Tayari Tanzania, Burundi na Nusu ya Wakenya wanaisapoti Congo DR huku pia Uganda na Nusu ya Wakenya wakiisapoti Rwanda.
Wazungu ambao Siku zote hawataki Kuiona Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ikistawi wamefanikiwa Kutugombanisha na kwa Uzuzu wa Wanaogombanishwa wamekubali Kuingia katika huu Mtego wa Kimkakati.
Hivi kwa Miradi mingi ya Kimaendeleo na Kimkakati Iiliyoko katika Jumuiya hii ya EAC mnadhani Congo DR na Rwanda (Wanachama wa EAC) zikiingia Vitani hawa Marafiki zao wakubwa Tanzania hatomsaidia Congo DR au Uganda haitomsaidia Rwanda?
Mnaacha kuwa Neutral katika huu Mzozo sasa Tanzania imeamua kuchukua upande kwa Kuisaidia Kisiri Congo DR kwa mategemeo ya kupata Tenda na Fursa nyingi za Kibiashara na hata Kumegewa kidogo Madini ya Congo DR Ili yawasaidie.
Na Uganda nayo vile vile (japo Kisiri) imeamua kuwasaidia Rwanda kwa ahadi ya Kufaidika na Madini ambayo kwa 60% yako upande wa Jirani na Taifa la Rwanda na chini ya Udhibiti mzuri wa Jeshi la Rwanda.
Saaa ni rasmi kuwa Vita ya Panzi huwa ni Furaha kwa Kunguru hivyo basi Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda na kwa nchi za Tanzania na Uganda nao kuchukua upande wa Kuzisaidia ni Ushindi mkubwa kwa Wazungu ambao wametumia Akili Kubwa Kutugombanisha ili Jumuiya ya EAC isifanikiwe na waendelee Kutugawa ili tuendelee Kuwategemea huku Wao Wakitunyonya (hasa katika Rasilimali zetu) kutokana na Upan'gang'a (Upumbavu) tulionao.
Tulianza na Free Trade, kisha Customs Union, tupo njiani kwenda katika Monetary Union kisha tumalize na Political Federation ili EAC ikamilike kwa 100% ila kwa huu Upuuzi uliochanganyika na Unafiki wetu na Chuki zetu sioni Ukamilifu huu wa Kimalengo kwenda Kutimia na baadae kila nchi itaamua kuendelea na yake.
Wenye Akili tuliliona hili zamani mno.