Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Mozambique nimefika, unachosema ni kweli ni kama bado wapo miaka ya 90's hata usafiri shida tu
 
Kigali nimefika, mji msafi ila ni mdogo, huwezi linganisha na dar, ila Nairobi iko juu sana, nilifika nikakubali imejengeka kuliko dar
 
Amka usingizini, hiyo ilikuwa zamani sikuhizi makanisani kumejaa umbea na mtu anaangaliwa sadaka kama si mtoaji au hana cha kutoa anakosa sauti na anakuwa haheshimiki wala kushirikishwa kwenye maamuzi au vyeo hapati. Mtu anaangaliwa mafanikio huko makanisani mpaka maskini wanapata stress huko
 
Ukiona nchi au eneo flani la nchi lina wafuasi wengi wa dini jua vilevile kuna umasikini mwingi na hawana kazi ya kufanya zaidi ya kukesha makanisani kujiliwaza na neno la Mungu.Na ukitaka kuwa maskini kupindukia kuwa muimba kwaya wa kanisa.
 
Burundi kuwa koloni la Ufaransa?

Historia ya primary au secondary hiyo?
Burundi ilikua koloni la German East Africa pamoja na Tanzania na Rwanda, baada ya Ujerumani kushindwa vita vya 1, vya dunia, Burundi na la Rwanda zikaenda kwa Belgium iliokua ikitawala Kongo, kumbuka hao Wabelgiji wanaongea Kifaransa, kwahiyo ni sawa kusema Kongo, Rwanda na Burundi wametawaliwa na Ufaransa. N.B, Nchi ya Ubelgiji nusu ya Nchi wanaongea Kifaransa na nusu nyingine ni Kidachi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…