Kwa nilichokiona Morogoro, ni sahihi kusema Serikali ya CCM inachelewesha maendeleo ya huu mkoa kwa makusudi kabisa!

Kwa nilichokiona Morogoro, ni sahihi kusema Serikali ya CCM inachelewesha maendeleo ya huu mkoa kwa makusudi kabisa!

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Nina mwaka wa nne kwenye huu mkoa sasa. Tangu nifike hapa kwa mara ya kwanza nilikuwa mtembezi sana, ili kufahamu maeneo, uchumi, na tabia za wenyeji wa huu mkoa.

Niligundua mambo yafuatayo:
1. Wenyeji ni watu wasio na makuu na waungwana (kama tu tabia za Wazaramo na makabila ya Pwani), ni wavivu (hilo nilithibitisha mara nyingi. Lakini huu uvivu wa hawa watu unafanya mkoa uwe na ombwe la fursa nyingi za kiuchumi, nitaieleza kwa kina)

2. Una vivutio vingi sana vya kitalii ambavyo vingeweza kuufanya huu mkoa kuwa na volume kubwa ya shughuli za kitalii kama ilivyo Arusha, lakini hali haipo hivyo.

3. Ni mkoa ambao biashara zinakuwa kwa kasi sana. Mahoteli mengi ya Morogoro yanatengeneza pesa sana na biashara nyingine zinazotesa huku ni chakula, bidhaa za mavazi, na vitu vya nyumbani. (Kwenye chakula, hii imechochewa zaidi na tabia za waluguru kuwa wavivu wavivu, kwahiyo wao kupika mara kwa mara inakuwa ngumu kidogo--wanapenda kula migahawani). Hizo biashara zimetengeneza pesa sana.

4. Ni centre nzuri sana ya kufanya manufacturing ya viwandani, kwasababu mbili kubwa kwamba ipo jirani na masoko yanayochipukia kama Dodoma, Iringa, na Mbeya. Na kuna faida ya nguvu kazi nafuu, ipo ya kutosha. Wenyeji wanazaliana kama panya.

5. Miaka 3 iliyopita manispaa ya Morogoro imeshuhudia ongezeko kubwa sana la idadi ya watu, na hii pia imechangia pakubwa ukuaji mkubwa wa biashara kwa miaka hii mitatu ilopita.

Mambo hayo yakaifanya Morogoro ikue kiuchumi mpaka leo hii ipo nafasi ya tatu kitaifa nyuma ya Dar es salaam na Mwanza, ikiwa na mchango wa Trillioni 9... kama sijakosea.

Kwa karatasi inaonekana ni performance nzuri ya kiuchumi, ila ukilinganisha na potential ya huu mkoa, ingepeswa kuwa ya pili kitaifa ikiwa na uchumi usiopungua Trillion 15.

Kwahiyo unaweza kusema: mkoa wa Morogoro ni sleeping giant. Na mimi binafsi nailaumu sana serikali ya CCM kwa hilo.

Kwanini nailaumu CCM?
Uchumi wa Morogoro, pamoja na kuwa na potentials nyingi za rapid growth ila bado umefungiwa kwenye kichumba--kwenye minyororo.

1. Ni vigumu mtu kupanda ndege ukitokea Morogoro kwenda nje ya mkoa (kwasababu hakuna uwanja wa kutua ndege kubwa). Hii kitu ilinishangaza sana kwamba, mkoa wenye potential kubwa sana ya biashara ya utalii inakosaje uwanja wa ndege mkubwa?

Ikanibidi niingie chimbo kuchunguza ni kwanini. Nilichokigundua kikanifanya niamini kwamba, kuna baadhi ya maeneo nchi hii, umasikini unatengenezwa kwa makusudi na serikali ya CCM.

Niligundua ya kwamba Morogoro hakuna uwanja mkubwa wa ndege wa kiraia kwasababu kuna uwanja wa ndege wa kijeshi wa Ngerengere. Kwahiyo nikaambiwa kwamba, ili kuzuia mgongano wa rada za kijeshi na ndege za raia basi hakutakiwi kuwe na uwanja wala ndege za abiria kukatiza hapo.

Kwakuwa sababu yenyewe ilikuwa imekaa ki-usalama basi sikutaka kuendelea kuhoji zaidi.

Lakini swali moja nililibakiwa nalo najiuliza ni hili: ina maana serikali ya CCM wanaona ni sawa tu kuifungia potential ya zaidi ya Trillioni 6 (ambayo ingeweza kuongezeka kwenye mkoa wa Morogoro), kwa kukataa kujenga uwanja mkubwa wa ndege ambao utaufungua mkoa wa Morogoro?

Ni kwanini basi uwanja huo wa kijeshi na amana zake zisihamishiwe mkoa wa Lindi ambao upo jirani na Morogoro?

Ili huo uwanja wa kijeshi wa Ngerengere ufanyiwe expansion na kuanza kutumika kama uwanja wa ndege wa kiraia. Na jeshi wao wahamie Lindi kujenga uwanja wa ndege.

Na jeshi wanaweza kufanya leasing ya huo uwanja wa Ngerengere na ikawa inakusanya mapato yote ambayo wanaweza kuyatumia ku finance huo uwanja huko Lindi.

Hilo likifanyika, uchumi wa mkoa wa Morogoro utafunguka kwa kasi sana. Sekta ya utalii, madini, kilimo na biashara vitakuwa kwa kasi sana, kwasababu hizo sekta, hapa Morogoro ndo nyumbani kwake.

Ila kwa akili ilotumika MO29, sina imani kama serikali ya CCM wataweza kufanya hili jambo kwa umakini na kwa wakati sahihi, kwasababu wakati ni sasa!

Wenu
MC
 
Morogoro wana kila kitu cha kufanya uwe mkoa tajiri sana, issue ni moja tuu, tunaongozwa na wajinga wa ccm
Upo sahihi kuwaambia CCM ni wajinga. Namimi nawatusi tena: ni wajinga!

Mkoa ni tajiri sana. Tena wewe unasema kilimo, ila kuna maeneo eneo huku yana madini, watu makini wanatengeneza hela, sema ndo hivo. Mkoa umefungwa na CCM
 
Mkoa wa Morogoro kwa sasa unazalisha mpunga kwa wingi baada ya wahamiaji kutoka kanda ya ziwa hususani Wasukuma kuhamia mkoani humu..
Inawezekana ni mkoa wenye wahamiaji wengi sana kwa sasa. Fundamentals za Morogoro zinafanana kabisa na za Dar es salaam, nadhani ni kwasababu ni mikoa ya waswahili wanaoendana.

Huku waluguru hawalimi. Anakuambia, "mimi nakula unga robo kwa siku, nilime ili iweje?" Hahahaha
 
Kuna mtu analipwa 28M kwa mwezi hapo Moro, lakini akiwa na dharura ya kwenda Dar/Dom ni kuendesha tuu.

Chief Kingalu anatakiwa aulizwe.
Moro kwa jiografia yake, ardhi yake na maliasili ilizonazo, ilitakiwa iwe numero uno kwenye kuchangia mapato kwenye kapu kuu na kimaendeleo.

Hili si kwa Moro tu, bali mikoa yote Tanganyika ni "potential kiuchumi".

CCM wanajua hili, na kwa makusudi kabisa, wanalitumia kwa kujinufaisha binafsi.
 
Mikoa yeyote au Jamii yeyote ambayo imewekeza kwenye Kilimo au Mifugo hakuna Maendeleo.

Chunguza mara mbili, Ni kwasababu ya sera mbovu za Kilimo na mifugo.
Ila tukiwa objective kwenye hoja yako. Kwahapa Morogoro inaweza kuwa tofauti kidogo na mikoa mingine--ardhi ya huu mkoa inatoa tija kubwa sana. Kwahiyo wanaojihusisha na kilimo wanapata.

Tofauti na mikoa mingine ambayo watu wanalima lakini tija ni ndogo, kitu inayopelelea wao kuendelea kuwa masikini. Hususani ukilima mpunga ekari moja Geita na ukalima ekari moja Ifakara Morogoro, tija ya Ifakara itakuwa kubwa kuliko Geita. Maana yake hapo unaona kabisa mkulima wa Ifakara atakuwa na kipato kikubwa kuliko wa Geita.

Nakubaliana na wewe kwenye sera mbovu za nchi hii. Na hata sio kwenye kilimo peke yake.

Kila sekta nchi hii kuna sera mbovu. Ndo maana malalamiko hayaishi.

Kwasababu sera ndo zinaathiri moja kwa moja vipaumbele na miradi ya kuchochea uchumi.
 
Mafanikio nilonayo, nimeyatoa Morogoro

Mlimba na Mbenja ya kipindi serikali haijawatimua wakazi wa maeneo hayo

Mwaka 2014, niliingia Mbenja nikakodisha mbuga ya mpunga hekari 60 kwa m3.

Hapo ndipo niliipigia Saluuti Morogoro, ilinipa Gunia 1400,

Kutokea hapo nilitamani kununua maeneo ya kulima mipunga huko, nikanusa harufu ya kwamba hayo si maeneo rasimi na kwamba, ipo siku serikali lazima itawafukuza wakazi wa maeneo hayo

Ilinibidi nitafute namna ya kuwashawishi wananchi ili kwamba kuanzishwe shule, tuliianzisha maeneo ya Kipingu, hata hivyo bado machale yalinicheza,

Niliondoka kuja Dar kuanzisha miradi yangu, ila Ki ukweli, Morogoro ni habari nyingine
 
Kuna mtu analipwa 28M kwa mwezi hapo Moro, lakini akiwa na dharura ya kwenda Dar/Dom ni kuendesha tuu.

Chief Kingalu anatakiwa aulizwe.
Moro kwa jiografia yake, ardhi yake na maliasili ilizonazo, ilitakiwa iwe numero uno kwenye kuchangia mapato kwenye kapu kuu na kimaendeleo.

Hili si kwa Moro tu, bali mikoa yote Tanganyika ni "potential kiuchumi".

CCM wanajua hili, na kwa makusudi kabisa, wanalitumia kwa kujinufaisha binafsi.
Inakwamisha sana. Sasa hapo kweli utamtoa mtalii aje kutembea kilometa 200 kuitafuta airport? Halafu unalalamika majukwaani watalii hawaji Morogoro. Sababu ndo hizo na zipo wazi
 
Back
Top Bottom