trilioni). hivi nyinyi si wasomi ‘is that healthy’ (hiyo ni afya). Kuna siku nchi itapigwa mnada hii”
 
Yeye ma wafuasi wake ni tatizo.

Pia yeye ndo sababu deni letu linakuwa sababu alianzisha miradi mikubwa mingi ambayo huwezi izuia kwani itabidi umlipe mkandarasi, hivyo hawa nao wameona wakope wamalize tu
Huku tuendako tutaingia kwenye madeni mazito maana viongozi wameshaona watanzania wanadanganyika na miradi ya ujenzi tu ndio inaonekana ni maendeleo na vinginevyo hivyo kiongozi akiingia ni kukopa na kujenga na kuzindua miradi bila kujali kama hiyo miradi ni bubu , (white elephant) ama la maana inaonekana ili uonekane wewe ni kiongozi bora basi jenga, hivyo wanashinndana kukopa hela za kujenga
 
Back
Top Bottom