Kwa mwaka 1 na miezi 9 Serikali ya Samia imeokoa Trilioni 20

Kwa mwaka 1 na miezi 9 Serikali ya Samia imeokoa Trilioni 20

Hivi ilikuwaje kipindi cha Jiwe TRA ikitoaga report kuwa makusanyo ni Tril 1.3, 1.4, au 1.6 watu wakawa wanabisha kuwa jamaa anapika Data! ila sasahv wanasema wamepiga zaidi hatusikii zile story za ZItto kuwa wanaendelea kupika Data!!
Shida ya Jiwe Ni kwamba alikuwa anataka kulazimisha makusanyo ya kila mwezi yafanane kiasi kwamba kupika.data kulikuwepo..

Pia ukiangalia makusanyo ya mwisho wa mwaka baada ya kujumlisha na kugawanya kwa data za kila mwezi yalikuwa haya tally ndio maana walisema anapika.

Kuhusu awamu ya 6 ni.kwamba wao hitoa takwimu kila robo na ule mwezi wenye makusanyo mengi ndio huutaja peke yake,hii inasaidia kwamba Kuna Baadhi ya miezi makusanyo yanakuwa kidogo..

Mwisho Hadi Jiwe anaondoka Madarakani wastani wa makusanyo kwa mwezi ilikuwa Til.1.4.
 
Mkuu huo uchumi wako ulisoma wapi? Hivi hata unajua nini maana ya mikopo?

Kwamba kuna mikopo ilizuiliwa kipindi cha jiwe ndio imekua kuachiwa sasa hivi? Okay tukubali unachokisema, kama ilizuiliwa, hiyo aliyokopa jiwe ilitoka wapi Trilioni 36?

Kwa maelezo yako ni kwamba kuna mikopo iliacha kutolewa enzi za Magufuli halafu Magufuli alipotoka tu ikaachiwa automatiki, sio?

Aisee.
Hilo sio swala la Uchumi Ni suala la uhalisia na ukweli.

Mkopo wa WB,

Mkopo dola.mil.500 za India,

Dola mil.460 za mradi wa HEET nk nk
 
Sikiliza wewe, Serikali unakusanya Pesa kutoka taasisi kadhaa sio TRA peke yake..

Unakusanya Pesa kutoka TRA, Halmashauri, Kampuni zake za Biashara na Mamlaka zingine zinazojiendesha au kujitegemea mfano Bandari na Mamlaka za Maji..

Baada ya hayo makusanyo yote deficit hufidiwa na mikopo na misaada ya wahisani.[emoji116]
Acha siasa, serikali yetu haiwezi na hakuna iliyowahi weza timiza bajeti kama ilivyopanga
 
Mimi mwenyewe nimeshindwa kuelewa matumizi ya hiyo trilioni 20 za Mkopo.

Kwani makusanyo yetu hizo trilioni 2/mwezi zinatumika kufanya Nini?
Duu una balaa,uwe unafuatilia Bajeti za Serikali ndio utajua zinachofanya.

Soma hapa mapato na matumizi 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220614-224601.png
    Screenshot_20220614-224601.png
    53.2 KB · Views: 2
Kwa miaka 5 Magufuli alikopa Trilioni 36, wastani wa Trilioni 7 kwa mwaka.

Magufuli alipofariki mwaka jana mwezi March aliacha Deni la Taifa liko Trilioni 71.

Toka mwaka jana Mwezi Aprili hadi October mwaka huu kwa mujibu wa ripoti ya Benki kuu ya Tanzania Deni la Taifa limeongezeka kwa Trillioni 20 na kufikia Trilioni 91.

Hii ni wastani wa kukopa Trilioni 1.05 kwa mwezi, ama wastani wa kukopa Trilioni 13 kwa mwaka. Kwa miaka 4 atakayokua madarakani hadi 2025 ataacha deni la Trilioni 51 na jumla ya Deni la taifa litakua Trilioni 122

Ndugai alikua sahihi, hii nchi ipo siku itapigwa mnada.

View attachment 2441891

Serikali bonanza na episode za mikopo wazuri hawafi wanaendelea kula nchi
 
Acha siasa, serikali yetu haiwezi na hakuna iliyowahi weza timiza bajeti kama ilivyopanga
Usikariri na kulinganisha failures wako.kina Mwendazake na Samia..

Mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/22 Serikali ya awamu 6 imetekeleza bajeti kwa 95% na kuna wizara Kama ya Maji ilipewa mgao kwa 100%.

Soma hapa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220628-120243.png
    Screenshot_20220628-120243.png
    153.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220628-115959.png
    Screenshot_20220628-115959.png
    129 KB · Views: 2
Hii ni wastani wa kukopa Trilioni 1.05 kwa mwezi, ama wastani wa kukopa Trilioni 13 kwa mwaka. Kwa miaka 4 atakayokua madarakani hadi 2025 ataacha deni la Trilioni 51 na jumla ya Deni la taifa litakua Trilioni
Ni dalili mbaya, tazama November 2022 walishindwa hata kulipa mishahara kwa wakati na walipolipa walilipa kwa vipandevipande
 
Ukisoma mwenendo wa makusanyo yetu ni wastani wa shilingi trilioni 2 kwa Mwezi Kwa mujibu wa Taarifa ya Wizara ya Fedha.

Wastani wa matumizi kwa mwezi ni bilioni 570 Mishahara na matumizi mengineyo ya uendeshaji wa ofisi za Umma (OC). Na Fedha zinazobaki wastani wa 500bilioni zinaenda kwenye miradi ya Maendeleo na nyingine ni akiba pamoja na kulipa madeni yaliyo iva.

Sasa tujiulize hizo Fedha zinakopwa zaidi ya 20trilioni kwa miezi 21 zimetumika kwenye miradi ipi?

Ndiyo hivyo vyoo pamoja na vyumba vya madarasa vinavyojengwa? Isije kuwa tunakopa Fedha nyingi hizo kumbe zinaingia kwenye mifuko binafsi ya watawala.

Vinginevyo tuoneshwe matumizi ya hizo hela, it doesn't make any sense mahela yote hayo alafu hakuna miradi tangible ya kuonekana zaidi ya Miradi iliyoachwa na JPM
Hiyo miradi aliyoacha jpm aliacha na hela!? 500b ni mishahara tu kwa mwezi na hiyo ni zaidi ya miaka mi5 iliyopita,kuendesha serikali siyo mishahara tu,bajeti 41b makusanyo hardly 24b,17b inatoka wapi!?
 
Hilo sio swala la Uchumi Ni suala la uhalisia na ukweli.

Mkopo wa WB,

Mkopo dola.mil.500 za India,

Dola mil.460 za mradi wa HEET nk nk
Uhalisia upi?
Mkopo upi kutoka WB, amount ipi na iliombwa lini na imetolewa lini?

Dola milioni 500 za India bank gani, ziliombwa lini na zimetolewa lini?

Leta basi ushahidi, sio hadithi.
 
Mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/22 Serikali ya awamu 6 imetekeleza bajeti kwa 95% na kuna wizara Kama ya Maji ilipewa mgao kwa 100%.
Ni wapi yanakotoka maji hivi leo, huyo waziri wa maji ni mtu hatari sana, hizo pesa zinapelekwa kwenye miradi anazunguka nyuma kwenda kuzichukua tena
 
Mimi mwenyewe nimeshindwa kuelewa matumizi ya hiyo trilioni 20 za Mkopo.

Kwani makusanyo yetu hizo trilioni 2/mwezi zinatumika kufanya Nini?
Bajeti 41tr,makusanyo 20tr...unauliza zimeenda wapi na kwa nini tumekopa?..unapoambiwa bwawa la umeme limefika 70+% na sgr inaenda nk unadhani pesa zinatoka wapi!?
 
Sikiliza wewe, Serikali unakusanya Pesa kutoka taasisi kadhaa sio TRA peke yake..

Unakusanya Pesa kutoka TRA, Halmashauri, Kampuni zake za Biashara na Mamlaka zingine zinazojiendesha au kujitegemea mfano Bandari na Mamlaka za Maji..

Baada ya hayo makusanyo yote deficit hufidiwa na mikopo na misaada ya wahisani.👇
Unaweza kutusadia ni taasisi gani ama kampuni gani ya serikali ambayo inapata faida na kupeleka hela ama gawio serikalini?

TPA sio kampuni ya serikali, ni taasisi inayokusanga pesa kwa niaba ya serikali, TPA haifanyi biashara yoyote.

Kwenye bajeti kuu ya serikali, makusanyo ya TPA, halmashauri nk na taasisi zake zote hua yanatajwa kama mapato yasiyo ya kikodi, non tax revenues.
 
Back
Top Bottom