Kwa Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda nani ananibishia kuwa EAC haiendi kufa na Wazungu kufurahia?

Suluhisho kikosi kazi kiingie misitu ya Congo Munusco ikapumzike imeshindwa Jukumu


Atajulikana anayewatuma wale waaasi

Inachosha Africa ya Waasi na makundi yanayotajwa ya kigaidi na jihadi zao za Kwenye machimbo ya Madini na Mafuta

MONUSCO popote ilipo haiendi kupigana vita yenyewe kazi kubwa ni kulinda amani, japo wanaweza tu kujilinda kama ikitokea wameshambuliwa, hiyo ni kwa mujibu wa sheria za umoja wa mataifa, ndio maana kipindi kile Tanzania , malawi na south africa ndio zilipeleka kikosi maalumu chini ya mwavuli wa SADC ili kuichapa M23 , lakini askari wa Tanzania waliokua kwenye mission ya MONUSCO iwe Goma, Beni au Beni mavivi hawakuingia direct kwenye army ambush ya SADC,
 
Kwani Rwanda akiiba hayo madini anabaki nayo?, si anawateja wake wakubwa hao uliowataja wenye ndege zao hapo?

Rwanda hana dhahabu amefanikiwa kujenga ALDANGO GOLD REFINERY ambayo ni kubwa East And Central Africa yaani process za dhahabu huishia hapo yaani kupitia hiyo refinery ataweza kupata hadi Mapato ya Dollar bilion 1.5 kwa mwaka, na dhahabu hiyo ni kutoka Congo hapo jumlisha anayoiba yeye, halafu kuna watu wenye migodi midogomidogo na ya kati watachimba Congo na kupeleka Rwanda kiwandani na kuamua kuuza tu pale pale maana tayari waliokua wanakimbilia Dubai au Canada au Australia watauzia kigali kwa bei nzuri matajiri watafungua ofisi zao kigali hivo kigali itageuka soko kubwa la kimataifa la dhahabu
 
Umeona mambo hayo, sasa Rwanda itakubali conflict iishe kweli?
 
Wanalinda vipi amani bila kupigana kwa kuzuia majeshi hasimu kupigana?
 
Hii shida itatatuliwa na majeshi ya Sadeki,, Zimbabwe, Angola, zambia
Sidhani kama majeshi ndio suluhisho la kudumu maana miaka nenda rudi hayo mapambano hayajaleta amani, ni vyema diplomasia pia itumike.
 
Kwani Rwanda akiiba hayo madini anabaki nayo?, si anawateja wake wakubwa hao uliowataja wenye ndege zao hapo?
Sasa mbona Watanzania hamuwachukii hao Wengine ila Chuki yenu Kubwa ni kwa Rwanda, Rais Kagame na Watutsi? au kwakuwa wengi wenu ukiwepo ( ila siyo wote ) hamna Akili?
 
Nikusaidie tu ( tena kwa msaada wa BBC na Nipashe ya Radio One ) kuwa Wanajeshi ( Askari ) wa Tanzania walioko MONUSCO huko Congo DR hawatakiwi na Wakongo ( hasa wa Kivu, Goma na Beni ) kwakuwa Wanaua hovyo, Wanabaka bila Aibu na Wezi wa Madini ya Wakongo huko.
 
Umeona mambo hayo, sasa Rwanda itakubali conflict iishe kweli?
Ufaransa, Ubelgiji, Italy, Russia, South Africa na Tanzania ambao nao ni Wezi wa Madini ya Congo DR nao watakubali kweli hii Vita iishe?

Mnafiki na Mpuuzi Mmoja mkubwa Wewe.
 
Tulifanya makosa makubwa kabisa kuikaribisha Rwanda ,Burundi na Dr Kongo.

Tungeungana kwanza sisi watatu halafu kila anayekuja anakuta Kuna linchi kubwa Pkweli kweli.

Kuikubali Kongo ni sawasawa na kununua kiwanja chenye mgogoro na tulivyoiingiza Burundi na Rwanda ni sawasawa na wake wenza hawawezi pendana.

Nini kifanyike maana hakutatokea mshikamano Wala Afrika Mashariki kuwa Taifa moja abadan.

Tubadilishe mtazamo, malengo kuhusu hii jumuiya.

N.B tuzikubali OGAD countries kuingia Afrika ya Mashariki.
Jumuiya iregulate kama SADC tu nothing fruit will come out
 
Sasa mbona Watanzania hamuwachukii hao Wengine ila Chuki yenu Kubwa ni kwa Rwanda, Rais Kagame na Watutsi? au kwakuwa wengi wenu ukiwepo ( ila siyo wote ) hamna Akili?
Yaani nimchukie anaenunua TV ya wizi badala ya kumchukia mwizi?! Ni muda muafaka sasa ukaacha kutumia makalio kufanya kazi ya kichwa.
 
Mpaka sasa sijajua nini EAC inafanya katika kutatua mgogoro huu!
Halafu wazungu wakiamua kuuingilia utasikia EAC,na AU,ndipo wataamka ohho,mambo ya Africa mtuachie wenyewe,wakati kwa sasa kila mtu anaogopa kujionyesha yupo upande upi,wakati mkorofi anafahamika miaka yote,Afrika ni wanafiki sana.
 
Tatizo la hizo nchi ni utawala kwa mabavu.
 
Halafu wazungu wakiamua kuuingilia utasikia EAC,na AU,ndipo wataamka ohho,mambo ya Africa mtuachie wenyewe,wakati kwa sasa kila mtu anaogopa kujionyesha yupo upande upi,wakati mkorofi anafahamika miaka yote,Afrika ni wanafiki sana.
Mkorofi ni huyo Mwizi Rwanda, tuogope nini sasa na anafahamika kila siku
 
Ilikua n makosa makubwa kuiruhusu rwanda kuingia kwene EAC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…