Kwa niliyoyashuhudia ibadani Kenya ni sahihi kabisa alichofanya Rais Magufuli kuzuia mikutano holela ya kisiasa hadi wakati wa kampeni

Kwa niliyoyashuhudia ibadani Kenya ni sahihi kabisa alichofanya Rais Magufuli kuzuia mikutano holela ya kisiasa hadi wakati wa kampeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jana nimebahatika kuhudhuria ibada katika Kanisa moja pale Mtwapa katika pwani ya Kenya, ama kwa hakika ibada iligeuka kuwa " kama" mkusanyiko wa wanasiasa.

Watu wanazungumzia nani awe Rais wa Kenya baada ya Uhuru kanisani wakibishana juu ya William Rutto, Raila Odinga na Gideon Moi.

Nilimouliza mwenyeji wangu uchaguzi wanafanya lini, akaniambia ni mwaka 2022 na kwamba Kenya nzima hata shughuli za uchumi zimerora kwa sababu kila kona mawazo ya watu yametawaliwa na mijadala ya uchaguzi.

Ndipo sasa nikaikumbuka marufuku ya Rais Magufuli kule nyumbani kwamba mikutano ya kisiasa ibakie majimboni tu tena ikihusu shughuli za maendeleo chini ya wabunge na madiwani husika tu, na kwamba mikutano mingine ya akina Polepole wa CCM na Tumaini Makene wa Chadema isubiri wakati wa kampeni.

Rais Magufuli alifanya maamuzi sahihi kabisa.

Niko njiani narudi nyumbani Tanzania, Mniombee tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
"kila Kona mawazo ya watu yametawaliwa na mijadala ya uchaguzi"!!!
huu ni uongo na hapo umetembelea Mtwapa na upo njiani kurudi hme tz.....
punguzeni uzushi wenu
 
"kila Kona mawazo ya watu yametawaliwa na mijadala ya uchaguzi"!!!
huu ni uongo na hapo unetembelea Mtwapa na upo njiani kurudi hme.....
punguzeni uzushi wenu
Uzushi upi bwashee?!

Ibada nimesali Dominica ya jana hapa nipo ndani ya Tahmeed narudi Dsm..... sasa unashangaa nini?!
 
Huu Nao Siyo Ukweli
Mbona Pole Pole Yupo Majukwaani Daily
Huko Kesho Nadhani Utakuwa Hujafika Uzuri Wakenya Wapo Humu Jukwaani
 
Uzushi upi bwashee?!

Ibada nimesali Dominica ya jana hapa nipo ndani ya Tahmeed narudi Dsm..... sasa unashangaa nini?!
Uzushi wako upo hapo nilipo quote maneno yako unapenda hesabu za kujumlisha sio.....
unetembelea sehemu moja umejumlisha nchi nzima!!!
 
Mkuu Kenya tunaenda kila siku...tunaona na kusikia....
CHAiiiiiiii..............
 
johnthebaptist, Ina maana kabla ya Rais Magufuli siasa zilikua zinafanywa makanisani na misikitini hapa Tanzania? Tuanzie hapo, kwangu mm sina kumbukumbu kama Tanzania tuliwahi kufika huko, wakenya wana namna yao ya kufanya siasa tofauti na sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu Nao Siyo Ukweli
Mbona Pole Pole Yupo Majukwaani Daily
Huko Kesho Nadhani Utakuwa Hujafika Uzuri Wakenya Wapo Humu Jukwaani
Polepole alikuwa jukwaani lini?

Bwashee usichanganye na mikutano ya ndani ambayo hata Chadema juzi na jana walijichimbia pahala wanamjadili mbunge aliyehama!
 
Ina maana kabla ya Rais Magufuli siasa zilikua zinafanywa makanisani na misikitini hapa Tanzania? Tuanzie hapo, kwangu mm sina kumbukumbu kama Tanzania tuliwahi kufika huko, wakenya wana namna yao ya kufanya siasa tofauti na sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Prof Lipumba alikuwa anajifunza kareti kwenye nyumba za ibada labda wewe ulikuwa mdogo zama hizo!
 
Mi nitakupa vipande hutaelewa,nashauri tafuta katiba ya nchi soma,tafuta sheria ya vyama vya siasa pia,ndipo utajuwa hilo unaloshabikia ni sawa au unaungana na wakandamizaji?
 
Back
Top Bottom