Pombe ni kinywaji kinacholevya na zinagawanyika katika aina mbili ambazo ni bia(iliyotokana na kuchachuliwa nafaka) na pia divai ama mvinyo(iliyotokana na matunda).Pombe nyingine ni zao la kutonesha bia ama divai. Mhubiri 9:7,inakutaka unywe divai kwa kuchangamka kwa kuwa Bwana amekwishazikubali kazi zako.Uamuzi wa dini ama dhehebu si wa kutoka katika Injili bali ni maoni ya Mtume Paulo alipoamua kuwa mnadhiri wa Mungu.Mnadhiri wa Mungu alifungwa na masharti ya kutokunywa pombe,kutonyoa nywele na kutoshuhudia maiti.Endapo mnadhiri akishuhudia maiti kuna tambiko maalum atalifanya ili kuirudia nadhiri yake.Hata wewe wawezafunga nadhiri na je,kama si mnadhiri ipendeze kuhubiri kuwa kunywa pombe ni dhambi?