johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Jana nimebahatika kuhudhuria ibada katika Kanisa moja pale Mtwapa katika pwani ya Kenya, ama kwa hakika ibada iligeuka kuwa " kama" mkusanyiko wa wanasiasa.
Watu wanazungumzia nani awe Rais wa Kenya baada ya Uhuru kanisani wakibishana juu ya William Rutto, Raila Odinga na Gideon Moi.
Nilimouliza mwenyeji wangu uchaguzi wanafanya lini, akaniambia ni mwaka 2022 na kwamba Kenya nzima hata shughuli za uchumi zimerora kwa sababu kila kona mawazo ya watu yametawaliwa na mijadala ya uchaguzi.
Ndipo sasa nikaikumbuka marufuku ya Rais Magufuli kule nyumbani kwamba mikutano ya kisiasa ibakie majimboni tu tena ikihusu shughuli za maendeleo chini ya wabunge na madiwani husika tu, na kwamba mikutano mingine ya akina Polepole wa CCM na Tumaini Makene wa Chadema isubiri wakati wa kampeni.
Rais Magufuli alifanya maamuzi sahihi kabisa.
Niko njiani narudi nyumbani Tanzania, Mniombee tafadhali.
Maendeleo hayana vyama!