Kwa nilichokiona Morogoro, ni sahihi kusema Serikali ya CCM inachelewesha maendeleo ya huu mkoa kwa makusudi kabisa!

Asante kwa kuweka mfano halisia kabisa. Na kitu kingina naskia huu mkoa una makambi karibu 30 ya kijeshi, kitu kinachibitisha kwamba kila ardhi unayoigusa Morogoro unaambiwa ni ya jeshi! Au serikali wayaichukua. Kwahiyo zote hizo zinajumuika ku elevate risk factors na kuifanya Morogoro kuendelea kubaki kwenye kichumba.
 
Miaka 5 baada ya CCM kuondoka au akipatikana kiongozi mwenye akili, mikoa mingi Tanzania itakuwa na ukuajo mkubwa sana wa uchumi. Ila zaidi ya yote itakuwa ni Morogoro.
 
Uwanja wa ndege gharama sana so watoboe barabara hata ya vumbi kuunganisha moro na lindi uone mkoa utakavyotajirika ghafla, moro kuna kila aina ya chakula na soko kubwa lipo kusini ila tatizo hakuna barabara. Mfano ndizi za moro zinauzwa mia moja ila ikifika lindi moja inauzwa buku maana imepita dar
 
Ni vipaumbele tu. Kama ingekuwa hoja ni gharama mbona serikali ilijenga uwanja Chato ambao sasahivi unanyewa na popo?

Na kuhusu Moro, kama jeshi wakihia Lindi ule uwanja wa Ngerengere utumike kama uwanja wa ndege za kawaida.

Kwasababu na-assume kutakuwa na runway kwa ndege kutua na kupaa.

Hata kama kukiwa na uhitaji wa pesa, lakini haiwezi kuwa nyingi kwasababu facility ipo. Hapo labda pesa ya renovation tu kidogo
 
Maji Ya Kuchamba Koo Shida
Hahahahaa... umenikumbusha kauli ya, "kuchamba koo," alipenda sana kuitumia rafiki yangu mmoja, akimaanisha Bia. Mbona zipo tu bia huku...

Au una maanisha maji kama maji? Ambayo pia yapo tele milima ya uluguru kuna mito kule ya mwaka mzima haikauki, uzembe tu wa serikali. Plus wanasiasa wa Morogoro wamelala usingizi mzito.
 
Kule msalabani kwenye milima ya Uluguru, hauwezi kutembea 1 km bila kuvuka mto/mito. Mito ni mingi sana saana.

Kule wakilima hawajui mbolea ni nini, muda wote ardhi ni kijani. Mida ya usiku tu ukiingia ndani hasa saa 3 kwenda mbele, utasikia sauti za mito ya maji yanavyoteremka kutoka milimani.
 
Kuhusu mkoa kuwa na rada kubwa ya kisheshi ni kweli kabisa, lakini haizuiii ndege za kiraia tena nchi zote hapo ndo panakuwa salama zaidi, Ni kweli Ngerngere kuna Kizuka Air base Ngerengere ndo kambi kubwa ya ndege na ghala la silaha za jeshi la anga, pia kuna ngerengere kambi na kikosi cha makomandooo , kuna kiwanda cha silaha mzinga corporation, na kuna pangawe chuo cha maofisa, tano kulikuwa na kambi nne za siri za wapigania uhuru, wami mbiki, dakawa, chilonga, na kidatu

Mkoa wa Morogoro ndo mkoa wenye mito midogo midogo mingi kuliko mikoa yote na hali yake ya hewa inaruhusu mazao mengi sana , Kuna mabonde matano makubwa ya mpunga yanayotosha kulisha watu bilioni 3 yakitumiwa vizuri( Usije kubisha soma data za dakawa rice institute cha wakorea wao wanasema bilioni 6 ) pili ndo busu ya sukari yote Tanzania inapozalishwa, karibu umeme wote Tanzania kabla ya JNHP ilikuwa ni kitadu, mtera na kihansi na kama sio kuharibu mazingira ilikuwa tunaweza kuwa na mabwawa mengine matano kupitia kilombero, na ruaha mbuyuni

Nkianza kuelezee morogoro napata kichaaaa ni mkoa potential balaaa nimeishi hapo 1994 mpaka 2002 nikarudu 2016 mpaka 2018
 
Kabisa, maji Morogoro sio issue, ni basi tu mamlaka zinazohusika haziendani na kasi kubwa ya ukuaji wa mji ndo maana kunaonekana kuna uhaba.

Ni kichekesho sana, kukosekana maji wakati kuna maji mengi yapo mlimani hapo.
 
Hii ni chai hakuna kitu kama hichi umedanganya mchana kweupe huko ulipo pataja napajua vizuri sana. Kweli moro ni kuzuri lakini hapa umeongeza chumvi mkuu
 
Hivi mkuu kiwanja cha heka 1 maeneo ambayo sio mbali na mjini inaweza ikawa ni bei gani?
Soko la ardhi huku limechangamka sana miaka hii miwili na nusu ilopita. Kabla ya hapo kwa mwendo wa kilometa 8 au 10 kutoka centre ya mji ungeweza kupata hilo eneo kwa 15 million au pungufu kidogo ya hapo.

Ila kwa sasa, demand ya ardhi ime-shoot kiasi na bei imepanda. Lakini kwasababu soko la ardhi la Moro bado lipo local kulinganisha na lile la Dar es salaam, inakuwa vigumu kupata taarifa sahihi za bei ya ardhi.

Ila nitatafiti juu ya hili.
 
Asante kwa taarifa. Mimi mtu niliyemuuliza alikomaa kabisa kwamba hiyo rada ya kijeshi kuwepo hapo na hayo maghala ya silaha ndo imezuia shughuli zote za ndege za kiraia kupita anga la Morogoro na hata kuwa na uwanja kwa hofu ya kuzuia kupelelezwa.

Ila I wonder! US na mateknolojia yao huko angani utawaficha kitu gani dunia hii? Maana yake hizo taarifa wanazo, na wanaweza kuziuza kwa maadui wa Tanzania.

Kwahiyo hata mimi sioni logic ya Morogoro kukosa uwanja wa ndege kwa kisingizio cha ki-usalama.
 
Hii ni chai hakuna kitu kama hichi umedanganya mchana kweupe huko ulipo pataja napajua vizuri sana. Kweli moro ni kuzuri lakini hapa umeongeza chumvi mkuu
Inawezekana alivuna kwa misimu tofauti tofauti. Watu wengi kijijini wanafanya hivo. Unakuta mtu anajifungia shambani kwa misimu yake kama 6 kwa miaka mi 4 au mi 3 akitoka hapo unakuta kakusanya gunia kama 500.

Kwahuyu mdau wa gunia 1400, kwa ekari hizo 60 kama angeweza kupata hata gunia 7 kwa ekari basi hapo ni misimu mi 3 tu anakuwa amekamilisha gunia 1400
 
Amini nnawaambia, mkoa wa Morogoro ungechangamka mapema leo hii tusinge kua na Dodoma. Fuatilia hii.
Kabisa, sema kwa mapesa serikali waliyoweka Dodoma imechechemua kwa kiasi kikubwa sana ukuaji wake.

Kukua kwa kasi kwa Dodoma kumeisaidia sana Morogoro, kwa kuongeza wigo wa fursa za uchumi.
 
Kabisa, sema kwa mapesa serikali waliyoweka Dodoma imechechemua kwa kiasi kikubwa sana ukuaji wake.

Kukua kwa kasi kwa Dodoma kumeisaidia sana Morogoro, kwa kuongeza wigo wa fursa za uchumi
Serikali haijachangia kukua uchumi wa dodoma, imelazimisha.

Lakini nina uhakika Dodoma haikutakiwa kuwa kama ilivo sahizi. Na wasinge ingilia kati huu uwekezaji ambao serikali imeufanya Dodoma, raia walitaka waufanye Morogolo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…