Kwa nini hizi barabara za Mwendo kasi zifanye biashara?

Kwa nini hizi barabara za Mwendo kasi zifanye biashara?

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,882
Reaction score
5,087
Kuwekwe kiwango fulani cha tozo kwa Gari binafsi kwa wale wanaotaka kutumia miundo mbinu hiyo ili kukwepa kero sugu ya foleni ya jijini Dar.

Mathalani waweza kuchaji Gari dogo shilingi elfu hamsini kutokea Kariakoo au Ferry mpaka Mbezi au Kibaha au Chalinze siku wakifikia huko.

Naamini kabisa wapo wengi tu wenye uwezo na uhitaji wa kufanya hivyo badala ya kung'ang'ana tu na sheria zinazowakosesha hata pesa ya kusimamia vyema miundo mbinu hiyo. Hii pia Itakuwa ni chanzo ziada cha mapato ambayo hata yatajazia pale kunapopelea kutokana na nauli isiyokidhi wanayoilalamikia mara kwa mara.
 
Kipande cha Kimara mwisho mpaka Mbezi Magari Saba naomba usiwang’ate sikio maana huko ndiyo wengine tunaponea kupunguza viriba tumbo na kuweka afya ya akili sawa.
 
Mods nirekebishieni nilikusudia kuandika "kwa nini ziSIfanye biashara".
 
Kipande cha Kimara mwisho mpaka Mbezi Magari Saba naomba usiwang’ate sikio maana huko ndiyo wengine tunaponea kupunguza viriba tumbo na kuweka afya ya akili sawa.
Kabisa huwa mpaka najiuliza siku Wahusika wakianza kuitumia hiyo miundo mbinu yao itakuwaje?maana sasa ni kama imekuwa ndio short cut ya Watembea kwa miguu wakikwepa adha ya kupishana na Magari maana barabara hata hazina sehemu ya Watembea kwa miguu.

Na jua likizama imekuwa ndio sehemu salama kwa Watembea kwa miguu maana ni ngumu kuvamiwa na vibaka wakiwa wanatembea katikati ya barabara tofauti na kule pembezoni.
 
Back
Top Bottom