KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za muda huu,
Bila shaka hili sio jambo geni hata humu jamvini na linaweza kuonekana kama jambo la kawaida kulingana na wakati husika.
Ni jambo la kawaida kwa macho ya kawaida lakini kwenye masuala ya kuukamilisha uanamume mbele ya mwanamke makazi ni jambo la msingi sana mwanaume kuwa na makazi yake mwenyewe kunaweka tafsiri ya mambo mengi sana chanya dhidi yake bila kujali ubora au Hali ya makazi hayo.
Mwanaume unapokubali kwenda kuishi kwa mwanamke au ukweni kwa mkeo unakuwa umejondoa nusu ya uanamume wako sio tu kwa mkeo bali hata kwa wanao.
Tunatambua kuwa maisha wakati mwingine yanaleta changamoto za hapa na pale lakini ni jitahidi hilo jambo la makazi kulipambania mpaka dakika ya mwisho.
NB; Nimeshuhudia kijana hapa akidhalilishwa kwenye mji wa mkewe waliyezaa nae watoto watano na miaka zaidi ya 15 kwenye ndoa kwa kweli nimejisikia vibaya kama mwanaume.